Mh. Rais sitisha ujenzi wa stendi za mabasi ya Nyamhongoro na Nyegezi Jijini Mwanza

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Mh. Rais, serikali yako imetenga mabillion ya pesa kwa ujenzi wa stendi za mabasi katika maeneo ya Nyamhongoro na Nyegezi jijini Mwanza, hili ni jambo zuri la kupongezwa katika juhudi za kuboresha miundombinu ya miji yetu,

Mh Rais najua unalifahamu vizuri jiji la mwanza ndio maana naandika haya kama mwanachi ninayeguswa na maendeleo ya Taifa letu.

Jiji la Mwanza kwa sasa limebanana sana maeneo yanayotaka kujengwa stendi hayafai kabisa kwa sasa na hata kwa baadae, tuomba uingilie kati hili suala otherwise tutafanya mambo kama watu tusiokuwa na maono wala fikra za baadae ili tu kufanikisha malengo ya wanasiasa fulani.

USHAURI : Mh Rais sehemu nzuri na ambayo ipo strategic kwa stendi ya nyamhongoro ni kisesa na kwa Nyegezi ni Nyashishi, suala la mivutano ya mapato kati ya halmashauri na mambo ya kitoto na yasiyoangalia maslahi mapana ya ujenzi wa taifa letu.

Kama itakupendeza Mh Rais ni bora kuirudisha Kisesa na Usagara ndani ya jiji ili kuondoa hii mivutano ambayo naona haina tija kabisa.

Stendi ikijengwa kisesa itasaidia magari yanayoenda Dar na mikoa mingine yanayotokea musoma kutoingia jijini bali kupitia njia mpya ya kisesa -usagara iliyojengwa na serikali yako

Pia Mh Rais unaweza amua kuunganisha pesa za hii miradi miwili ukajenga stendi moja kubwa na ya kisasa maeneo ya FELA itakayohudumia mabasi yote ya mikoani na daladala zitafanya kazi za kusomba watu, kwanza itachochea uwekezaji katika hayo maeneo na kukuza miji yetu.

Hata station kubwa ya abiria wa standard gauge ningeshauri ijengwe FELA kuliko kuipeleka katikati ya jiji, SGR station ya Mwanza ikijengwa FELA na stendi kubwa ya mabasi ikijengwa FELA na kituo kikubwa cha daladala design ya kama kile cha mbezi basi tutakuwa ni watu tunaofikilia miaka 30 mbele, hata ikitokea Mwanza ikapata mradi Wa mwendo kasi itajengwa Kwa mpangilio unaoeleweka.

Ikikupendeza Mh Rais naomba ulifikilie wazo langu kwa kina, ujenzi wa hizi stendi kwa miaka michache ijayo hazitakuwa na tija tena na itabidi kuhamisha tena.
 
Manofu

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
1,312
2,000
Unalionaje wazo lakini? Sababu pale pamebanana sana mkuu, angalia stendi ya Ubungo imehama,, sasa jiulize nyegezi na Nyamhongoro tayari pamebanana, ningependa mipango yetu iwe inaangalia mbali, hayo maeneo ni kuongeza jam tu
Sasa pale nyegezi wanataka kuijenga wapi maana ile yenyewe iliyopo ni ndogo na maeneo ya wazi kwa sasa hakuna kwenye eneo la nyegezi. By the way hivi kisesa inaludi mwanza au Magu?
 
Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Sasa pale nyegezi wanataka kuijenga wapi maana ile yenyewe iliyopo ni ndogo na maeneo ya wazi kwa sasa hakuna kwenye eneo la nyegezi. By the way hivi kisesa inaludi mwanza au Magu?
ndio swali hata mimi nilikuwa najiuliza hivi wataalamu wetu wanaangalia mbali kweli? Kwa ufupi stendi inajengewa pale pale nyegezi ndio maana nimeandika hili ili Mh Rais azishtue akili zao, hauwezi kuwa na fikra sahihi kwa kujenga stendi nyegezi
 
Na issue kubwa ni mvutano wa mapato sababu Nyashishi ipo wilaya ya misungwi na kisesa ipo magu so jiji wanaona hii miradi ikienda huko watakosa mapato, kwanza kisesa na usagara zingerudishwa tu jiji sababu tayari zimeshashikana na jiji la mwanza na halmashauri za magu na misungwi hazina uwezo wa kuhudumia hayo maeneo
 
Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
360
1,000
Habari Wanabodi.

