Mhariri wa Mwananchi, Theophil Makunga, naye kuburuzwa Mahakamani leo!

Kumbe Mwigamba ndo amiri geshi mkuu? najua watu wnegi ni wavivu wa kusoma makala ila sasa hii makala itatafutwa mno, na ujumbe utafikia wengi. Na hawatakuwa kama walivo jana.
 
Mkuu nakuheshimu..! Pia nadhani utakuwa na level fulani ya taaluma (hata kama si ya uandishi wa habari). Sasa naomba nikuulize kwa kile nilicho-highlight red hapo juu:
  1. Umesema bila shaka uhuru huo umezidi mipaka bila ku-cite ni wapi au kipengere kipi katika makala Mwigamba alivuka mipaka na mpaka ni upi. Ufafanuzi tafadhali..?
  2. Ni wakati muafaka wa kurudisha mambo yawe kama yanavyopaswa kuwa au kama yalivyokuwa..? Maana kama ndivyo yanavyopaswa kuwa basi nchi hii iko hatarini kubaki vipande vipande. Uhuru wa kutoa/kupokea maoni unaingiliwa, we Mtanzania mwenzetu unachekelea?
Huu ni wakati wa kila Mtanzania kusimama imara kupinga huu unyanyasaji. Maana hata katiba mpya itaandikwa kwa maoni kama ya Mwigamba, sasa kama tayari tunaanza kutishwa namna hii kweli kuna katiba mpya hapo..?

Take: Tuionee huruma nchi yetu Tanzania..!

Mkuu usipate pressure,

Katika msafara wa mamba..... na especially wale ambao wanaishi kwa kuweka mikono nyuma ili waonewe huruma na kupatiwa kilo ya unga ili siku iende.....Hawana tena uhuru hao....Their price is fixed!!
 
Dark City hii ni moja ya sheria 40 za ukandamizaji ambazo zilipaswa kufutwa tangu zamani. Kwa vile ilikuwepo na haikutumika, tasnia ya habari ikabweteka kwa kujiaminisha kuwa haitatumika sasa serikali imeikumbuka inaitumia ndio sasa waandishi tunaamka tunaona tunaonewa!.

Hii kesi itakuwa ndio landmark case ya kuhakikisha this time inakuwa scrapped off from the books of laws!.

Kama mtazamo ni huo....I can now take half of Xmass holiday!
 
Pamoja na nguvu ya fedha, lakini Kikwete aliingia madarakani akisaidiwa pia kwa nguvu ya vyombo vya habari. Alipoingia, walimuomba awasaidie kitu kimoja tu, abadilishe sheria zilizopo kwa sababu zilikuwa zinawakandamiza. Walimuomba kirafiki na akawaambia kuwa hilo litatekelezwa katika mwaka wa kwanza wa utawala wake.

Miaka sita imepita sasa na badala ya kuzifuta sheria hizo na kuzileta zitakazowasaidia rafiki zake waliomsaidia kuingia madarakani, serikali anayoiongoza inazitumia sheria zile zile kuwashughulikia wale waliokwua wanaamini kuwa ni rafiki yao. Ama kweli...
 
Hii ikiendelea uhuru wa vyombo vya habari uatatoweka!tutabaki na magazeti kama ya uhuru!
 
Dark City hii ni moja ya sheria 40 za ukandamizaji ambazo zilipaswa kufutwa tangu zamani. Kwa vile ilikuwepo na haikutumika, tasnia ya habari ikabweteka kwa kujiaminisha kuwa haitatumika sasa serikali imeikumbuka inaitumia ndio sasa waandishi tunaamka tunaona tunaonewa!.

Hii kesi itakuwa ndio landmark case ya kuhakikisha this time inakuwa scrapped off from the books of laws!.

Pasco,

Ningependa kufahamu itatokea tokeaje hii sheria kuwa scrapped off the books of laws kupitia kesi hii.
Kwamba hakimu anaweza kuitangaza kuwa iko kinyume cha katiba? ama kupitia kesi hii wanahabari/wanasheria wanaweza kupata platform ya kufungua kesi kuipinga sheria hii?
 
Tatizo kubwa ni wanahabari wetu,hii sheria ipo muda mrefu lakini hawakuisemea sana,waliipuuza! Wanahabari hawana umoja wa dhati wa kujitoa,hata hii movement tunayoiona hapa ni juhudi binafsi za Pasco lakini bila Pasco kupata sapoti ya kutosha kuipinga sheria hii hatofanikiwa(kumbuka kwa wamiliki wa vyombo vya habari,habari kama hìi haiuzi).hatuna wanahabari wa kujitoa haswa na hata waliopo wanajitoa lakini hawadumu pumzi inakwisha kwasababu ya uchache wao unaofanya washughulikiwe kirahisi kama ndugu yetu Pasco wa JF! Namuombea na Mkuu Max asiishiwe pumzi mapema maana ndio only Survival ambaye target tu haijamlenga ili wamlipue! Tutafika kwa uwezo wa Mola!
Mtazamo, nimeguswa sana na maneno yako!. Wanahabari walibweteka sana na sasa they are caught by surprise!.

Ama kweli penye miti hapana wajenzi!. Waandishi ni wapiga debe wazuri wa haki za wenzao lakini zao!.

Waandishi ni kama maboga, baba anasuka sana mikeka, lakini watoto wake wanalala chini!.

Hii kesi ndio fungua macho, huu sasa ndio wakati muafaka sio tuu kushikia bango sheria hii, bali kushika bango sheria mpya ya habari ipitishwe kwenye cabinet muswada upelekwe bungeni tuondokane na ukwandamizaji huu wa uhuru wa kutoa maoni.
 
