Mhe. Rais Kikwete, Onesha mfano... maneno matupu hayatoshi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,694
40,720
Imeripotiwa hivi karibuni kuwa Rais Kikwete ametaka wale wote wanaofuja fedha za serikali wafikishwe polisi badala ya Taasisi ya Rushwa au kuitwa kwenye vikao vya nidhamu. Maneno hayo yamesifiwa na vyombo vya habari vya bongo na baadhi ya watu ambao upeo wao wa kufikiri umetiwa kiwingu na kutangaa kwa Mhe. Kikwete. Hata hivyo, siyo wote ambao ni vipofu!!

Mhe. Rais,

a. Ulipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, je kuna fedha zozote ambazo zilipotea "kiana"? Je kuna mtu yeyote chini ya iliyokuwa wizara yako ambaye alituhumiwa kufuja fedha za umma? Kama yupo, je huyo mtu amefikishwa polisi?

b. Katika nafasi yako ya sasa kama Rais wa JMT, je kuna mtu yeyote ambaye chini ya ofisi ya Rais ametuhumiwa kufuja fedha, na bado yupo kwenye nafasi yake hiyo? Je uko tayari kumsimamisha mtu huyo na kumfikisha polisi ili uchunguzi ufanywe?

c. Je kati ya mawaziri na viongozi kadhaa uliowateua tangu uchukue madaraka kuna yeyote ambaye chini ya uongozi wake kiasi cha fedha kimepotea bila maelezo ya kutosha? Je uko tayari kumsimamisha mtu/watu hao kutoka nafasi hizo ili polisi wafanye uchunguzi na ikibidi afikishwe mahakamani?

Mkono mtupu haulambwi!! na maneno matupu hayavunji mfupa!!!!! Onyesha mfano badala ya kutuzuga!!!! Kama hauko tayari kuonyesha mfano usitegemee wengine wafuate!!!!

Thanks you!!!
 
mheshimiwa mwanakijiji,

kama wewe ndie yule mwenye podcast nianze kwa kukushukuru kwa ujumbe wako maridhawa ambao huwa unautoa katika hizo, i am a great fan na keep it up!

Nasikitika umeshindwa kuelewa context ya mazungumzo ya Rais kwa vile alichosema na ndio maana kimepokelewa vizuri na waandishi wa habari ni kile alichosema kwamba kwa sasa sheria za sasa zilizopo zina walakini hazina meno ya kutosha kuwang'ata wale wanaoshukiwa kuhusika na ubadhirifu wa pesa manake kwa sasa ni utaratibu uliopo ni kwamba ubadhirifu ni suala la kinidhamu kazini hivyo mtu akituhumiwa kwa upotevu wa mamilioni basi atasimamishwa kazi uchunguzi uendelee na kisha ikija kubainika basi atafukuzwa kazi sheria ichukue mkondo wake, katika utaratibu aliorecommend sasa ni kwamba mtuhumiwa wa ubadhirifu na wizi wa fedha za serikali atakuwa chini ya uchunguzi wa kosa la jinai meaning atapelekwa ndani na kisha polisi kufanya kazi yake.

Hii inaenda sambamba na hatua za waziri mwapachu kuhakikisha polisi wanakuwa na elimu ya kutosha na meno ya kutosha kung'ata penye uhalifu, kwa sasa polisi wana udhaifu mkubwa katika kushughulikia makosa/uhalifu wa kisomi kwa vile wengi ni beyond elimu wanazoweza baini wizi wa namna hii.

Rais pia aliwahi kusema kwamba atahakikisha PCB inapewa nguvu za kutosha kupeleka kesi mahakamani wao wenyewe na sio kupeleka jalada kwa DPP ili kufungua mashtaka hii ni kuongeza urasimu usio na maana.