Kuna kinachoendelea hapa Mwanza katika Mradi wa Ujenzi wa Stendi Mpya Kubwa na ya Kisasa Nyegezi Stendi hakika ni Makosa mengine Makubwa ya Kimpango Miji na Taaluma Yake..

Kama inavyo Fahamika kua Mwanza ni kati ya Majiji yanayokua kwa kasi sana Africa na hivyo Kuhitaji Mpango Miji Madhubuti ili kuondoa Misongamano Isiyokua ya Lazima ya Watu na Magari hapo baadae.

Awari ili kuanza kudhibiti Hali hii ya Msongamano kulikua na Mipango ya Kuzihamisha Stendi Kuu Mbili za Jijini Mwanza yaani Stendi ya Buzuruga na Stendi ya Nyegezi na kuzipeleka nje kidogo ya Jiji.

Ambapo stendi ya Buzuruga ingehamishiwa Kisesa ( Hii haina shida kwani mpango wake bado upo palepale)
Shida inakuja hapa kwenye hii Standi ya Nyegezi ambayo ndio stendi kubwa kabisa kwa hapa Mwanza kuendelea kulazimishwa kubaki hapa Nyegezi japo kiuharisia hii Sehemu imekua ndogo sana kuhudumu kama Stendi Kuu ya Mwanza.

Ili Kuipanua Stendi Hii Serikali itahitaji Bilioni nyingi za fedha kama Fidia kwa kulipia mejengo mbalimba ambayo yamejengwa kuizunguka Stendi.
Lakini pia hata Ikilazimishwa Kupanuliwa bado haitaweza kupata Eneo kubwa la Kukidhi Mahitaji yatakayotekea Miaka Miwili baadae.
Pia Hatua hii ya Kuipanua Stendi hii ya Nyengezi haitalisaidia Jiji la Mwanza kuanza kudhibiti Msongamano wa Magari na Watu mapema iwezekanavyo kabla Tatizo la Msongamano halijawa kubwa kama katika Majiji mengine Africa.

Stendi hii ya Nyegezi ilikua Ihamishiwe Usagara ambapo bado kuna Maeneo ya Mashamba ambapo Fidia yake ingekua ndogo sana kulinganisha na Mabilioni ya Kufidia Majengo Nyengezi.

Faida Nyingine ya kuhamishia Stendi Usagara ingekua ni Upatikanaji wa Eneo kubwa kabisa kwa Ujenzi wa Stendi Kubwa Kabisa na ya Kisasa ambayo Ingehudumu kwa Miongo kadhaa tofauti na Stendi kuwepo Nyegezi.

Pia kwa Jiografia ya Usagara ni Sehemu Muafaka kwa Stendi kubwa ya Mkoa kwani ipo njia Panda, Hapa kuna Njia Kuu Kuelekea Mkoa wa Geita, Shinyanga na hata Mkoa wa Mara via Usagara to Kisesa Road. Ni Njia Panda Muafaka kabisa kwa Abiria Kufanya Connection Kirahisi.

Faida nyingine Ilikua ni Kudhibiti Msongamano wa Mabasi na Maroli kwani Ujengwaji wa Standi Usagara ungesababisha Mabasi yote yasipite au kufika Katikati ya Jiji na hivyo kupunguza Msongamano wa Watu.

