Mh. Rais sitisha ujenzi wa stendi za mabasi ya Nyamhongoro na Nyegezi Jijini Mwanza

Hili wazo la kujenga stand kubwa eneo la FELA ni wazo zuri sana, kwanza kuna station ya treni hapo hivyo abiria wa treni hatalazimika kufika mjini, atateremkia fela na kukamata usafiri wa bukoba geita musoma, stand za nyegezi na nyamhongolo zibaki kwa ajili ya daladala za mjini, lakini stand kuu ijengwe FELA kwa kweli,
Umeona mzee? Tunaule ushamba wa kulundika kila kitu katikati ya mji, miji itakuwaje sasa ? Unapeleka station ya standard gauge pale mwanza mjini, abiria wakishuka ndio waanze sasa kubanana kutoka nje ya mji, jam zitapungua kweli?
 
Hivi ni Njia gani Muafaka ya Kuufikisha Ujumbe Huu kwa Serikali Kuu au kwa Raisi Mwenyewe. Nadhani tunawajibikwa kwa hili kama Wazalendo wa Kweli, nipeni njia nilifikishe hili.
Labda tuombee apite hapa JF sababu naamini hata yeye akitafakari atasitisha huu mradi, ni akili za kijinga kujenga stendi nyegezi pale au nyamhongoro
 
Mawazo mazuri sana haya . Ndugu zetu wa mipango miji wangeyazingatia kwa kweli. Tatizo sasa utakuta kuna watu wachache ambao kwa namna fulani wanafaidika stendi ikijengwa Nyegezi, hivyo watatetea mpaka ijengwe hapo na hata rushwa zitatembea ili kukidhi haja. Suala hili lifikishwe tu ngazi za juu kwa mujibu wa taratibu. Naamini hata Mh. Rais Magufuli akiliona na hoja za msingi zilizotolewa atatoa maagizo ipasavyo. Sasa je litamfikia kwa wakati?

Suala la msingi kabisa na lipo wazi kwanini muombe msaada wa Rais kwa maamuzi yenu? kwa mtu mwenye akili timamu nani sasa hivi atashauri kujenga stendi pale Nyegezi?
 
Mh. Rais, serikali yako imetenga mabillion ya pesa kwa ujenzi wa stendi za mabasi katika maeneo ya Nyamhongoro na Nyegezi jijini Mwanza, hili ni jambo zuri la kupongezwa katika juhudi za kuboresha miundombinu ya miji yetu,

Mh Rais najua unalifahamu vizuri jiji la mwanza ndio maana naandika haya kama mwanachi ninayeguswa na maendeleo ya Taifa letu.

Jiji la Mwanza kwa sasa limebanana sana maeneo yanayotaka kujengwa stendi hayafai kabisa kwa sasa na hata kwa baadae, tuomba uingilie kati hili suala otherwise tutafanya mambo kama watu tusiokuwa na maono wala fikra za baadae ili tu kufanikisha malengo ya wanasiasa fulani.

USHAURI : Mh Rais sehemu nzuri na ambayo ipo strategic kwa stendi ya nyamhongoro ni kisesa na kwa Nyegezi ni Nyashishi, suala la mivutano ya mapato kati ya halmashauri na mambo ya kitoto na yasiyoangalia maslahi mapana ya ujenzi wa taifa letu.

Kama itakupendeza Mh Rais ni bora kuirudisha Kisesa na Usagara ndani ya jiji ili kuondoa hii mivutano ambayo naona haina tija kabisa.

Stendi ikijengwa kisesa itasaidia magari yanayoenda Dar na mikoa mingine yanayotokea musoma kutoingia jijini bali kupitia njia mpya ya kisesa -usagara iliyojengwa na serikali yako

Pia Mh Rais unaweza amua kuunganisha pesa za hii miradi miwili ukajenga stendi moja kubwa na ya kisasa maeneo ya FELA itakayohudumia mabasi ya yote ya mikoani na daladala zitafanya kazi za kusomba watu, kwanza itachochea uwekezaji katika hayo maeneo na kukuza miji yetu.

Hata station kubwa ya abiria wa standard gauge ningeshauri ijengwe FELA kuliko kuipeleka katikati ya jiji

Ikikupendeza Mh Rais naomba ulifikilie wazo langu kwa kina, ujenzi wa hizi stendi kwa miaka michache ijayo hazitakuwa na tija tena na itabidi kuhamisha tena.
Mmemfanya rais kama Mungu mtu, huko chini kote hakuna mchakato wa kulifanyia kazi hili mpaka kila kitu kiletwe kwa rais?
 
Tanzania rais amefanywa kama Mungu mtu.

Kikatiba rais amepewa mamlaka makubwa sana.

Kichama rais ndiye mwenyekiti wa chama tawala.

Anateua kuanzia mabalozi, mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wakuu wa mashirika ya umma, mpaka wenyeviti wa tume ya uchaguzi.

Halafu zaid ya hapo, hata mambo ya serikali za mitaa huku chini bado watu wanamlilia rais?

Huyo rais watu hawaoni kwamba wanamkuza kuliko uwezo wa mtu?
 
Bado Nyegezi kuna eneo kubwa kwa nyuma kama utampata design mzuri wa kujenga na kubobomoa vijibanda vibanda.Ishu nyingine halmasharu ya jjiji la mwanza kuiachia stendi kwa sababu Nyashishi ipo Misungwi.Kwa hiyo jiji litakosa mapato.Ushauri mwingine ile barabara ijengwe to two lane toka town mpaka usagala itakuwa poa.
 
