Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,092
- 866
Makamu wa Rais wa Jamhuri va Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), leo tarehe 08 Oktoba 2026.
Mkataba wa Nairobi (Nairobi Convention) unalenga kuimarisha uhifadhi, usimamizi endelevu na ulinzi wa mazingira va bahari na Ukanda wa Pwani katika eneo la Magharibi mwa Bahari ya Hindi.
Mkutano huo, ulioanza tarehe 06 Oktoba 2026 na unaotaraiiwa kuhitimishwa tarehe 09 Oktoba 2026 unafanvika sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi. ulioanzishwa mwaka 1985.
Aidha, mkutano huo unalenga kujadili mikakati ya kukuza uchumi wa buluu kupitia uvuvi endelevu, kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya bahari na athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuimarisha uhifadhi wa bayoanuai za baharini na maeneo ya pwani.