Lakini pia Ujenzi wa Stendi ungefanyika Usagara ungeongeza Kasi ya Upanuaji wa Jiji kua kubwa zaidi na Miradi mingi ingeanzishwa Usagara tofauti na Stendi kubaki Nyegezi ambapo kwa sasa ni Pafinyu kwa Maendeleo Mapya.

Sababu Kubwa inayosemekana na kusababisha Kung'ang'ania Stendi ya Nyengezi kulazimishwa kubaki hapo ilipo ni Hofu ya Halimashauri ya Nyamagana kupoteza Mapato kutokana kwamba Usagara ipo Wilaya Nyingine ya Halimashauri ya Misungwi.

Sababu Nyingine kuna Tetesi kua Matajiri walio wekeza Mahotel na Vituo vya Mafuta wamecheza Rafu ili kushinikiza Jiji, Stendi hii ya Nyegezi ibaki hapo ilipo japo ni wazi kua Eneo Hilo halina Sifa wala Uwezo wa kubeba Stendi kubwa na ya Kisasa kwa wakati huu.

Sababu Nyingine ni ya Kisiasa na Hofu alioyonayo Mbunge wa sasa wa Jimbo la Nyamagana kupoteza Kula kama hatofanya jitihada za kuzuia kuhamishwa kwa Stendi hii.

Hitimisho.

Naliomba Jiji na Utawala wa Mkoa wa Mwanza liangalie zaidi Faida na Hasara za Sasa na za Baadae za Kung'ang'aniza Stedi hii Nyengezi Kubaki Nyegezi Na Walinganishe na Faida zitakazopatikana Sasa na Baadae kwa Stedi Hiyo Kuhamishiwa Usagara kama ilivyo kwa Stendi ya Buzuruga Kuhamishiwa Kisesa.

Sababu za Kitaalamu na Gharama kwa Serikali zizingatiwe zaidi kuliko hizo sababu za Mapato ya Kiwilaya, Siasa na Watu Binafsi.

Atakae weza Aufikishe Uzi Huu kwa Serikali Kuu au hata Kwa Magufuli Ili Mwanza ipate Kupona Dhidi ya Msongamano Unaokuja Mbeleni.
 
Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Ila jambo ambalo haujui stendi ya buzuruga imehamishiwa Nyamhongoro na sio kisesa kwa sababu hizo hizo za mapato na mivutano ya kijinga ya wanasiasa na watendaji yasioangalia mbeli bali maslahi yao
 
christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,115
2,000
ndio swali hata mimi nilikuwa najiuliza hivi wataalamu wetu wanaangalia mbali kweli? Kwa ufupi stendi inajengewa pale pale nyegezi ndio maana nimeandika hili ili Mh Rais azishtue akili zao, hauwezi kuwa na fikra sahihi kwa kujenga stendi nyegezi
Aisee kwa jiji la Mwanza lilivyo hata mimi sishauri hiyo stendi ijengwe nyegezi kwani stendi itakuwa ndogo sana sababu eneo ni dogo, pili itasababisha msongamano wa magari usio na tija wa barabara inayoingia mjini.

Mimi sio mtaalam ila kwa akili yangu ya kawaida tu naliona hilo tatizo miaka michache ijayo.
 
christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,115
2,000
Ila jambo ambalo haujui stendi ya buzuruga imehamishiwa Nyamhongoro na sio kisesa kwa sababu hizo hizo za mapato na mivutano ya kijinga ya wanasiasa na watendaji yasioangalia mbeli bali maslahi yao
Siasa ndizo zinakwamisha maendeleo mimi ndio maana huwa namkubali sana Mh. JPM huwa hapendi cheap popularity kwenye mambo ya maendeleo.
 
Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Siasa ndizo zinakwamisha maendeleo mimi ndio maana huwa namkubali sana Mh. JPM huwa hapendi cheap popularity kwenye mambo ya maendeleo.
kabisa , ngoja tumuandikie labda ataone hili suala, it doesn't make any sense kujenga stendi nyamhongoro au nyegezi, nikupoteza tu hela
 
KITEKSORO

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
291
500
Habari Wanabodi.

