Mzee Kikwete: Mzigo wa Ujenzi wa SGR Umebebwa na Rais Samia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
54,603
64,730
Ukweli huu Kuna kundi la watu Huwa hawataki Asante sana JK Kwa kuweka mambo hadharani 👇👇

View: https://twitter.com/mamanafanikisha/status/1818568426115260588?t=D2CN2fHPvVBoX3HjF4w7KA&s=19

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete amesema tumpongeze Rais Samia kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, huku vipande vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Akijibu swali la Idriss Sultan katika Podcast maalumu iliyofanyika nyumbani kwake, Rais huyo wa awamu ya nne wa Tanzania, amesema kuwa wazo la SGR lilianza baada ya Mkapa kufanya mazungumzo na Rais Kagame wa Rwanda juu ya kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Kigali.

Hata hivyo Kikwete amesema tumpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kubeba mzigo mzito katika kukamilisha mradi huo utakaogharimu takriban Dola bilioni 7 za kimarekani.

Chanzo: Habari Mpya

Pia soma

My Take: Miradi yote ya urithi ilikuwa chini ya 40% lakini Samia ameikamilisha bila mbwembwe bila kujimwambagai.

Hongera sana mama kazi umeniweka Kwa ufanisi mkubwa 👇👇

sgr.jpg
 
Jk asizunguke kwenye media kumsemea Samia…! Samia na JPM walianza kuitekeleza hiyo miradi kwa hiyo yeye JK hana alichofanya zaidi ya kuongea!

JK anaumia hakufanikisha hiyo miradi na anaumia zaidi watanzania wanajua miradi ni mchango na nguvu za JPM!

JK kila leo anazunguka kufanya interview za kulazimisha JPM asionekana amefanya lakini bado ana gonga mwamba 😂😂😂😂
 
Kakamilisha aliyoikuta 40% tu ila aliyoianzisha yeye imwkwama nenda Lot 5 kwa taarifa zaidi
Kipaombele ni kukamilisha,kwani yeye Magufuli alikamilisha ndani ya awamu ya kwanza? So hiyo ya Samia itakamikishwa awamu ijayo
 
My Take
Ukweli huu Kuna kundi la watu Huwa hawataki kuambiwa.

Miradi yote ya urithi ilikuwa chini ya 40% lakini Samia ameikamilisha bila mbwembwe bila kujimwambagai.

Hongera sana mama kazi umeniweka Kwa ufanisi mkubwa 👇👇

View: https://twitter.com/WizarayaUC/status/1817837705088110853?t=PBQsCCJDW5JMDK5PfH9ItQ&s=19

MAMA SAMIA RAISI WETU ANA TOFAUTI KUBWA MNO NA WATANGULIZI WAKE. KWA JINSI ALIVYOKAMILISHA MIRADI YA MTANGULIZI WAKE BILA KUPIGA MAKALELE NI MAAJABU AMBAYO VIONGOZI WOTE WANATAKIWA KUJIFUNZA.
 
raisi Samia akiweza kujenga hata 5 km tu pass Dom ni ikakamilika pamoja na station ya maana ndiyo nitampa sifa yoyote, hiyo Dar-Moro/Dom kila kitu kilishafanyika na hata Kandarasi aliachwa site, ajenge beyond Dodoma kwanza ndiyo nimpe sifa kwa upande wangu, aifikishe hata Manyoni (Singida) tu na tuone station imekamilika kila kitu …
 
Jk asizunguke kwenye media kumsemea Samia…! Samia na JPM walianza kuitekeleza hiyo miradi kwa hiyo yeye JK hana alichofanya zaidi ya kuongea!

JK anaumia hakufanikisha hiyo miradi na anaumia zaidi watanzania wanajua miradi ni mchango na nguvu za JPM!

JK kila leo anazunguka kufanya interview za kulazimisha JPM asionekana amefanya lakini bado ana gonga mwamba 😂😂😂😂
Wote hao wanafuata ilani ya CCM ni kama mbio za vijiti kupokezana kwa hiyo hapa huwezi kuwatoa viongozi wote hao kwenye maendeleo ya nchi hii
 
raisi Samia akiweza kujenga hata 5 km tu pass Dom ni ikakamilika pamoja na station ya maana ndiyo nitampa sifa yoyote, hiyo Dar-Moro/Dom kila kitu kilishafanyika na hata Kandarasi aliachwa site, ajenge beyond Dodoma kwanza ndiyo nimpe sifa kwa upande wangu, aifikishe hata Manyoni (Singida) tu na tuone station imekamilika kila kitu …
KWA HIYO HUKTAKA AKAMILISHE AWAMU YA KWANZA NDIO AENDELEE HADI HUKO UNAKATOKA?
 
la hasha, nimefurahia sana mpaka sasa hivi na kukamilishwa kwa Dar-Moro/Dom, nina furaha isiyo na kifani chozi lilinitoka siku treni ilipoondoka na abiria Dar na kufika Moro, nikasema yes we did it …
 
Jk asizunguke kwenye media kumsemea Samia…! Samia na JPM walianza kuitekeleza hiyo miradi kwa hiyo yeye JK hana alichofanya zaidi ya kuongea!

JK anaumia hakufanikisha hiyo miradi na anaumia zaidi watanzania wanajua miradi ni mchango na nguvu za JPM!

JK kila leo anazunguka kufanya interview za kulazimisha JPM asionekana amefanya lakini bado ana gonga mwamba 😂😂😂😂
Amesahau kuwa hii generation sio ya wajinga
 
raisi Samia akiweza kujenga hata 5 km tu pass Dom ni ikakamilika pamoja na station ya maana ndiyo nitampa sifa yoyote, hiyo Dar-Moro/Dom kila kitu kilishafanyika na hata Kandarasi aliachwa site, ajenge beyond Dodoma kwanza ndiyo nimpe sifa kwa upande wangu, aifikishe hata Manyoni (Singida) tu na tuone station imekamilika kila kitu …
Andika ueleweke
 
Jk asizunguke kwenye media kumsemea Samia…! Samia na JPM walianza kuitekeleza hiyo miradi kwa hiyo yeye JK hana alichofanya zaidi ya kuongea!

JK anaumia hakufanikisha hiyo miradi na anaumia zaidi watanzania wanajua miradi ni mchango na nguvu za JPM!

JK kila leo anazunguka kufanya interview za kulazimisha JPM asionekana amefanya lakini bado ana gonga mwamba 😂😂😂😂
JPM alimfunika sana Kikwete kiasi kuwa bado inamuuma sana hata baada ya JPM kutangulia. Kikwete angekuwa na busara, angeacha historia ijiandike yenyewe badala ya yeye kujaribu kupanga historia iweje. Juhudi hizi za kuandika historia upya zitamharibia jina zaidi kwenye historia itakayojiandika yenyewe.

Anachotakiwa kufanya sasa hivi ni kuzungumzia mstakhbali wa nchi na jinsi ya kusonga bele kama nchi badala ya kukomalia mambo yaliyokwisha pita ambayo hawezi kubadili.
 
Back
Top Bottom