Mhandisi aliyeelimika vyema na mraibu wa crack anaeleza kwa nini crack inalevya sana (1981)

Madwari Madwari

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
1,110
1,936
Hii video inaongelea madhara ya madawa ya kulevya. Mhandisi wa Mawasiliano Bob Williams. Alijifunza kutumia Crack Cocaine kutoka kwa mchumba wake wa kwanza. Anadai kuwa alitumia dola 50,000 katika miezi tisa ya kwanza ya kuwa mraibu wa crack. Hiyo ni sawa na $165,478.55 katika pesa za leo. Ukibadilisha kwa shilingi ni sawa sawa na 411,351,212.99 Tshs. Anajua kabisa madhara ya Crack lakini bado anaendelea kutumia. Alipata kazi nzuri akaipoteza ndani ya wiki mbili.Miaka ya themanini hali ilikuwa mbaya lakini hiki kilikuwa kitu kipya kwa Serikali ya Marekani. Hali yetu ya leo tuna majanga kama haya lakini ni jambo geni kwa jamii yetu kwa ujumla. Hii hali ya uraibu ni jangwa kubwa sana kwa vijana wa leo. Kuna watu wana taaluma wanaharibu maisha yao kwa sababu ya uraibu. Pia hata ulevi uliokithiri ni Janga tunachukulia poa kuhusu pombe. Inabidi tunywe kistaaarabu. Ukiona una starehe inakuendesha mpaka unashindwa kupanga maisha yako achana nayo. Kuna starehe nyingi sana ambazo zinaleta uraibu ila hatujafunguka na kuzijua kisawasawa. Starehe kama ngono, pombe, ubashiri wa michezo(sport betting) n.k. Binadamu tunajisahau unakuta kuna vitu muhimu unatelekeza kisa unaendekeza starehe. Starehe sio mbaya lakini tuwe tunafanya kwa kiasi.
 

Attachments

  • ENG BOB WILLIAMS.mp4
    13.3 MB

Similar Discussions

Back
Top Bottom