Mh Rais umenishtua!

Mh Rais umenishtua!

Kizotaka

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
561
Reaction score
107
ni kweli Mh JK amenishtua. leo amewakaribisha wa Turkish kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwamo kilimo! yani kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa huru na kujitawala,leo tunamkaribisha bepari aje kuwekeza kwenye kilimo! ilitakiwa tuwaambie tuna hotculture products bora,pamba bora kahawa bora,korosho bora,ngano bora katani bora,ndizi bora tunahitaji soko wafungue milango. wawekeze kwenye kilimo!?!wasaidie kilimo kwanza au!? kilimo kwanza kimeshindwa hadi mnakaribisha mabepari kuwekeza kwenye kilimo! shame on us, shame to the government. Sikubaliani hata chembe na Mh JK hata chembe katika hili,totally sounds like a fail government
 
Watanzania ni watu wa kulialia tu muda wote. Sasa kama wewe uliyetakiwa uje kuwa mwekezaji ndiyo umeamua kuwa mchumia tumbo wa CHADEMA, unaanzisha thread zako za kiPropaganda, ulitaka serikali ifanyeje?
 
Mkuu umekalia msumali wa moto nini??mbona unakurupuka kama wanakuserukamba???
 
ni kweli Mh JK amenishtua. leo amewakaribisha wa Turkish kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwamo kilimo! yani kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa huru na kujitawala,leo tunamkaribisha bepari aje kuwekeza kwenye kilimo! ilitakiwa tuwaambie tuna hotculture products bora,pamba bora kahawa bora,korosho bora,ngano bora katani bora,ndizi bora tunahitaji soko wafungue milango. wawekeze kwenye kilimo!?!wasaidie kilimo kwanza au!? kilimo kwanza kimeshindwa hadi mnakaribisha mabepari kuwekeza kwenye kilimo! shame on us, shame to the government. Sikubaliani hata chembe na Mh JK hata chembe katika hili,totally sounds like a fail government
ccm wanarudisha nchi yetu kwa wakoloni tena!
 
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!
 
Siyo Waturuki tu. Amewakaribisha Wamarekani, amewakaribisha Wasaudia, wote watapewa maelfu ya ekari kwa mikataba ya miaka 99 na sisi anasema ni "watu wa pembezoni." Kazi yetu itakuwa ni kuwachotea maji, kuwakatia kuni na kuwaoshea sahani zao baada yao kula. Tanzania ni shamba la bibi wewe!
 
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!

Songoro,
Naomba utufungue macho kuhusu kilimo cha Botswana. Ni nani anayelima huko? Ni Mturuki pia?
 
Ninakerwa sana na wawekezaji wanaoletwa nchini na serikali ya CCM.Mambo anayofanya Kikwete kuhusu uwekezaji ni pigo kubwa kwa Watanzania hasa katika kuendeleza nchi yao!
 
Watanzania ni watu wa kulialia tu muda wote. Sasa kama wewe uliyetakiwa uje kuwa mwekezaji ndiyo umeamua kuwa mchumia tumbo wa CHADEMA, unaanzisha thread zako za kiPropaganda, ulitaka serikali ifanyeje?

Ndugu mbona una panick,mimi nimekosoa juhudi za serikali kuwekeza kwenye maendeleo ya kilimo. kwanini tumbabaike mwekezaji kwenye kilimo,ulioutiwa uti wa mgongo.ya chadema yametokea wapi?
 
Irudishe fedha za uswizi ziwekeze katika kilimo, Watanzania ni mbumbumbumbumbumbu sana sana sana sana, Hebu kukataa hili niambie tangu raisi wetu ameanza kutembea huko ughaibuni na wa ughaibuni kuja tanzania niambie ni lini ulisikia watanzania tunatakaribishwa kwenda kuwekeza huko kama si wao na sisi kuwambia njoeni muwekeze kwetu. Hivi kwa nini kila siku waje wawekeze tanzania na si tanzania kuwekeza kwao?
 
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!
songoro,kumbuka hawa hawawezi kulima kwa manufaa yetu, kilimo kwanza kimeshindwa,kweli serikali inafanya juhudi za dhati kumkombo mkulima. hembu fuatilia habari za kigoda cha mwalimu kilichomalizika juzi
 
ni kweli mh jk amenishtua. Leo amewakaribisha wa turkish kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwamo kilimo! Yani kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa huru na kujitawala,leo tunamkaribisha bepari aje kuwekeza kwenye kilimo! Ilitakiwa tuwaambie tuna hotculture products bora,pamba bora kahawa bora,korosho bora,ngano bora katani bora,ndizi bora tunahitaji soko wafungue milango. Wawekeze kwenye kilimo!?!wasaidie kilimo kwanza au!? Kilimo kwanza kimeshindwa hadi mnakaribisha mabepari kuwekeza kwenye kilimo! Shame on us, shame to the government. Sikubaliani hata chembe na mh jk hata chembe katika hili,totally sounds like a fail government

namnukuu,bw,khamisi swedi kagasheki,,,,,,hardhi,,,yote tanzania,ni mali ya bwana mkubwa,rais,hakuna mtanzania yoyote mwenye hati miliki ya hardhi,kuwa mali yake isipokua umilikiswa kwa miaka,36,99,mwisho wa kumnukuu,,sasa kwa maneno haya na kwa katiba hii ya sasa inampa rais dilitu za kutuuza kila anapotaka,wewe huoni anavyo safiri na kaulimbiu yake ni kwenda kutafuta wawekezaji,wanaokuja kupewa maekari ya mashamba,alafu watanzania wanatolewa kama wakimbizi juu ya hardhi yao,watanzania wenzangu tuamke nchi inauzwa kwa kasi ya fasti jet,,,lakwanza ni kupigania hakizetu zinazotaka kuporwa na ccm kwenye mchakato wa katiba,ya sasa,na kuakikisha rais anakua mtumishi na sio mungu mtu,mimi katika maisha yangu sijaona wazungu waki omba omba,misaada kama matonya,na nchi zao hazina utajiri wa rasilimali kama africa,ebu tujiulize wa tanzania tumelogwa na nani,nchi tajiri kama tanzania,bado viongozi wanabeba mabakuli,nchi za nje na kuomba omba kama matonya,haya gesi imeshapatikana,hata wazungu wanatucheka sana kila siku utasikia wawekezaji wawekezaji,uhu ni ujinga wa kufikiriatu kwa serikali ya ccm,
 
Tutasikia mengi mpaka atoke madarakani, next atawaomba wazungu waje kuwekeza kwa wake zetu.
 
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!

Mwenyeheri Julius Nyerere
 
Tanzania tuna good laws and policy but we lucky good leadership
 
Ndugu mbona una panick,mimi nimekosoa juhudi za serikali kuwekeza kwenye maendeleo ya kilimo. kwanini tumbabaike mwekezaji kwenye kilimo,ulioutiwa uti wa mgongo.ya chadema yametokea wapi?

Kizotaka, kama huna habari ni kwamba kwa mujibu wa propoganga iliypikwa na kuiva pale Lumumba - ye yote anayeikosoa serikali au kulalamika kuhusu utendaji mbovu wa serikali ya CCM huyo moja kwa moja anavalishwa beji ya CHADEMA. Ndio maana unaona mkakati mpya wa Waheshimiwa Wabunge wa CCM katika kuchangia hoja bungeni: kabla ya kuanza kueleza mapungufu ya bajeti ya serikali wanaanza na 'sala' ya kulaani CHADEMA (wawafurahishe watawala), kisha wanaeleza mapungufu hususan serikali kushindwa kutoa huduma stahiki majimboni mwao (wawafurahishe wapiga kura) na kisha kumalizia kwa kuunga mkono bajeti kwa asilimia mia (ili wasije kupewa beji ya u-CDM). Ndo bongoland inavyodidimia hivyo.
 
Watanzania ni watu wa kulialia tu muda wote. Sasa kama wewe uliyetakiwa uje kuwa mwekezaji ndiyo umeamua kuwa mchumia tumbo wa CHADEMA, unaanzisha thread zako za kiPropaganda, ulitaka serikali ifanyeje?
Hii kweli ni Sumu! CCM & CDM...
 
Last edited by a moderator:
Songoro,
Naomba utufungue macho kuhusu kilimo cha Botswana. Ni nani anayelima huko? Ni Mturuki pia?

hoja ni mwekezaji mwenye mtaji wa kutosha hata akiwa Mngindo haina shida, au tatizo la mleta mada ni kwa kuwa mwekezaji mwenyewe ni Mturuki? Hata Nyerere mwenyewe hakuwa na mafanikio kwenye kilimo cha kijamaa
 
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!

Wataenda mara ngapi? Cheki humu News kuna baadhi.
 
songoro,kumbuka hawa hawawezi kulima kwa manufaa yetu, kilimo kwanza kimeshindwa,kweli serikali inafanya juhudi za dhati kumkombo mkulima. hembu fuatilia habari za kigoda cha mwalimu kilichomalizika juzi

Achana na siasa za Kigoda cha mwl kwenye Kilimo, Mwl mwenyewe hana mafanikio kwenye sekta ya kilimo tatizo la wabongo ni kuweka mbele siasa kwenye kila kitu, Huna mtaji, soko,utaalam lakin unaota kuwa Na Estates za kilimo cha biashara.Kuongea na kutekeleza ni vitu viwili tofauti hivi sasa watu hawajadili kuingia kwenye mfumo wa kibapari bali wanajadili jins ya kuish na Ubepari hicho kigoda kinazungumzia Utopian Socialism ulomshinda even muasisi wake.
 
Back
Top Bottom