Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

hivi jimbo ni la kutafutiwa?Fikra za kiunua mgongo ktk nafasi za kuchapa kazi kujenga taifa.
 

Kuwa promoted kutoka Assistant Lecturer hadi Lecturer siyo kigezo (kwa vyuo vya Tanzania) cha kusema huyo jamaa amepata PhD!!
 
kila kizuri mnataka kiende kwenye siasa? Nauliza tu kwani mtu makini hawezi kuishi nje ya siasa? Mwacheni mwanazuoni huyu akae nje ya boksi
 
Siyo kila mtru anaejua kuongea ni mtendaji mzuri au mchapa kazi. Mleta mada umeshindwa kupambanua haya, kumbuka, talanta ya kuongea ni tofauti na utendaji!
 


kwa hiyo hata slaa ataendelea kuangukia pua milele? nimekuelewa mkuu
 
Huyu jamaa namkubali yupo njema kwenye kujieleza. Not sure kwenye utekelezaji wa yale anayoyaamini ikiwa ni pamoja na kufuatilia hadi kuona outcomes zake.
 
mie nilijua kwamba mtu anagombea anapokubalika au kwao, sasa hii ya kutafutiwa jimbo ni balaa
 
Ni kweli ndugu yangu! Huyu mtu ni dhaifu. Na ana tatizo la kudhani yeye ndo muislam msomi. Kutana naye masjid, ongea naye ndo utamuelewa.

Tatizo pia kwa mtoa mada. Anamsifia kwa Kuwa amemsikia redioni au TV na kudhani Ana sifa hizo. Wako wengi bora kuliko yeye. Kuhojiwa na vyomblo vya habari haiendani na umakini wake. Ni kwa sababu anapatikana anapohitajika.

Kwa ujumla sijawahi kusikia uchambuzi wa kisomi toka kwake.
 
haha..mmeshafikia hapo?Si wa kile kitengo cha wapiga matarumbeta wa kukodi toka chuo kilichoipa nchi hasara UDSM.?Haha...napita tuu.
jina lake(BASHIRU UHADI).. linadhihirisha DINI YAKE..
na kwa uwezo wake wa kitaaluma na ushawishi, unadhani atakuwa tishio kwa wale WAMILIKI WA CHAMA(CHAGAZ)
kwa dini,kabila na uwezo wake nina hakika hamuwezi kumkubali na nashukuru UMETUDHIHIRISHIA HIVYO..
NAKUPENDEA HAPO TUU UNAPOTANGULIZAGA CHUKIIIIIII
 

Sikumjua huyu bwana vizuri ila majuzi kwa kumsikiliza BBC nimemwona akijipambanua very clearly kuwa ana UDINI mkubwa sana hasa ukimchokoza na masuala ya Marekani Vs Ugaidi hapo anakosa kujizuia na kutiririka kuutetea Uislam.

Huyu siyo mtu neutral nafikiri wako na Prof. Lipumba. Siku si nyingi atapoteza umaarufu kama akiendelea ktk mrengo huo wa kutetea dini yake.
 
Subiri katiba mpya mtakoma. Wabunge hawaruhusiwi kuwa mawaziri!! Safi sana, maana vituko vya wasomi kukimbilia bungeni ni kupata nafasi za ulaji za uwaziri na unaibu waziri. Ningefurahi kama mapendekezo yangu yangeingia kwenye Katiba Mpya kuwa Mbunge mwenye aliyekuwa mtumishi wa umma atapata mshahara na marupurupu sawa na ule aliokuwa akipata kabla ya kuwa mbunge!
 
haha..mmeshafikia hapo?Si wa kile kitengo cha wapiga matarumbeta wa kukodi toka chuo kilichoipa nchi hasara UDSM.?Haha...napita tuu.
He does not fit in to your CDM system because of the following three concrete reasons...
1. he is neither chaga nor chaga oriented person
2. he is muslim and its your culture(CDM) to hate and marginalizing muslims
3. he is so smart to be dragged by uneducated CDM leaders that do not want knew challenges and ideas.
kwa chama chenu, watu wa maana ni kama wewe na wenzio wenye akili FUPI KAMA MAISHA YA FUNZA ila kwa wale wanojielewa na waliojaaliwa akili na upeo mkubwa, huwa ni maadui.
zitto kabwe,prof safari,kitila mkumbo,mwesiga baregu n.k mnawaona kama wahaini tuuuuu
 
He is good in every aspect, tatizo ni jina lake.....
 

Fixed point,
Umesema niliyotaka kusema. Nyongeza tu ni kuwa maendeleo ya Taifa letu yanahitaji wataalam waadilifu na wanaoweka mbele maslahi ya Taifa katika nyanja zote za maendeleo hususani uchumi, siasa, huduma za jamii (kama afya, elimu n.k). Natambua umuhimu wa kuwa na wanasiasa wazuri na wenye weledi wa hali ya juu kwa sababu ndio wawakilishi katika vyombo vya kutunga sheria, maamuzi na wasimamizi wakuu wa serikali kwa niaba ya wananchi. Lakini hii haimanishi kuwa wasomi wote waende kwenye siasa, kwa sababu pia sheria nzuri zitakazotana na siasa zinahitaji watendaji wazuri watakao tekeleza maamuzi ya wanasiasa.

Tatizo kubwa la nchi yetu ni mfumo wa kimaslahi ambao umependelea kwa kiasi kikubwa kundi la wanasiasa na ku slideline kada nyingine karibu zote muhimu katika nyanja za uzalishaji na huduma. Matokeo yake sasa kila mtu anaona namna rahisi ya kutoka kimaisha ni kuwahi kwenye siasa hata kama kiuhalisia huyu mtu sio mwanasiasa. Mifano ipo mingi. Tunawafahamu wasomi wengi ambao kabla ya kuingia kwenye siasa, walikuwa watendaji wazuri sana kwenye taaluma zao, lakini leo hatuoni wanafanya nini. Kibaya zaidi mfumo wa uongozi hasa wa chama tawala ni wa kunyamazishana zaidi na kulazimishana kutii 'the machinery' kuliko kusikiliza na kuheshimu mawazo ya kila mmoja. Maslahi wamepata, lakini hakuna walichosaidia jamii ya Tanzania!

Kwa kifupi, tunahitaji kuweka uwanja sawa (the playing ground) kiumfumo na kimaslahi kwa kada zote ili anayetaka kwenda kwenye siasa aende si kwa sababu ya maslahi tu, bali kwa sababu anaona huko ndio anaweza kufanya vzr zaidi. Vivyo hivyo, anayetaka kuwa mchumi, daktari, mwalimu, muuguzi, afisa ugani, mkulima, mfanyabiashara n.k. naye afanye hivyo akijua ana mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa na anastahili ujira na maslahi yake halali kwa kazi hiyo.
 
Akiingia kwenye hawezi kuwa na hiyo misimamo yake km ni cdm ajue kina Mbowe watamdrive na atageuka kuwa mburula. Mwache aeneze maarifa.

Mbona Dr. Kitila Mkumbo hajageuka mburula wakati kila siku anatoa taauma runingani, tena za maana!!!!!! Sema hajaamua!!! Akiamua ataingia siasa kama atakavyochagua mwenyewe!!!! CDM off course imejaa wasomi, wenye weledi!!!!! Na kwa taarifa wako wengi wasomi wamebeba kadi ya chama cha majambazi ila kura yao ni CDM!!
 
Kama anataka kufanikiwa anatakiwa ajipambanue na makamanda wa ukombozi wa pili wa taifa letu, vinginevyo aamue kuendelea kufundisha na kubwabwaja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…