Ama kuhusu mifano:
Yes inawezekana wakati akiwa waziri wa mambo ya nje fedha zilipotea kiaina, tumewahi kusoma kuhusu missing milllions katika balozi kadhaa, lakini mara alipoingia urais kafanya nini, yupo balozi amefutwa kazi, ni costa mahalu aliekuwa italia huyu anashutumiwa kula takriban bilioni moja kaondolewa kabisa katika utumishi serikali na sasav PCB wanawork out on how to recover the money and sue him.

Tangu kawa rais amekuwa akielezea namna anavyoweza kudeal na rushwa kivitendo lakini huwezi kuanza kufukuza watu, rushwa imejikita ndani mno ya jamii kiasi ukisema uifute basi waweza ondoa serikali nzima au at least unaweza kuboggy step, the best way ni kudeal na mianya ya rushwa be it in terms of sheria dhaifu, watendaji dhaifu au kuimarisha mamlaka husika.

Kama unavyojua serikali yetu imekuwa na uwezo mdogo wa kulipa wafanyakazi wake hivyo inakuwa vigumu kwa wafanyakazi wenyewe kujizuia na chauchau hivyo moja ya mbinu zinazotumika hivi sasa ni kuanzisha executive agencies yaani ofisi ambazo zipo chini ya usimamizi wa serikali lakini zina semi autonomy ya kujipangia baadhi ya viwango vya mishahara, ndio maana utaona taasisi kama hizo mfano, TRA na Customs sasa hivi mishahara ni mikubwa kwa watumishi na opportunities nyinginezo hivyo mambo ya rushwa siwezi kusema hamna bali yamepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Next in line ni kuondoa kabisa mashirika ya biashara katika usimamizi wa serikali manake mengi yamekuwa yakifa kwa sababu uteuzi wake ulikua ni wa kisiasa zaidi kuliko ujuzi hivyo huko nyuma tulikuwa tunapata watu wanaongoza mashirika ya biashara kusoma balance sheet hawawezi! Sasa hivi serikali imefungua milango kwa wataalamu wajiunge na mashirika waweze kuongoza. Katiba inabadilishwa kuhakikisha rais anaondolewa madaraka ya kuteua watu wengi, manake kwa sasa ni rahisi kwa rais kuteua mtu asiemjua manake wewe mwenyewe angalia rais ateue mawaziri na manaibu na makatibu wakuu na mabalozi na manaibu katibu wakuu, maRAS ma DC na Marc na wakuu wengine wa mashirika mengi zaidi wakati ingekuwa wanachaguliwa kwa sifa watu hawa ingekuwa poa zaidi.

Kwa hiyo mwanakijiji mimi nasema ni mwanzo mzuri tumpe rais muda na tufuatilie kwa makini maneno yakioanishwa na vitendo, if not utaniona tena hapa nikicomment kwa kukubaliana nawe!
 
Kwikwikiw tafiti bwana .Sitaki kuamini kwamba ni mwanamtandao wa JK ila maneno yako na ulinzi ama utetezi wako bwana .Ni mawazo yako ni mazuri ila mimi siamini kitu hadi vitendo vifanyike nani asiye ijue CCM kwa kuandaa ripoti ama taarifa nzuri kuanzia serikalini hadi kwenye Chama ? Zinaishia wapi ? Naomna kuungana na mwanakijiji kwamba JK fanya vitendo kama kweli u mean it .Ok kasema wacha tungoje tuone nini kitafuata . Swala la Mahalu liache hakuna kitu kinaendelea pale bwana yote ni mazinga ombwe Mahalu hana njaa kapoa tu na hatashitakiwa wala nini .Tuombe uzima utayaona mwenyewe .
 
RAISI ALIDAI ANA USONGO NA WALA RUSHWA NA HASIRA ZAKE TUTAZIONA KARIBUNI. NI MIEZI MINANE SASA.

Hakuna sheria au utaratibu ambao hautakuwa na matatizo ya hapa na pale. Kulingana na hoja ya Mtafiti, DPP ndiye kikwazo kwa PCB kushitaki wala rushwa. Je, kwanini asiteuliwe DPP mpya na apewe maelekezo ya kushighulikia mafaili ya PCB kwa nguvu zaidi, na kasi mpya. Where is the President who did his home work??!!

