Mhanga wa Sabaya atinga Mahakamani. Awataja wengine waliomteka

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mmoja ya wahanga wa tukio la Kushambuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Simon Mnyampamda ambaye Ni Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hai, ametinga katika Mahakama ya Wilaya Arusha na kukutana uso kwa uso na mtesi wake wakati huo Ole Sabaya na wenzake walipofikishwa Mahakamani leo.

Mnyampamda ambaye alivunjwa miguu yake miwili kwa kipigo baada ya kutekwa na kikosi Cha Uhalifu Cha Sabaya wakidai amekutwa na mke wa mtu, alifika mahakamani hapo kusikiliza shauri la Sabaya na wenzake ambao walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi mbalimbali ikiwemo ya Unyang'anyi wa kutumia silaha .

Ajiongea mahakamani hapo alisema sahau Agosti 7 mwaka 2020 ndio siku alipotekwa na kikosi hicho na kumshambulia kwa kipigo wakitumia chuma na kumvunja miguu yote miwili na baadaye kumtelekeza akiwa uchi wa mnyama usiku wa manane na kuokolewa na msamalia mwema.

Mnyambaa ambaye aliokotwa na wasamalia wema akiwa ametupwa porini, kwa sasa anatembea kwa kuchechemea na aliwatambua baadhi ya watu waliokuwa wakimteka na kumtesa siku ya tukio ni pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM.

Niliobahatisha kuwatambua ni pamoja na Ole Sabaya ambaye alinifuata na kunipa dakika 20 nisali kabla mauti kunifika, mwingine ni Martin Munisi Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Fredrick Pangani Diwani wa Kata ya Masama kusini, Inocent Malya Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Hai, Omari Mlekwa Mwandishi wa Habari na mshauri wa migambo Hai, Siao (Black), Bashiri Uroki, Lameck Swai (MC Lameck) na mchungaji Mashimo kutoka Dar, Said Kagumba Afisa Tarafa Machame, wengine sikuweza kuwatambua kwa sababu walikuja na gari tatu na watu waliokuwa Ni wengi.

Hata hivyo Sabaya wakati akiteremka kwenye karandinga la Magereza alikumbana na adha ya matusi na zomea zomea kutoka kwa Wananchi waliokuwa wemefurika Mahakamani hapo.

IMG-20210618-WA0005.jpg
IMG-20210618-WA0006.jpg
IMG-20210618-WA0007.jpg
 
Mmoja ya wahanga wa tukio la Kushambuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya ,Simon Mnyampamda ambaye Ni Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hai,ametinga katika mahakama ya wilaya Arusha na kukutana uso kwa uso na mtesi wake wakati Sabaya na wenzake walipofikishwa mahakamani leo.

Mnyampamda ambaye alivunjwa miguu yake miwili kwa kipigo baada ya kutekwa na kikosi Cha Uhalifu Cha Sabaya wakidai amekutwa na mke wa mtu ,alifika mahakamani hapo kusikiliza shauri la sabaya na wenzake ambao walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi mbalimbali ikiwemo ya Unyang'anyi wa kutumia silaha .

Ajiongea mahakamani hapo alisema sahau Agosti 7 mwaka 2020 ndio siku alipotekwa na kikosi hicho na kumshambulia kwa kipigo wakitumia.chuma na kumvunja miguu yote miwili na baadaye kumtelekeza akiwa uchi wa mnyama usiku wa manane na kuokolewa na msamalia mwema.

Mnyambaa ambaye aliokotwa na wasamalia wema akiwa ametupwa porini ,kwa sasa anatembea kwa kuchechemea na aliwatambua baadhi ya watu waliokuwa wakimteka na kumtesa siku ya tukio ni pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM.

Niliobahatisha kuwatambua Ni pamoja na Ole Sabaya ambaye alinifuata na kunipa dakika 20 nisali kabla mauti kunifika, mwingine ni Martin Munisi diwani wa kata ya Machame Magharibi, Fredrick Pangani diwani wa kata ya Masama kusini ,Inocent Malya katibu mwenyezi wa CCM wilaya ya Hai,Omari Mlekwa mwandishi wa habari na mshauri wa migambo Hai,Siao (Black),Bashiri Uroki ,Lameck Swai (mc Lameck) na mchungaji Mashimo kutoka Dar na said kagumba afisa tarafa Machame,wengine sikuweza kuwatambua kwa sababu walikuja na gari tatu na watu waliokuwa Ni wengi.

Hata hivyo sabaya wakati akiteremka kwenye karandinga la Magereza alikumbana na adha ya matusi na zomea zomea kutoka kwa wananchi waliokuwa wemefurika mahakamani hapo.View attachment 1822849View attachment 1822853View attachment 1822886
Inasikitisha sana binadamu kugeuka kuwa shetani
 
Ndiyo yeye, ukiwa Mahabusu kuhusu chakula na mavazi siyo jambo geni. Mtu hupewa treatment nzuri tu kama ndugu zako wanaweza kukuhudumia....
kwahiyo ndio kusema mahabusu ya sabaya haina tabu maana anahudumiwa na familia yake.
 
kwahiyo ndio kusema mahabusu ya sabaya haina tabu maana anahudumiwa na familia yake.
Utaratibu wa kuwa Mahabusu ni tofuati na kuwa Mfungwa, kwa mahabusu unaendelea kupelekewa huduma ikiwemo chakula na mavazi, kuna utaratibu umewekwa na magereza.

Mfungwa utaratibu wa chakula ni kila Jumapili (siku ya kuona wafungwa), unaweza kupeleka pesa, vyakula au viatu ukampa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom