Mhariri Tanzania Daima ashikiliwa na Polisi!

Mhariri Tanzania Daima ashikiliwa na Polisi!

Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Edson Kamukara anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu asubuhi mpaka muda huu.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi hazijaweka bayana kosa la Mhariri huyo ingawa amehojiwa kutokana na habari anazozihariri.

Baada ya serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi gazeti linaloandamwa kwa sasa ni Tanzania Daima.Inadaiwa serikali haifurahishwi na habari mbalimbali zinazotolewa na gazeti hilo hasa taarifa zinazoonekana kukitangaza na kukijenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA

sasa wakimkamata ndiyo iweje, wawa funge wote lakini CDM ni zaidi na Taarifa zitawafikia wananchi kwa namna tofauti kabisa, Magazeti yote , maredio yote, maTV yote, Wasanii wote, Wanakwaya wote, zaidi ya mia tano yote hayawatoshi? mnataka hata hilo moja mlifungie? haya lifungueni mfurahi.

Wananchi hawategemei Tanzania daima kupena habari Mabadiliko ni Lazima tuuu hata iweje
 
Wawahoji na gazeti la Mtanzania waliosema kuna magaidi wa Al-Shabab Ukerewe na waliomuua Padri Zanzibar wakamatwa Nairobi na gazeti la Uhuru.
 
Kweli bora kichaka kiwe ndo jirani yako kuliko mchawi.. huyu HB kwa ghiriba na visasi duh! salia la mkaburu mweusi .
 
..., kwani gazeti la Tanzania Daima ni la CHADEMA?

ndiyo ni la chadema, mpambano ni mkali-mwangosi, mwanahalisi, dr ulimboka, bunge halionyeshwi, hoja za mnyika kutupwa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho utakuja ambiwa Dr Slaa siyo raia wa nchi na huu utakuwa mwisho wa nchi ya Tanzania(machafuko)
 
Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Edson Kamukara anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu asubuhi mpaka muda huu.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi hazijaweka bayana kosa la Mhariri huyo ingawa amehojiwa kutokana na habari anazozihariri.

Baada ya serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi gazeti linaloandamwa kwa sasa ni Tanzania Daima.Inadaiwa serikali haifurahishwi na habari mbalimbali zinazotolewa na gazeti hilo hasa taarifa zinazoonekana kukitangaza na kukijenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA

Huu kweli ni uwendawazimu wa Serikali ya CCM.

Mbona CCM wana magazeti yao ya UHURU,MZALENDO,DAILY NOISE na mengine ya UDAKU ambayo kila siku yanakisifia chama chao cha Majambazi huku yakivikandia vibaya vyama vya upinzani???Mbona hatujasikia wahariri wa UHURU,MZALENDO au DAILY NOISE kushikiliwa na Polisi????????????????

Nafikiri Serikali ya CCM na PoliCCM walipofikia sasa ni kwamba hawawezi kufikiri tena kabisa. Huu ndiyo tunaita uchochezi wa wazi. Kwamba wewe ukiwasema wenzako vibaya wao wanyamaze tu lakini ukisemwa wewe ni kosa la jinai. Hii haikubaliki kwenye jamii iliyostaarabika kuna siku watu wataamua kutwangana makonde kwa upuuzi huu wanaofanya serikali.

Hivi kama matokeo ya F4 yamekuwa mabaya wanataka Magazeti yaaandike nini????Kama serikali kupitia Wizara ya Elimu hawana Mitaala wanataka vyombo vya habari viandike nini???Kama wabunge wa CCM wanatoroka Bungeni na hata wakiwemo wanalala Bungeni na hata wasipolala hawana hoja za kuchangia,Tanzania Daima waandike nini????

Kweli Kikwete anatuharibia nchi na hafai kuwa Rais wa nchi hii.
 
Waacheni wahangaike na magazeti wakidhani tatizo ni vyombo vya habari. Chadema hainezwi na vya habari, chadema inaenezwa na "word of mouth", labada wawafunge midomo watanzania wote kwa magufuli wasiongee!
mkuu umesahau kingine umaskini wa watanzania unazidi kuongezeka wakati zirone anazidi kuwa tajiri sasa hivi nasikia anajaribu kuwafikia akina baresa. hakyamungu akimchumbia dada yangu nampa bure siku hiyo hiyo japo na sisi familia yetu ipewe sheli moja zile za panone
 
****** habari za kumtukana Zitto ndio zitakazo mpeleka shimoni.

Hata mimi nashangaa sana unaweza kudhani huenda Zitto anauhasama na Mhariri mhusika. Very strong message about Zitto Kabwe je nyie kama Tanzania Daima kwa Zitto Kabwe mnamjenga au mnambpmoa. Tunawashangaa sana.
 
Huu kweli ni uwendawazimu wa Serikali ya CCM.

Mbona CCM wana magazeti yao ya UHURU,MZALENDO,DAILY NOISE na mengine ya UDAKU ambayo kila siku yanakisifia chama chao cha Majambazi huku yakivikandia vibaya vyama vya upinzani???Mbona hatujasikia wahariri wa UHURU,MZALENDO au DAILY NOISE kushikiliwa na Polisi????????????????

Nafikiri Serikali ya CCM na PoliCCM walipofikia sasa ni kwamba hawawezi kufikiri tena kabisa. Huu ndiyo tunaita uchochezi wa wazi. Kwamba wewe ukiwasema wenzake vibaya wao wanyamaze ukisemwa wewe ni kosa la jinai. Hii haikubaliki kuna siku watu wataamua kutwangana makonde kwa upuuzi huu wanaofanya serikali.

Hivi kama matokeo ya F4 yamekuwa mabaya wanataka Magazeti yaaandike nini????Kama serikali kupitia Wizara ya Elimu hawana Mitaala wanataka vyombo vya habari viandike nini???Kama wabunge wa CCM wanatoroka Bungeni na hata wakiwemo wanalala Bungeni na hata wasipolala hawana hoja za kuchangia,Tanzania Daima waandike nini????

Kweli Kikwete anatuharibia nchi na hafai kuwa Rais wa nchi hii.

mnataka kikwete awaache muendelee kuigawa nchi vipande vipande??????????????????????????????????????????
 
waandishi wenyewe ni akina isango yule jamaa mwenye njaa halafu ni mlevi anaandika habari za kuokoteza mitaani anaita za kiuchunguzi........ lazima waning'inizwe hawa
 
tanzania daima lilijijengea heshima lakini hivi sasa watanzania wamelishtukia, linaandika udaku sana
 
NI UJUHA KUJADILI KiTU MSICHOKIJUA, HAMJUI SABABU LAKIN MNAANZA KUUNDA HOJA ZISIZO NA MAANA.

KAMA AMEIBA? AMEBAKA? AMETUKANA? KATEMBEA NA MKE WA MTU?

INAMAANA MTU AKIWA MHARIRI ASIKAMATWE NA POLISI? SUBIRINI KWANZA MJUE SABABU YA KUKAMATWA KWAKE NASIO MNAKUJA NA HISIA TU KAMA SIO WASOMI.

USHABIKI WA KISIASA WA KUPINDUKIA HUPUNGUZA UWEZO WA KUTAFAKARI.
 
kweli hatuna serikali.

Mkuu, kwani hujui kama nchi iko under Auto-Pilot?

Vasco da Gama ametoka Ethiopia kaenda Uganda Kumzika Babake Museveni, huenda safari ya Ulaya tena ikaja soon

Only in Tanzania!
 
CHADEMA haienezwi na gazeti lolote ila Mungu amekipa kibali kukubalika kwa watanzania"
 
Back
Top Bottom