Kwa upande mwingine hivi tumeshajiuliza wachumi wetu wanaochambua faida za kiuchumi na mikataba tunayosaini wanafanya kazi gani? Mimi nafikiri matatizo ya hii mikataba yako katika mgawanyo wa mapato na faida, si siyo utekelezaji "sheria."

Ninachojaribu kusema ni kwamba kazi ya mwanasheria ktk hii mikataba ni kuweka vifungu vya sheria vinavyomlazimisha mwekezaji kutupatia gawio kama ilivyoshauriwa na wachumi wetu. Kama tunaona tunalaghaiwa basi tuwahoji wachumi wetu.

sasa inawezekana labda wachumi hawashirikishwi, na shughuli ya kuandaa mikataba inaachiwa wanasheria peke yao. Kama ni hivyo basi hayo ni makosa makubwa.
 
Nina wasi wasi nyie watu wa hadhara hii hamna kazi ya kufanya sasa.Swala la JK kufanya yale ambayo tulidhani anaweza ni ndoto Kesha sema na si mara moja wala 2 kwamba yeye anafuata yale aliyo yaanzisha Mkapa na kuyaacha mengine haya aliyo bahatika kufanya ni baada ya kuona hana namna . Sasa mnasikiliza mbwembwe za semina endelezi wazee ? Wacha anunue madege na matukutuku ila pesa za wanafunzi kukopeshwa hawana na Nchi ni masikini ilapesa za kukaa Ngurdoto wiki nzima zinapatikana .
 
tafiti,
You should know that kesi ya Mahalu is CLOSED. Wameshasema hakuna ushahidi wa kumpeleka mahakamani. IT IS OVER KWENYE AWAMU HII. Halafu umaposema tumpe muda unamaanisha nini? Tufunge midomo yetu mpaka amalize urais hiyo miaka mitano au vipi? Mimi ninavyojua rais akipewa lungu anatakiwa kuanza kulitumia siku hiyo hiyo. Tulipokuwa BCS, ni mimi na Mzee ES ndiyo pekee tuliojitokeza hadharani wakati wa kampeni kumpigia debe kwamba anafaa ukilinganisha na wengine. Kwa upande wangu nilimpigia debe siyo kwa sababu kwa rekodi yake ya utendaji wa kazi ila kwa sababu kulikuwa hakuna mtu mwingine ambaye niliona anaweza kuwa rais kutoka kwenye vyama vya upinzani. Hakuna hotuba ambayo ilinifurahisha kama ile aliyoitoa bungeni na nilikuwa najua ile hotuba ndiyo itakuwa dira ya uongozi wake lakini kama alivyosema Mwanakijiji tunashuudia maneno matupu bila matendo ni kibaya zaidi watanzania wanapenda maneno tu.
tafiti, kama wewe umo ndani ya serikali mnatupa hofu kubwa, umesema katiba inabadilishwa mbona wananchi hawahusishwi labda uniambia kuna mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yanaandaliwa.
 
Mzee sam heshima yako man

Swala la JK kusema haya yote kwangu nasema ni impossible kwanza historia inaonyesha kwamba alichuka Urais kwa rushwa na majungu na pia mweka hazina wake wa pesa chafu Kingunge na wengine wote ndiyo wamemzunguka wakiwa na kila aina ya miradi michafu nje na ndani ya Serikali . Angalia akina Karimagi etc leo anaweza kusemama lolote ? Anaongelea rushwa iliyo jificha kashindwa kumkemea karimagi mwenye madai kwamba JK anamtaka yule Mhindi kuwa mwekezaji na yeye Karimagi pia anamtaka ? Pesa za huyu Mahalu zilimsaidia JK kuukwaa Urais kila mmoja anajua leo anaweza kusema lolote ? Poleni sana
 
bwana mkubwa murangira

naomba uthibitisho kwamba jk aliingia kwa rushwa?

