Mhe. Rais,Mkapa na Kikwete nao sasa ni 'vifaa vya kijeshi' kama MV Bagamoyo?

Nasubiri siku hiyo mikataba ikitinga bungeni, na kujadiliwa kwa uwazi, nitapaka bati za nyumba yangu rangi za kijani na kuchora jembe na nyundo.
utasubiri sana mkuu. kama wahusika wakuu mkulu kasema wasiandikwe hata magazetini je mikataba itaenda bungeni?
 
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Katiba na sheria zetu zisiporekebishwa tunachofanya hakina maana hata kidogo. Tunapoteza muda, maana Magufuli anaweza kufanya mambo mazuri lakini akaja mwingine akaharibu haya na ana kinga ya sheria mtamfanyaje? Surely we are not serious, on what we are doing. Sheria ndiyo chanzo cha haya yanayotokea
 
04bdeaff97dfae527139e730a60f6ca5.jpg

Akili kichwani mwako
Ukweli mchungu huo
 
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
MENO YA MBWA HAYAUMANI!
 
JK na BM hawaepukiki katika hizo shida wanazotuaminisha. Hakuna waziri ama AG aliyetoka nyumbani kwake kwenda kusaini hiyo mikataba. Waweke wazi muhtasari,tujue mwenyekiti aliamua nini baada ya majadiliano.

Kuwa na sheria mbovu za kuzuia watu kushtakiwa ndio kunatuleta hapa,leo nae Magu akiamua anafanya yake sie tupige mayowe tu ye apige mkwanja akimaliza muda wake untouchable. Uongozi wa namna hii unamuwajibisha vipi mtu kutenda kwa haki mbele ya raia. Yeyote awajibishwe ili kila anaepata nafasi awe mkali na makini katika utendaji wake. tunapoelekea hili litawezekana tu,nasubiri akina chenge and co. wachukuliwe hatua afu hawa waliobaki sijui kama watakubali. Siku zote hizi ndio huwa chachu kuelekea sheria nzuri hasa baada ya wao kuumizana.
 
Watanzania wengi hawajui kuwa hayo yote mnayoyaskia ni mbinu tu za serikali kutawala nchi kirahis, kwa kuwachanganyachanganya wananch na wabunge wao kama chagalawe kuwapotezea::
1. Mda wao
2. Njaa na ukali Wa maisha yao
3.fikra kwenye jambo moja ndan ya nchi
4. Hasra za upande mmoja na wapili
4. Dira yenu na kutizama dira ya mtawala
6. Akili timamu ili muwe kama wendazimu ili mtawalike kirahsi
Kiufupi mnapigwa sarakasi za kisiasa!
Tumieni akili timamu kufkri na kutafakar mambo sio kusubri matokeo ya jambo flan kisa limeanzishwa!
 
Tupo kwenye mjadala wa madini. Kichwa cha habari ni MAKINIKIA. Mjadala umepamba moto. Tunakumbushana,tunasemana,tunatajana na kurekebishana. Kwa upana wa kitaifa.

Lakini,Rais na Mawaziri wako wawili wa Sheria na Katiba pamoja na yule wa Habari mmepunguza uwanja. Uwanja wa majadiliano. Mmekataza kutajwa kwa Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwenye mjadala.

Nakumbuka kivuko cha MV Bagamoyo nacho kilijadiliwa. Kuhusu ununuzi wake na matumizi yake. Rais ukatufunga mdomo kwa kukikabidhi jeshini. Ukatuambia kuwa sasa kimekuwa kifaa cha kijeshi na ni risk kukijadili. Tukanyamaza

Je,Mzee Mkapa na Mzee Kikwete nao wamekuwa vifaa vya kijeshi na hivyo hawajadiliki? Waliotajwa tuwajadili?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Serikali imetaharuki. PhD3 (mbili zikiwa za sheria) zinatufundisha demokrasia. Inanikumbusha Kenya miaka ya 1970's Njonjo alipiga mkwara kuwa kufikiria Mzee Jomo atakufa au kuwaza tu nani atamrithi ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifo (Sir Charles Njonjo wakati huo alikuwa Attorney General)
 
