Mhadhiri UDOM aliyetaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi afunguliwa shtaka la uhujumu uchumi

Kutaka uchi na uhujumu uchumi wapi na wapi? Au wanataka kusema watoto wa kike wanatembea na uchumi au uchumi wanao wameukalia?
Aise nimejiuliza Sana uhujumu uchumi kwenye ngono mtu ameomba ngono ili ampe maksi nyingi, hii sielewi imekaje lakini wao ndio walivyoamua . Awamu ya house.
 
Kutaka uchi na uhujumu uchumi wapi na wapi? Au wanataka kusema watoto wa kike wanatembea na uchumi au uchumi wanao wameukalia?
Takukuru imejaa vilaza kama lumumba tu,mahakama nayo ingekua na ueledi hiyo kesi wasipokee mana haieleweki
 
Mpumbavu Huyo....

Kutojiamini kiasi gani kwa MWANAUME mwenzetu kulazimisha NGONO kupitia RUSHWA?!!!!

Yeye anapata fedha,kwanini asizitumie kununua "WAUZAJI" kitaani huko?!!!!

Anataka kumtandazia "gridi" Shemeji yetu mchumba wa WADOGO ZETU....

Funga Huyo.
Mxsxieeeeew
 
LOL... Amehujumu uchumi wa nchi, siyo? Uchumi wa nchi umekaa hapo katikati, siyo? Sitetei alicholifanya lakini jamani hii sheria ya uhujumu uchumi siyo ya kukomoana kweli?
Kibaya zaidi ni kwamba wakikufungulia hii hakuna namna hutoki unakaa huko huko ndani yaani imekaa kukomesha komeshana hivi
 
Walikuwa waislam mkawatoa kwa hila zenu mkaleta watu wa rushwa na wabakaji
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma inatarajia kumfikisha mahakamani Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jacob Nyangusi (43) na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kinyume cha sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa namba 11/2007.

Mkuu wa Takukuru Dodoma, Sosthenes Kibwengo, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema watamfikisha mahakamani leo jijini Dodoma.

Alisema majira ya saa 3 usiku Oktoba 3, 2018 Takukuru ilimkamata Nyangusi akiwa nyumbani kwake eneo la nyumba mia tatu jijini Dodoma muda mfupi kabla hajatekeleza nia ovu ya kufanya ngono na aliyekuwa mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza wa shahada ya Sanaa katika Jiografia na Mazingira.

Alisema awali alipokea taarifa kuwa mtuhumiwa alimtaka mwanafunzi wake kingono kama sharti la kumsaidia ili aweze kufanya mitihani ya marudio na kumuwezesha kufauli katika somo lake.

“Ndipo tukaweka mtego kumkamata baada ya uchunguzi kukamilika na Ofisi ya Mashtaka kuridhia kwa mujibu wa sheria ndipo mtuhumiwa anafikishwa mahakamani,” alisemaKibwengo

===
Pia soma

Mhadhiri UDOM ashikiliwa na Vyombo vya Dola kwa tuhuma ya kutaka rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kike
Ukiitembelea UDOM tabia hii utaiona iko wazi sana. Kuna waalimu UDOM wanahitaji kuelimishwa na kubadilishwa akili. Wengi wamerithi tabia za walioshindikana waliokianzisha chuo, wakitokea UD! Hawafanyi utafiti, bado ni watu wa kuelekezwa na mentors na bahati mbaya wamepewa hata nafasi za utawala kabala ya muda wao.
 
Shitaka hilo litatupwa Uchumi anaotaka kuuhujumu ni upi?
Kungekuwa na ukwepaji kodi?

Ina maana huyo dada ana bikira? Si bora angeliwa tu na gamba anapata ataliwa kwa nusu kuku na failure juu.
Alitaka amfelishe ili serikali ikose pesa ya Ada anayolipa huyo dada .Huko Ni kuhujumu uchumi wa chuo cha UDOM
 
Aise nimejiuliza Sana uhujumu uchumi kwenye ngono mtu ameomba ngono ili ampe maksi nyingi, hii sielewi imekaje lakini wao ndio walivyoamua . Awamu ya house.
Kama alikuwa anasoma kea kupitia bodi ya mikopo Ni uhujumu sababu Kama alikuwa wa kufeli kwa Nini umfaulishe bodi ya mikopo iendelee kumpa mkopo mtu ambaye hakustahili? Huo Ni uhujumu


Pia Kama hakustahili kufeli akataka kumfelisha makusudi na yeye Ni mlipa ada Hilo Ni uhujumu kukinyima mapato chuo kinachokulipa mshahara kwa ngono zake
 
Vyuoni kuna madem wamejaliwa bwana
Ukiwa dhaifu lazima uzalendo ukushinde

Ova
 
Back
Top Bottom