Stand ya nyegezi kubaki pale sio sawa wazee. Hii stand mahala pake ni usagara. Asubuhi mabasi yakiwa yanatoka stand Kuna kua na foleni Sana kuyasubiri yaishe.
 
Mmemfanya rais kama Mungu mtu, huko chini kote hakuna mchakato wa kulifanyia kazi hili mpaka kila kitu kiletwe kwa rais?
Ni mungu mtu ndio, sasa unafikili nani anaweza saidia kwa haraka? Hao watendaji wamebaki kubishania mapato na jinsi gani watafaidika na mradi, hawaangalii kabisa faida na hasara, ndio maana tumeamua kwa huyo unaemuita mungu mtu ili asaidie kulitatua
 
Sina hakika kama Rais Maguful yupo Jf?
Nafkir ni bora ukatumia njia respective ya kutoa Maoni kwa nia njema kabisa ambayo unayo ili yafanyiwe kazi..
Failure that watasoma Post hii watu mbal mbali kutoka sekta mbal mbal za Gv.
Mh. Rais, serikali yako imetenga mabillion ya pesa kwa ujenzi wa stendi za mabasi katika maeneo ya Nyamhongoro na Nyegezi jijini Mwanza, hili ni jambo zuri la kupongezwa katika juhudi za kuboresha miundombinu ya miji yetu,

Mh Rais najua unalifahamu vizuri jiji la mwanza ndio maana naandika haya kama mwanachi ninayeguswa na maendeleo ya Taifa letu.

Jiji la Mwanza kwa sasa limebanana sana maeneo yanayotaka kujengwa stendi hayafai kabisa kwa sasa na hata kwa baadae, tuomba uingilie kati hili suala otherwise tutafanya mambo kama watu tusiokuwa na maono wala fikra za baadae ili tu kufanikisha malengo ya wanasiasa fulani.

USHAURI : Mh Rais sehemu nzuri na ambayo ipo strategic kwa stendi ya nyamhongoro ni kisesa na kwa Nyegezi ni Nyashishi, suala la mivutano ya mapato kati ya halmashauri na mambo ya kitoto na yasiyoangalia maslahi mapana ya ujenzi wa taifa letu.

Kama itakupendeza Mh Rais ni bora kuirudisha Kisesa na Usagara ndani ya jiji ili kuondoa hii mivutano ambayo naona haina tija kabisa.

Stendi ikijengwa kisesa itasaidia magari yanayoenda Dar na mikoa mingine yanayotokea musoma kutoingia jijini bali kupitia njia mpya ya kisesa -usagara iliyojengwa na serikali yako

Pia Mh Rais unaweza amua kuunganisha pesa za hii miradi miwili ukajenga stendi moja kubwa na ya kisasa maeneo ya FELA itakayohudumia mabasi ya yote ya mikoani na daladala zitafanya kazi za kusomba watu, kwanza itachochea uwekezaji katika hayo maeneo na kukuza miji yetu.

Hata station kubwa ya abiria wa standard gauge ningeshauri ijengwe FELA kuliko kuipeleka katikati ya jiji

Ikikupendeza Mh Rais naomba ulifikilie wazo langu kwa kina, ujenzi wa hizi stendi kwa miaka michache ijayo hazitakuwa na tija tena na itabidi kuhamisha tena.
 
Sina hakika kama Rais Maguful yupo Jf?
Nafkir ni bora ukatumia njia respective ya kutoa Maoni kwa nia njema kabisa ambayo unayo ili yafanyiwe kazi..
Failure that watasoma Post hii watu mbal mbali kutoka sekta mbal mbal za Gv.
Hizo njia tutatizoa wapi mkuu? Ni kama kilio cha samaki, kama kuna muungwana atamfikishia tutashukuru, sababu kuna watu wapo JF na wana access nae
 
Kama maamuzi ni kujenga standi kuu ya Mwanza nyegezi uamuzi huu uyakuwa ni wa watawala na sio wananchi.
Kwa sasa nyengezi ni Katikati ya jijk na ili kipanua mji stand kui inapaswa kujengwa Usagara na ikishindikana sana ni Nyashishi.
 
Hata hivyo SG inaishia Fela nijuavyo ndio maana issue za ubomoaji zilisimama kupisha SG huku mjini.
Suala la stand ni huo mvutano wa mapato ndio chanzo kinachosemekana.
 
Ni mungu mtu ndio, sasa unafikili nani anaweza saidia kwa haraka? Hao watendaji wamebaki kubishania mapato na jinsi gani watafaidika na mradi, hawaangalii kabisa faida na hasara, ndio maana tumeamua kwa huyo unaemuita mungu mtu ili asaidie kulitatua
Tatizo ukishaanza kuandika "unafikili" naweza kuelewa kwamba hata Kiswahili hujui, na ndiyo maana hatuelewani.
 
Sawa mwalimu wa kiswahili, naona upo kazini, anyways, sina shida yangu ujumbe ufike, we endelea kupitia comments na kufanya masahihisho ya grammar
 
Kama maamuzi ni kujenga standi kuu ya Mwanza nyegezi uamuzi huu uyakuwa ni wa watawala na sio wananchi.
Kwa sasa nyengezi ni Katikati ya jijk na ili kipanua mji stand kui inapaswa kujengwa Usagara na ikishindikana sana ni Nyashishi.
Ndio wameshaamua hivyo, na contractors wameshaanza kazi za awali, ndio maana tunamuomba JPM aingilie kati
 
Back
Top Bottom