Magufuli anajishushia tu heshima yake.Mnafungia gazeti kwa sababu limemtuhumu Mkapa na Kikwete kwa wizi? Magufuli is not serious at all! This is "it cant be!!"
Kwani kamati za rais ndio zimechimbua kila kitu? Kwamba hamna other source of information nje ya hizo kamati mbili?
MATUMANI HEWA SAWA NA MAISHA BORA HEWA KWA KILA MTANZANIA
Hamna cha kupigana vita wala nini .
Huyu Magufuli ni msanii tu tena usanii wenyewe ni ule wa kizamaaani.

Akadanganye wajinga
 
Ukiwakuta wanaongea kwa hisia unaweza kufikiri wameguswa na wameumizwa sanaaaa kumbe unafiki mtupuu.Hajui maskini nchi nyingine marais wastafu wamefungwa,kwingine bado wanakesi za kuharibu walipokuwa madarakani.hawa wakwetu wameharibu uchumi wetu kwa usimamizi mbaya wa rasilimali zetu tushindwe tu hata kuwataja hata kwa sababu za kuwafundisha watawala waliopo na wanao kuja umuhimu wa kufanya vizuri wanapopata nafasi kwa sababu kunakuulizwa baada ya kumaliza kutumikia nafasi zao,nako ni kosa?Ma rais wa Tanzania wamekuwa watakatifu kiasi cha kutokukosolewa wakitoka madarakani?,2020 waondoke hawa watu mweeeee angalau tubadilishe hata stori za kuongea.
 
Anakiogopa kivuli chake na cha wastaafu!!! Mwanzoni alimsema JK kuwa amefanya mambo ya hovyo (uzinduzi wa Maktaba UDSM) leo amekomaa anawalinda kwa nguvu zote maana yeye pia ana mikono michafu.... nyumba na meli mbovu ya jeshi!! Ahhahahaha
Kuna kipindi Sizonje zinamruka na kujiona mtakatifu hasa akiona kamera baadae zinarudi akikumbuka alivyohifadhiwa madudu yake.
 
Ukiwakuta wanaongea kwa hisia unaweza kufikiri wameguswa na wameumizwa sanaaaa kumbe unafiki mtupuu.Hajui maskini nchi nyingine marais wastafu wamefungwa,kwingine bado wanakesi za kuharibu walipokuwa madarakani.hawa wakwetu wameharibu uchumi wetu kwa usimamizi mbaya wa rasilimali zetu tushindwe tu hata kuwataja hata kwa sababu za kuwafundisha watawala waliopo na wanao kuja umuhimu wa kufanya vizuri wanapopata nafasi kwa sababu kunakuulizwa baada ya kumaliza kutumikia nafasi zao,nako ni kosa?Ma rais wa Tanzania wamekuwa watakatifu kiasi cha kutokukosolewa wakitoka madarakani?,2020 waondoke hawa watu mweeeee angalau tubadilishe hata stori za kuongea.
CCM CCM CCM CCM CCM CCM CCM CCM . . , CHAMA CHA MAJAMBA&1 . . .
 
Mzee Tupatupa,

Nimekuwa najiuliza kwa nini huu mjadala wa makanikia uanzishwe wakati huu wa bunge la bajeti ilhali ungekuwa ni wakati muafaka kwa wananchi kufuatilia na kufahamu jinsi serikali ilivyotekeleza bajeti ya 2016/17 ili waweze kupima utendaji wake?

Naona hii hadithi ya makanikia imefunika kabisa bunge la bajeti. Je hii imepangwa kiujanja au imetokea tu?

Naona kuna goli la mkono hapa!
Na Mimi nimeliona!
Unajua yawezekana bajeti hii ikapitisha vitu vya ajabu sana maana watu wameshindwa ku-focus kabisa!
 
Back
Top Bottom