ADE(Advanced Diploma in Engineering) inatambulika kama degree.Ni equivalent ya B.Eng,B.Tech in Engineering au Bsc in Engineering
Besides mbaka salutation yake ianze na Engineer ujue huyo mhusika kashatambulika na bodi ya wahandisi na ni engineer kamili(Professional Engineer)
Miaka ya nyuma vyuo vingi vilikuwa vinatoa Advanced Diploma. DIT, UCLAS, MBEYA TECH,CBE, MZUMBE-IDM et al. Sasa kwa wale wahitimu wa Engineering kutoka vyuo hivyo nje ya UDSM ambayo pekee ilitoa degree, walitambuliwa na ERB kama Technician Engineers na wale wa Degree kama Engineers(Graduate Engineer) Ukifanya SEAP na kuandika report ERB unakuwa Professional Engineer, lakini kwa wale wa Advanced walikuwa wanafanya mitihani ya bodi- ERB, na hivyo kuwa Professional Engineer.
Likewise pale UCLAS wengi walisoma Advanced Diploma in Building Economics,wengine Survey na Geormatic et al. Quantity Surveyors wengi tulio nao ambao ni age ya miaka kama45-50 na kuendelea wote hao ni Advanced Diploma kwani pale UCLAS degree ilianzishwa baadae. They are all QS bila kujali ni Advanced au Degree.
Baadae vyuo vingi viliamua ku phase out Advanced Diploma na kuweka Degree, watu wa mwanzo mwanzo wakiwa ni Mzumbe,UCLAS- Ardhi University, baadae DIT, MUST na baadae CBE, TIA na IFM
Hivyo namalizia kwa kusema kama mama Stella alimaliza Advance na kupata cheti na baadae kujisalimisha ERB, huyo ni Engineer halali na inapaswa nimelize kwa kusema honger Eng. Stella Manyanya!
Body ya Wahandisi hutoa barua kwa muhusika kumueleza kuwa kuanzia sasa jina lako litaanzia na initial Eng. mwanzoni au mwiahoni kama hivi:-
1. Eng Invisible
2. Bujibuji PEng( T)
3. Faiza Foxy Grad Eng( Hii ni kwa Muhandisi ambae ni fresh from school, au ambae siyo professional, au ambae hajaandika report ya kuomba kuwa professional, bila kujali kakaa miaka mingapi au ni profesa au Bachelor)
Kama hujapewa barua kufanya hivyo hauruhusiwi kujiita Engineer