Ni wakati sasa wanahabari bila ya kuangalia itikadi zao za kisiasa kuungana ili hii sheria ifanyiwe mabadiliko ama sivyo tutarudi kule tuliko toka..U-dikteta wa uhuru wa habari..
 
Pasco,

Ningependa kufahamu itatokea tokeaje hii sheria kuwa scrapped off the books of laws kupitia kesi hii.
Kwamba hakimu anaweza kuitangaza kuwa iko kinyume cha katiba? ama kupitia kesi hii wanahabari/wanasheria wanaweza kupata platform ya kufungua kesi kuipinga sheria hii?
Mwita Maranya, tangu ilipotangazwa kuwa miongoni mwa sheria 40 za ukandamizaji, haikuwahi kutumika tena ndio sasa, hivyo hii ndio opportunity ya kuifumua rasmi na kuwa declared "unconstitutional" hivyo kuwa scrapped off from books of laws.
 
Vyombo vya DOLA ndivyo vinaimaliza serikali yake kwa kulifikisha suala hili hapo lilipofikia. Huenda vyombo hivi navyo vimeguswa na makala ile. Makala hii ilishatupita wengi tu hata tuliolinunua gazeti hili siku hiyo. Wanajeshi, Polisi, Magereza na hata UwT wengi hawasomi magazeti kabisa.
 
Alitaka kujitofautisha na yule pasco mayala wa gamba......

Afadhali umewatofautisha kwani yule Pascal Mayala mtangazaji ni kibaraka mkubwa wa ccm na gamba lake la KOBE halivuliki; hopefully these two are diffrent!
 
Mwita Maranya, tangu ilipotangazwa kuwa miongoni mwa sheria 40 za ukandamizaji, haikuwahi kutumika tena ndio sasa, hivyo hii ndio opportunity ya kuifumua rasmi na kuwa declared "unconstitutional" hivyo kuwa scrapped off from books of laws.
Mwambie pia kinagaubaga kuwa mahakama ina uwezo kisheria ku-declare kwua sheria fulani haifai na kutaka aidha ifutwe au irekebishwe
 
Mwita Maranya, tangu ilipotangazwa kuwa miongoni mwa sheria 40 za ukandamizaji, haikuwahi kutumika tena ndio sasa, hivyo hii ndio opportunity ya kuifumua rasmi na kuwa declared "unconstitutional" hivyo kuwa scrapped off from books of laws.

Pasco,

Ahsante kwa maelezo yako. Kama kweli sheria hii ilikuwa imewekwa kabatini tangu ilipobainishwa na tume ya Nyalali na sasa wameamua kuifungua tena, Je hudhani kwamba serikali inaweza kutia mkono wake na hatimaye mambo yanaweza kuwa kama kesi ya mgombea binafsi?
 
Mwambie pia kinagaubaga kuwa mahakama ina uwezo kisheria ku-declare kwua sheria fulani haifai na kutaka aidha ifutwe au irekebishwe

Mkuu bado tuna kumbukumbu na kesi ya mgombea binafsi, ndio maana bado tunakuwa na mashaka kama kweli kesi hii inaweza kuwa chanzo cha kuiscrap sheria hii.
 
Dalili zote za mwisho wa utawala wa hiki chama chetu chamapinduzi zinaonekana. Ni muda ndo count down.

WanaJf na wahariri na waandishi,

wote kwa ujumla napenda kutoa pole za dhati kwa usumbufu wote mnaopata. Ninawaombea moyo mkuu. Kazi yenu ni nzito, mnajukumu la kusimamia ukweli. Truth is only one and is indivisible. Simamieni ukweli daima. Msimsimaie mtu au upande wowote, bali simamieni daima ukweli na kweli tupu. Mtatukanwa, mtasemwa, mtakamatwa na hata kuhukumiwa lakini hatima ya yote ukweli utashinda. Piganieni ukweli daima na ukweli unauma, msikubali kuuza utu na heshima ya ya ubinadamu wenu, historia itawatuza hata kama kwa muda mtateseka na kunyanyasika.
 
Huyu Pasco nahisi ni mtu wao wa Tiss anakuja hapa kujifanya is concerned by the plight of the fraternity of jounalists at the same time anatutisha tusiandike kukosoa serikali eti wanaweza kulifunga jukwaa!! HAKUNA NCHI INAKOMBOLEWA BILA SADAKA YA WATU FULANI FULANI katika jamii na hawa wakina Mwigamba, Kibanda na Makunga wao ndio sadaka yenyewe ya kuelekea ukombozi wa nchi!!Watawala wetu hawako tofauti na wakoloni waliowafunga waandishi wa habari Makange na Baghdeleh na hatima yake nchi ikakombolewa toka ukolono!! Tatizo la hawa jamaa ni wavivu wa kusoma historia kazi yao kusikiliza mipasho ya taarab ya mzee Yusuf tu!!!
Ndinani, kuhisi pia ni miongoni mwa freedom of expression. Wasiliana na Faiza Foxy kuna post nilimjibu hadi kumuelekeza ofisini kwangu pale kwenye ule mjengo mkubwa jirani na St. Peters. Nawewe nakukaribisha ile pale ofisini hatuitani majina yetu halisi, kama uko serious njoo tuu iniulizie kwa jina la kazini waniita 'Chifu' ukifika tuu getini na kusema unakwenda kwa Chifu utaletwa moja kwa moja na utaniona.

Ili kunifahamu vizuri mimi Pasco wa jf, unaweza kutembelea profile yangu ukasoma thread zangu na posts zangu jinsi ninavyomfagilia JK na kuisifu CCM kwa kazi nzuri inayotufanyia!.

Most welcome!.
 
Back
Top Bottom