hivi una ushahidi gani kwamba mweka hazina ana pesa chafu?!!

mimi ni advocate wa kupenda hoja madhubuti hivyo mtu kama hana mpya jamani asikanyage humu manake ni rahisi kusema huyu kala rushwa huyu mchafu nk lakini hamna lolote la maana ni through critical debates ndio tunaweza kujenga hoja bombaaa!
 
tafiti then jadili,
lisemwalo lipo.....panapofuka moshi.......maneno ya kampeni ya kikwete kufadhiliwa na watu wa ajabu ajabu yameandikwa hata na magazeti ya nje.

kikwete anatakiwa kukaa mbali kabisa na rushwa na walarushwa.......hapaswi hata kuhisiwa katika mambo ya rushwa.........sijui kama unamkumbuka sumaye
 
tafiti
Nadhani sasa unaonekana kuwa matatizo kama hata hili la JK unataka kuanza jalamba . Ok ushahidi mimi nasema wacha tuone kama atafanya haya ambayo ameyadhamiria kuanzia na mikataba hadi kwa Mahalu hapo tutajua yasemwayo ni ya uongo .
 
tafiti
Unataka kuturudisha nyuma kabisa, ngoja nikuulize sali moja wale wajumbe wa mkutano mkuu pale stesheni la reli Dodoma walikuwa wanapewa zile bahasha ndani kulikuwa na nini? Je, hicho kitendo hakikutokea ni majungu au hujui kama kulikuwa na hilo jambo au ile ilikuwa takrima. Please! Wale waarabu wa Egpty waliokamatwa na polisi usiku wanaenda kwenye bwawa la mtera walikuwa Dodoma wanafanya nini? Hii siyo kesi ya mahakamani ukiambiwa zile hela zilikuwa zinatoka mahali fulani ni vigumu kudhibitisha lakini watu waliokuwa wanazigawa walikuwa wanasema wametumwa na nani. Tafiti, siku ukiamua kwenda Dodoma nitakupa majina ya watu na wanakokaa ambao walihusika na kugawa hizo hela ukaongee nao au kama unamjua mjumbe yeyote wa Mkutano mkuu wa CCM muulize kilichotokea Dodoma. Hayo yote ni nje ya kitu so called takrima ambayo ni rushwa tu.
 
Sam,

Nadhani Tafiti ameanza kuingia kwenye hizo forums karibuni. Mengi yaliongelewa kule BCS. Ila Sam naomba kukuuliza swali au nimechanganya?, wewe si ndio me against kikwete? ulimpigiaje kampeni? nakumbuka ulikuwa unamkandia JK, ES alikuwa (anaitwa sam wakati huo) anatoa maovu ya kundi la JK, nakumbuka kusoma ES akisema JK ni safi ila kundi lake ndio chafu!, nimekosea?

Tafiti, haya ya rushwa yamesemwa tena wakati yanatokea. Wanachodai wana bodi ni kuwa JK huwa hausiki direct, ila watu wake!. Mimi bado nina Question mark kuhusu hili la JK na Rushwa!

Swali langu la msingi ni kuwa, kwanini JK hakemei magazeti yanayomsifia tuuuu hata akivurunda?

Mwanakijiji, nilikuomba umuulize swali Mhariri wa This Day kuhusu kuwaandika na kuwaandama wasio wanamtandao? majibu yametoka?
 
Ilikuwa ni katika barabara ya Nairobi Arusha kenye saloon nakataka nywele majira ya saa nane mchana . Kijana wa saloon akapokea simu na baada ya hapo katoa rai chonde Mzeeshuhuli nina mteja ni mtu mkubwa sana Serikali na mwenyekiti wa Bodi kadhaa na mwana CCM na pia ni mtu wa kunusa akiwa na maana usalama .Yeye akija pale kukata nywele kumwachia kijana 50,000 kila mara kwa hiyo na huyo kijana tu anayemkataka nywele ama saloon ile ama nyumbani kwake.