Kuna kinachoendelea hapa Mwanza katika Mradi wa Ujenzi wa Stendi Mpya Kubwa na ya Kisasa Nyegezi Stendi hakika ni Makosa mengine Makubwa ya Kimpango Miji na Taaluma Yake..

Kama inavyo Fahamika kua Mwanza ni kati ya Majiji yanayokua kwa kasi sana Africa na hivyo Kuhitaji Mpango Miji Madhubuti ili kuondoa Misongamano Isiyokua ya Lazima ya Watu na Magari hapo baadae.

Awari ili kuanza kudhibiti Hali hii ya Msongamano kulikua na Mipango ya Kuzihamisha Stendi Kuu Mbili za Jijini Mwanza yaani Stendi ya Buzuruga na Stendi ya Nyegezi na kuzipeleka nje kidogo ya Jiji.

Ambapo stendi ya Buzuruga ingehamishiwa Kisesa ( Hii haina shida kwani mpango wake bado upo palepale)
Shida inakuja hapa kwenye hii Standi ya Nyegezi ambayo ndio stendi kubwa kabisa kwa hapa Mwanza kuendelea kulazimishwa kubaki hapa Nyegezi japo kiuharisia hii Sehemu imekua ndogo sana kuhudumu kama Stendi Kuu ya Mwanza.

Ili Kuipanua Stendi Hii Serikali itahitaji Bilioni nyingi za fedha kama Fidia kwa kulipia mejengo mbalimba ambayo yamejengwa kuizunguka Stendi.
Lakini pia hata Ikilazimishwa Kupanuliwa bado haitaweza kupata Eneo kubwa la Kukidhi Mahitaji yatakayotekea Miaka Miwili baadae.
Pia Hatua hii ya Kuipanua Stendi hii ya Nyengezi haitalisaidia Jiji la Mwanza kuanza kudhibiti Msongamano wa Magari na Watu mapema iwezekanavyo kabla Tatizo la Msongamano halijawa kubwa kama katika Majiji mengine Africa.

Stendi hii ya Nyegezi ilikua Ihamishiwe Usagara ambapo bado kuna Maeneo ya Mashamba ambapo Fidia yake ingekua ndogo sana kulinganisha na Mabilioni ya Kufidia Majengo Nyengezi.

Faida Nyingine ya kuhamishia Stendi Usagara ingekua ni Upatikanaji wa Eneo kubwa kabisa kwa Ujenzi wa Stendi Kubwa Kabisa na ya Kisasa ambayo Ingehudumu kwa Miongo kadhaa tofauti na Stendi kuwepo Nyegezi.

Pia kwa Jiografia ya Usagara ni Sehemu Muafaka kwa Stendi kubwa ya Mkoa kwani ipo njia Panda, Hapa kuna Njia Kuu Kuelekea Mkoa wa Geita, Shinyanga na hata Mkoa wa Mara via Usagara to Kisesa Road. Ni Njia Panda Muafaka kabisa kwa Abiria Kufanya Connection Kirahisi.

Faida nyingine Ilikua ni Kudhibiti Msongamano wa Mabasi na Maroli kwani Ujengwaji wa Standi Usagara ungesababisha Mabasi yote yasipite au kufika Katikati ya Jiji na hivyo kupunguza Msongamano wa Watu.

Lakini pia Ujenzi wa Stendi ungefanyika Usagara ungeongeza Kasi ya Upanuaji wa Jiji kua kubwa zaidi na Miradi mingi ingeanzishwa Usagara tofauti na Stendi kubaki Nyegezi ambapo kwa sasa ni Pafinyu kwa Maendeleo Mapya.

Sababu Kubwa inayosemekana na kusababisha Kung'ang'ania Stendi ya Nyengezi kulazimishwa kubaki hapo ilipo ni Hofu ya Halimashauri ya Nyamagana kupoteza Mapato kutokana kwamba Usagara ipo Wilaya Nyingine ya Halimashauri ya Misungwi.

