Siasa za huku kwetu tumeguza ni elimu. Watu wanadhani mwansiasa mzuri ni yule mwenye elimu fulani ya juu ndio maana unaona wengi wanahangaika kujitambulisha kwa elimu zao.
Ni sababu hiyo hiyo ndio maana unaona hata wakishakuwa ma dk na maprof badala wafanye mambo ya maaana kwa taaluma zao wanakimbilia siasa.
Hapa ndipo nchi ilipoharibikia. Hatutapiga hatua za maana hata baada ya miaka 100. Tutabakia kuwa tegemezi, angalia miaka 50 ya uhuru bado bajeti ya nchi inategemea wafadhili. Wafadhili wakigoma serikali inashindwa kulipa mishahara. Maamuzi mengi yamekaa kisiasa siasa sana. Utaalamu hauzingatiwi tena.
Wanasiasa wameweza kuwaonyesha wasomi popote [pale walipo kuwa wao si chochote na hawana heshima yoyote kitaifa kama hawajawa wanasiasa, na kama hawatawaunga mkono.
Wanasiasa wamehakikisha kuwa mishahara na marupurupu yao vinapanda kila baada ya muda mfupi na kwamba inakuwa minono kupita wasomi waliobobea.
Wataalamu wameacha kazi kwenye maabara za uvumbuzi kwenda kupasua vipaza sauti. Halafu nchi iendelee?
Wanasiasa wamevifunga viwanda nchini, km vya nguo, general tyre nk. nk. sasa wanaviua vya Sukari na Mashamba makubwa.
Letu sasa ni taifa linalokula bidhaa kutoka nje hatuzalishi chochote? Ile mitambo ya kuzalisha vitu tumeruhusu imechomolewa na kupelekwa nchi nyingine, yale majengo yaliyokuwa na ile mitambo yamegeuzwa ghala za kushushia bidhaa kutoka nje tena zisizolipiwa ushuru.
Sisi zaidi tunauza mali ghafi kwa dola moja tunainunua baada ya kugeuzwa bidhaa muhimu kwa dola 50 hadi 100.
Taifa badala ya kuwatunukia wasomi na wataalamu kwa kazi zao za kitaalamu pale walipo, wanawaita ama kuwavuta na kuwapa vyeo vya kisiasa.
Kinachoshangaza sana nchi nyingine hata wakimalza vipindi vyao vya uanasiasa huweza kurudia kwenye fani zao, lakini wetu ama hufia humo au huondoka wakiwa hoi na mara nyingi sana wakiwa "obese".