Mh. Samwel Sitta asibezwe, bali anahitaji kuungwa mkono

Mdachi Simple

Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
11
Reaction score
3
Mwenyekiti wa BMK hupaswi kubezwa, anapaswa kupongezwa. Tume ya warioba imekusanya maoni kutoka kwawatanzania 350000 tu. Katiba mpya ni mchakato wa wananchi ambapo mawanda mapana ya ushiriki wao ni jambo la msingi. Ingawa tume ya warioba ilikusanya maoni lakini bado Kuna makundi ya watu wanaona bado hawajafikiwa na Sauti Yao haijasikika. Wana haki ya kusikilizwa na sauti yao kupazwa. Sheria imetungwa lakini utekelezaji na usimamizi wake kunahitaji busara na hekima ukizingatia BMK ni chombo Cha mwisho ambacho kitakuja na rasimu ya mwisho ambayo itakwenda kupigiwa kura na wananchi. Hivyo umakini mkubwa unahitajika. ImageUploadedByJamiiForums1409044929.878368.jpg
 
  • Thanks
Reactions: gsu
Tupo pamoja na sitta tunajua anafanya kazi ya watanzania wengi tunaotegemea kupatikana katiba mpya.
 
Mwenyekiti wa BMK hupaswi kubezwa, anapaswa kupongezwa. Tume ya warioba imekusanya maoni kutoka kwawatanzania 350000 tu. Katiba mpya ni mchakato wa wananchi ambapo mawanda mapana ya ushiriki wao ni jambo la msingi. Ingawa tume ya warioba ilikusanya maoni lakini bado Kuna makundi ya watu wanaona bado hawajafikiwa na Sauti Yao haijasikika. Wana haki ya kusikilizwa na sauti yao kupazwa. Sheria imetungwa lakini utekelezaji na usimamizi wake kunahitaji busara na hekima ukizingatia BMK ni chombo Cha mwisho ambacho kitakuja na rasimu ya mwisho ambayo itakwenda kupigiwa kura na wananchi. Hivyo umakini mkubwa unahitajika.View attachment 180398
Waryoba alikuwa anaongozwa na wanaharakati, hakuwa anakusanya maoni ya wananchj
 
Bunge la Katiba si mahali pa kukusanya maoni. Mchakato wa kukusanya maoni ulifanyika kisheria na ukapitishwa hadi kuunda hilo Bunge la Katiba. Acheni kupotosha na kuhalalisha uharamia ambao mnawafanyia Watanzania. Hata hivyo jambo moja ni wazi na hakika. Hiyo katiba haramu inayoandikwa chini ya uongozi wa Sita haitakubaliwa na wananchi wa Tanzania.
 
Tupo pamoja na sitta tunajua anafanya kazi ya watanzania wengi tunaotegemea kupatikana katiba mpya.

Sitta mwenyewe kwenye kikao cha CC ya CCM amewahakikishia kuwa atatoka na Katiba ikayokidhi matakwa ya wananchi, lazima tuuungane naye ili kuepusha balaa la UKAWA la kutaka kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na msingi wowote
 
Bunge la Katiba si mahali pa kukusanya maoni. Mchakato wa kukusanya maoni ulifanyika kishria na ukapitishwa hadi kuunda hilo Bunge la Katiba. Acheni kupotosha na kuhalalisha uharamia ambao mnawafanyia Watanzania. Hata hivyo jambo moja ni wazi na hakika. Hiyo katiba haramu inayoandikwa chini ya uongozi wa Sita haitakubaliwa na wananchi wa Tanzania.

Ndiyo maana ya Bunge kuwa na mamlaka ya kuongeza au kupunguza na nata kubadili kikichoko kwenye rasimu ya wanaharakati na Waryoba wao. Haiwezekani makundi mengine yasiguswe kwenye rasimu halafu mambo yakaachwa kama yalivyo.
 
Mwenyekiti wa BMK hupaswi kubezwa, anapaswa kupongezwa. Tume ya warioba imekusanya maoni kutoka kwawatanzania 350000 tu. Katiba mpya ni mchakato wa wananchi ambapo mawanda mapana ya ushiriki wao ni jambo la msingi. Ingawa tume ya warioba ilikusanya maoni lakini bado Kuna makundi ya watu wanaona bado hawajafikiwa na Sauti Yao haijasikika. Wana haki ya kusikilizwa na sauti yao kupazwa. Sheria imetungwa lakini utekelezaji na usimamizi wake kunahitaji busara na hekima ukizingatia BMK ni chombo Cha mwisho ambacho kitakuja na rasimu ya mwisho ambayo itakwenda kupigiwa kura na wananchi. Hivyo umakini mkubwa unahitajika.View attachment 180398

hata kikwete hakuchaguliwa na nwananchi wote.
 
Waryoba alikuwa anaongozwa na wanaharakati, hakuwa anakusanya maoni ya wananchj

Naweza kuamini hili nikiangalia mtiririko wa matukio anayoyafanya yeye na wajumbe wenzake tangu tume hiyo ilipovunjwa kisheria.
 
Kama ndio hivyo unavyodai, kwa nini jambo hilo halikujadiliwa na rasimu kupingwa, kabla haijapitishwa kishwria na Bunge la Katiba kuundwa? Hayo ndiyo mnayaona leo? Mtapindisha we sheria lakini mwisho wa siku sheria itachukua mkondo wake.
 
Nina hakika Sita hajui mipaka ya kuongoza familia yake! Hivi yeye anaweza kwenda kwa wakwe zake na kutoa maagizo?! Au je mkewe anaweza kwenda kwa baba yake sita na kuanza kutoa maelekezo?!

Sita anapaswa kufahamu kuwa uongozi wake kifamilia unaishia kwa mkewe na watoto wake! Sidhani kama hua anakaribisha ndugu zake au wa mkewe kuongoza familia yake!!

Kwa muungano huu mambo ya Watanganyika ni ya Watanganyika tu! Na mambo ya Wazanzibari ya Wazanzibari peke yao!

Tushirikiane katika mambo ya muungano na si vinginevyo!
 
Ulichokisema ni jambo muhimu sana. Watu wanachangia kwa ushabiki. Kimsingi Sitta aungwe mkono.
 
Mwenyekiti wa BMK hupaswi kubezwa, anapaswa kupongezwa. Tume ya warioba imekusanya maoni kutoka kwawatanzania 350000 tu. Katiba mpya ni mchakato wa wananchi ambapo mawanda mapana ya ushiriki wao ni jambo la msingi. Ingawa tume ya warioba ilikusanya maoni lakini bado Kuna makundi ya watu wanaona bado hawajafikiwa na Sauti Yao haijasikika. Wana haki ya kusikilizwa na sauti yao kupazwa. Sheria imetungwa lakini utekelezaji na usimamizi wake kunahitaji busara na hekima ukizingatia BMK ni chombo Cha mwisho ambacho kitakuja na rasimu ya mwisho ambayo itakwenda kupigiwa kura na wananchi. Hivyo umakini mkubwa unahitajika.View attachment 180398

Wewe mdach simple hoja yako sio ya kweli,kama wanakusanya nan anayeyaratibu maoni hayo? lini yatawaslishwa ili tuyasikie? nan kakwambia maoni yanakusanywa kwa siri,maoni ni hadharan,kama warioba hakuja na maoni yanayoridhisha ya wtz wengi kwann haukuongezewa muda?
Pia nikuelimishe inayotoka bmk sio rasimu bali ni katiba inayopendekezwa
 
Back
Top Bottom