Sababu Nyingine kuna Tetesi kua Matajiri walio wekeza Mahotel na Vituo vya Mafuta wamecheza Rafu ili kushinikiza Jiji, Stendi hii ya Nyegezi ibaki hapo ilipo japo ni wazi kua Eneo Hilo halina Sifa wala Uwezo wa kubeba Stendi kubwa na ya Kisasa kwa wakati huu.

Sababu Nyingine ni ya Kisiasa na Hofu alioyonayo Mbunge wa sasa wa Jimbo la Nyamagana kupoteza Kula kama hatofanya jitihada za kuzuia kuhamishwa kwa Stendi hii.

Hitimisho.

Naliomba Jiji na Utawala wa Mkoa wa Mwanza liangalie zaidi Faida na Hasara za Sasa na za Baadae za Kung'ang'aniza Stedi hii Nyengezi Kubaki Nyegezi Na Walinganishe na Faida zitakazopatikana Sasa na Baadae kwa Stedi Hiyo Kuhamishiwa Usagara kama ilivyo kwa Stendi ya Buzuruga Kuhamishiwa Kisesa.

Sababu za Kitaalamu na Gharama kwa Serikali zizingatiwe zaidi kuliko hizo sababu za Mapato ya Kiwilaya, Siasa na Watu Binafsi.

Atakae weza Aufikishe Uzi Huu kwa Serikali Kuu au hata Kwa Magufuli Ili Mwanza ipate Kupona Dhidi ya Msongamano Unaokuja Mbeleni.
Mawazo mazuri sana haya . Ndugu zetu wa mipango miji wangeyazingatia kwa kweli. Tatizo sasa utakuta kuna watu wachache ambao kwa namna fulani wanafaidika stendi ikijengwa Nyegezi, hivyo watatetea mpaka ijengwe hapo na hata rushwa zitatembea ili kukidhi haja. Suala hili lifikishwe tu ngazi za juu kwa mujibu wa taratibu. Naamini hata Mh. Rais Magufuli akiliona na hoja za msingi zilizotolewa atatoa maagizo ipasavyo. Sasa je litamfikia kwa wakati?
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,529
2,000
Unalionaje wazo lakini?
Nimecheka kidogo kuhusu wazo la Daladala katika mipango hiyo.

Kiujumla ni kama wataalam wetu wa mipango miji hawaishi dunia hii. Wangeishi dunia hii ingekuwa rahisi kwao kutazama miji mingine duniani wamefanya nini kuhusu hili. Kuna majiji makubwa kabisa duniani ambayo yalishashughulikia matatizo kama haya, wao Mwanza wanataka kuvumbua utaratibu wao mpya?

Au pengine nisiwalaumu 'wataalam' kwa maana ni siasa ndio iko mbele ya kila kitu katika mambo yetu.
 
Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
360
1,000
Mawazo mazuri sana haya . Ndugu zetu wa mipango miji wangeyazingatia kwa kweli. Tatizo sasa utakuta kuna watu wachache ambao kwa namna fulani wanafaidika stendi ikijengwa Nyegezi, hivyo watatetea mpaka ijengwe hapo na hata rushwa zitatembea ili kukidhi haja. Suala hili lifikishwe tu ngazi za juu kwa mujibu wa taratibu. Naamini hata Mh. Rais Magufuli akiliona na hoja za msingi zilizotolewa atatoa maagizo ipasavyo. Sasa je litamfikia kwa wakati?
Hivi ni Njia gani Muafaka ya Kuufikisha Ujumbe Huu kwa Serikali Kuu au kwa Raisi Mwenyewe. Nadhani tunawajibikwa kwa hili kama Wazalendo wa Kweli, nipeni njia nilifikishe hili.
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
2,328
2,000
Ila jambo ambalo haujui stendi ya buzuruga imehamishiwa Nyamhongoro na sio kisesa kwa sababu hizo hizo za mapato na mivutano ya kijinga ya wanasiasa na watendaji yasioangalia mbeli bali maslahi yao
Nyamhongolo ipo sehemu gani mkuu kwa hapo mwanza
 
Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,997
2,000
HIVI WAAFRICA TULILOGWA NANANI?
KWANINI TUNAFIKIRIA KUKUZA TU MIJI NA KUFIKIA HATA KUHARIBU MASHAMBA NA MALISHO YA MIFUGO YETU?
ETI STENDI KUBWA IJENGWE FELA ILI ......... NA ILI JIJI LIKUE ...... NONSENSE!
NB: KWA MIPANGO MIZURI YA MATUMIZI YA ARDHI NA UJENZI WA KISASA, JIJI LA MWANZA HALIPASWI KUWA KUUBWA MPAKA KUIMEZA NA FELA!
 
bababkk

Member
Aug 11, 2018
79
125
Mh. Rais, serikali yako imetenga mabillion ya pesa kwa ujenzi wa stendi za mabasi katika maeneo ya Nyamhongoro na Nyegezi jijini Mwanza, hili ni jambo zuri la kupongezwa katika juhudi za kuboresha miundombinu ya miji yetu,

Mh Rais najua unalifahamu vizuri jiji la mwanza ndio maana naandika haya kama mwanachi ninayeguswa na maendeleo ya Taifa letu.

Jiji la Mwanza kwa sasa limebanana sana maeneo yanayotaka kujengwa stendi hayafai kabisa kwa sasa na hata kwa baadae, tuomba uingilie kati hili suala otherwise tutafanya mambo kama watu tusiokuwa na maono wala fikra za baadae ili tu kufanikisha malengo ya wanasiasa fulani.

USHAURI : Mh Rais sehemu nzuri na ambayo ipo strategic kwa stendi ya nyamhongoro ni kisesa na kwa Nyegezi ni Nyashishi, suala la mivutano ya mapato kati ya halmashauri na mambo ya kitoto na yasiyoangalia maslahi mapana ya ujenzi wa taifa letu.

Kama itakupendeza Mh Rais ni bora kuirudisha Kisesa na Usagara ndani ya jiji ili kuondoa hii mivutano ambayo naona haina tija kabisa.

Stendi ikijengwa kisesa itasaidia magari yanayoenda Dar na mikoa mingine yanayotokea musoma kutoingia jijini bali kupitia njia mpya ya kisesa -usagara iliyojengwa na serikali yako

Pia Mh Rais unaweza amua kuunganisha pesa za hii miradi miwili ukajenga stendi moja kubwa na ya kisasa maeneo ya FELA itakayohudumia mabasi ya yote ya mikoani na daladala zitafanya kazi za kusomba watu, kwanza itachochea uwekezaji katika hayo maeneo na kukuza miji yetu.

Hata station kubwa ya abiria wa standard gauge ningeshauri ijengwe FELA kuliko kuipeleka katikati ya jiji

Ikikupendeza Mh Rais naomba ulifikilie wazo langu kwa kina, ujenzi wa hizi stendi kwa miaka michache ijayo hazitakuwa na tija tena na itabidi kuhamisha tena.
Hivi jiji la mwanza halina wataalamu wa mipango miji?
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
12,978
2,000
Hata station kubwa ya abiria wa standard gauge ningeshauri ijengwe FELA kuliko kuipeleka katikati ya jiji
Hili wazo la kujenga stand kubwa eneo la FELA ni wazo zuri sana, kwanza kuna station ya treni hapo hivyo abiria wa treni hatalazimika kufika mjini, atateremkia fela na kukamata usafiri wa bukoba geita musoma, stand za nyegezi na nyamhongolo zibaki kwa ajili ya daladala za mjini, lakini stand kuu ijengwe FELA kwa kweli,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom