Katika suala lolote zuri, mwenzako akifanya vizuri LAZIMA UMPE PONGEZI na SIFA. Mhe.Magufuli mimi binafsi nimekuvulia kofia katika suala la madawati. Haitachukua muda mrefu shule zote zitafurika na madawati. Suala hili lilishinda watangulizi wako,wewe umeiweza. Kumbe jambo ukiliamua na kulisimamia na kuwa na ufuatiliaji kumbe linawezekana na hili umeliweza Mhe. Magufuli.
Mhe. Magufuli ninachokuomba sasa ulisimamie ni KILA MWANAFUNZI KUVAA VIATU. Shule nyingi hasa za msingi asilimia kubwa HAWAVAI VIATU na magonjwa mengi yanatokana na wanafunzi kutovaa viatu. Mimi ninawasifu wenzetu wa Mikoa ya Manyara na Arusha kwa asilimia kubwa wanafunzi wanavaa viatu. Nenda Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang', Ngorongoro, Monduli, Longido, Mbulu,Karatu na Babati asilimia kubwa ya wanafunzi wanavaa viatu japo ni kata mbuga lakini ni viatu. Mfano Ngorongoro asilimia karibu mia wanavaa viatu na hii ni kinyume na Wilaya kama ya Rorya, Chato,Muleba, Misungwi n.k. Toa agizo mara moja kila mwanafunzi avae viatu. Agizo la Rais ni Amri. Kitachofuata baada ya hili ni kila mwanafunzi apate chakula cha mchana. Nawasilisha.