Kijana akasema siasa tuache maana ni mzee wa usalama na mwana CCM. Mimi nikaanza kuwaza tutaujuaje ukweli wa JK na kuteuliwa kwake . Nikapata hint nikazifanyia kazi.Mzee kweli baada ya muda anaingia pale na mgari wake wa kifahari na dereva gari ina namba za watu wa AICC wa UN .

Nikamsalimu akaa chini mara habari kwenye radio ikasema juu ya CCM nami nikaanza sasa .Kwa kuwa nilijua Ntagazwa alipigwa chini kwa kuwa hatuoa rushwa ama hakuwa na mtandao na kwa kuwa nilisha jua kwamba huyo Mzee ni rafiki yake mkubwa Ntagazwa nikachola maneno .

Ninawauliza wale vijana kwa makusudi hivi jamani huyu Mzee Ntagazwa yuko mbona wapi mbona kimya sana ?Mzee akadakia Mzee yupo yule . Nikaendelea mbona sijamsikia akigombea Ubunge kaamua kuacha ?

Ndipo akaanza kusema sasa Uchaguzi wa mwaka huu ni mbaya sana.Hauna misingi ya Umainifu na hakuna mfuasi wa Mwalimu hata mmoja .Nikasema JK akasema kijana sitaki kusema sana .Lakini mimi siwezi kumachagua mtu ambaye amepita uteuzi kwa rushwa ya ajabu sana na uganga wa kienyeji.

Mimi nikashangaa mno . Mzee akasema Ntagazwa anaijua misingi ya uongozi na akafanya kazi na mwalimu hawezi kushiriki rushwa . Akasema yeye na Ntagazwa walikuwa Dodoma waliyo yashuhudia Mungu anajua . Anasema mzee kwamba yeye ni mwana CCM lakini kura ya Urais anampa Mbowe maana JK hafai kanunua uongozi na hatma ya Tanzania kwa miaka 5 baada ya kuwa Rais alikuwa haioni na anaomba Mungu aisaidie Tanzania .Akasema Kingunge ndiye mtunza fedha chafu na kajengewa jumba kubwa tu wapi sijui . Pesa chafu toka ndani na nje ya Nchi .

Haya ni maneno ya yule mzee siku ile pale anayeijua Nchi vyema mzee kichwa choooote ni Mvi na bado anasema JK hapana . Je wte hawa ni waongo bwana tafiti? Sijaingia kwa undani sana maana alisema maneno mazito yule Mzee .
 
Je, JK na maneno yake yote ya kuwa serious, ana ujasiri wa kufanya alichofanya Rais wa Chad? Rais wa Chad kayatimiua makampuni ya uchimbaji mafuta na kawafukuza mawaziri watatu..! Je JK yuko tayari kuyafukuza makampuni ya uchimbaji madini ambayo yanakaidi sheria zetu au yamelaghai kwenye mikataba na wakati huo huo kufukuza mawaziri wote waliohusika na deal hizo...??
 
fikiraduni said:
Mwanakijiji, nilikuomba umuulize swali Mhariri wa This Day kuhusu kuwaandika na kuwaandama wasio wanamtandao? majibu yametoka?

FD, bado sijafanya mahojiano nao... mara mbili wamenikimbia... ila nilikuwa likizo kidogo.... hadi wiki ijayo tutaona tutaanzia wapi..?
 
Kwa mtizamo wangu sidhani kama JK ana ujasiri kiasi hicho. Nilishasema katika moja ya post zangu kuwa as long as JK ni mtoto wa chama, hawezi kuwagusa mentors wake na watu wengine wa karibu waliomsaidia kufikia hadi hapo alipo hata kama wana tuhuma za ufisadi. Na hili tunaliona wazi kwenye baraza lake la mawaziri kuweka watu ambao wanaconflict of interest. Ndio maana hata anasema kuwa anatoa muda ili wafisadi wajirekebishe kana kwamba wakati wakitenda maovu hawakuvunja sheria. JK seems to be very good in rhetoric and political stunts but poor in delivering what he preaches.
 
