Mhe. Magufuli kweli nimekuvulia kofia kwa suala la madawati

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
276
Katika suala lolote zuri, mwenzako akifanya vizuri LAZIMA UMPE PONGEZI na SIFA. Mhe.Magufuli mimi binafsi nimekuvulia kofia katika suala la madawati. Haitachukua muda mrefu shule zote zitafurika na madawati. Suala hili lilishinda watangulizi wako,wewe umeiweza. Kumbe jambo ukiliamua na kulisimamia na kuwa na ufuatiliaji kumbe linawezekana na hili umeliweza Mhe. Magufuli.
Mhe. Magufuli ninachokuomba sasa ulisimamie ni KILA MWANAFUNZI KUVAA VIATU. Shule nyingi hasa za msingi asilimia kubwa HAWAVAI VIATU na magonjwa mengi yanatokana na wanafunzi kutovaa viatu. Mimi ninawasifu wenzetu wa Mikoa ya Manyara na Arusha kwa asilimia kubwa wanafunzi wanavaa viatu. Nenda Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang', Ngorongoro, Monduli, Longido, Mbulu,Karatu na Babati asilimia kubwa ya wanafunzi wanavaa viatu japo ni kata mbuga lakini ni viatu. Mfano Ngorongoro asilimia karibu mia wanavaa viatu na hii ni kinyume na Wilaya kama ya Rorya, Chato,Muleba, Misungwi n.k. Toa agizo mara moja kila mwanafunzi avae viatu. Agizo la Rais ni Amri. Kitachofuata baada ya hili ni kila mwanafunzi apate chakula cha mchana. Nawasilisha.
 
Kwa hiyo unataka baada ya mradi wa madawati serikali ifanye kampeni wadau wachangie pia viatu. Dah, huu ushauri wako naona una dhamira ya kupinguza wajibu wa wazazi. JPJM akiukubali nitamshangaa sana.

Kwa habari ya chakula cha mchana; tulipe kodi zaidi ili "elimu bure" iwe bure kweli kweli. Hata ukinunua pipi omba risiti ya kielektrojiki.
 
Acha kuponda unajua kampeni ya sekondari kwa kila kata ilianzishwa na nani?
Je kampeni ya kujenga mahabara kwa kila shule ya sekondari? Uyu kaja kumalzia tu watangulzi wake ndio wamefanya kazi kubwa.
 
Acha kuponda unajua kampeni ya sekondari kwa kila kata ilianzishwa na nani?
Je kampeni ya kujenga mahabara kwa kila shule ya sekondari? Uyu kaja kumalzia tu watangulzi wake ndio wamefanya kazi kubwa.
Sawa lakini sio kila sekondari ina mahabara isitoshe JPM ametumia muda mchache kutatua kero za madawat
 
Acha kuponda unajua kampeni ya sekondari kwa kila kata ilianzishwa na nani?
Je kampeni ya kujenga mahabara kwa kila shule ya sekondari? Uyu kaja kumalzia tu watangulzi wake ndio wamefanya kazi kubwa.

Mkuu ulishasoma mpango wa maendeleo wa 2025 uliosimamiwa enzi hizo na waziri wa sasa wa Fedha na Mipango? Awamu zote zilizopita zinadokoa dokoa vision za mule, hata hili la sasa la viwanda lipo mule. Kabla haujaanza kumsifia mtu angalia ujue nini kiko nyuma yake
 
Back
Top Bottom