Katika mojawapo ya matangazo yangu.. nilizungumzia juu ya Taifa la Maonyo!! Taifa ambalo viongozi wake hawafanyi lolote isipokuwa kuonyana!!
 
Bwana Tafiti then Jadili,

Ushahidi wa wizi wa kura wakati wa uchaguzi wa JK upo. Unataka tuuwekeje hapa? Wewe hukuuona? Ulikuwa pori gani mpaka usiuone!

Kuna ushahidi kamili kwenye bajeti ya 2006/2007 kwamba JK amewaibia wanafunzi wa Tanzania fedha zao. Walishapewa ahadi ya kupata mikopo, na sasa amewanyima. Sio kwamba fedha hazipo, zipo, na awamu iliyopita ilishapanga kuwapatia hizo fedha.

Wakati wa uchaguzi, ziliandikwa habari kwamba JK alipewa dola milioni 20 na Iran, kwa kupitia Rostam Aziz. Alitishia kuwashitaki walioandika hizo habari, wakamwambia afanye hivyo. Aliogopa. Unadhani kama sio kweli angeogopa kuwashitaki?

Kuna ushahidi wa wazi kwamba JK anatumia vibaya fedha za wananchi kwa kusafiri huko na huko na kutofanya kazi ofisini. Na inakera unapomuona kwenye picha kachukua kinywaji mkononi na Miss Utalii pembeni, eti ni sherehe ya ma DC na RC. Hao ma Miss Utalii ni ma DC wa wapi?

We are, I submit, being led by a band of sleazy characters whose main interest is to tackle the next skirt rather than the next national problem.

Augustine Moshi
 
FD
Kumbukumbu zako ziko sahii kabisa, na kama unakumbuka vizuri nilichukua hili jina pale Mzee ES alipotuaga kwamba anaenda nyumbani, kumpinga kwangu na kumkandia JK kulikuwa kabla ya uchaguzi wa CCM kule Dodoma. Labda kuna topic moja ilikupita, tuna topic moja kila mtu alikuwa anaeleza msimamo wake ni nani anafaa kuwa rais kati ya wagombea waliopo nilieleza sababu zangu na kueleza ni kwa nini nimeamua kumchagua rais. Hata leo wakirudi wale wale waliogombea urais nadhani itabidi nisimpigia debe yoyote kama itakuwa ni lazima nitaenda na JK pamoja na kumpinga kwenye mambo mengi. Unakumbuka wakati tunamuongelea Mbowe, nilikuwa mmoja ya watu wa mbele sana kupinga sera ya majimbo ya CHADEMA ambayo ilikuwa inasema fedha zinazopatikana na maliasili zitumike sehemu zinakopatikana kitu ambacho nadhani kitaleta tabaka kubwa ya maendeleo ya nchi kwani kuna sehemu nyingine hazina maliasili kabisa. Nadhani wote tunakubaliana shughuli zote za biashara zitaamia sehemu zenye maendeleo ya barabara, maji, umeme, n.k na kuziacha sehemu zisizo na maliasili watu wakiendelea kuwa masikini. Hivi majuzi tumesikia sera hiyo kumbe iliibwa na CCM kuhusu madini, halmashauri husika zitakuwa zinapata uraji. Kitu ambacho kimenifanya niwe njiapanda nisijue kwa kukimbilia, nasubiri CHADEMA watoe sera zao ambacho wanasema wamezifanyia marekebisho. You never know, maybe I will go with Mbowe and co. 2010.

Mzee Moshi taratibu, we all know.
 
hizi zote kauli za rushwa ni hear say tu.

nashindwa kutoa uthibitisho kwa vile naona mnaongea ongea tu

kukiwa na ciritical points tutaonana manake siwezi kudispute maneno aliyosema mzee akinyolewa! au maneno ya kuwa kulikuwa na bahasha za brown, sikuwepo dodoma!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom