Mh Rais Hakuvunja KATIBA yupo sahihi kwa katiba ya nchi yetu

Naronyo

hapa hakuna mambo ya tafsiri,kwani issue ipo wazi sana

kiapo kitamfanya waziri ama mbunge kufanya kazi husika,lakini kutokula kiapo hakimfanyi waziri ama mbunge asiwe mbunge

ataitwa mbunge ama waziri baada tu ya kutangazwa na mamlaka tajwa ktk katiba

Mkuu mbona Rais anatajwa na Tume lakini anakuwa Rais mteule hadi aape? Na kumbuka Rais akishatajwa na Tume hakuna wa kwenda kupinga hilo popote pale lakini hawezi kushika madaraka ya Urais hadi aape!
 
Naronyo

hapa hakuna mambo ya tafsiri,kwani issue ipo wazi sana

kiapo kitamfanya waziri ama mbunge kufanya kazi husika,lakini kutokula kiapo hakimfanyi waziri ama mbunge asiwe mbunge

ataitwa mbunge ama waziri baada tu ya kutangazwa na mamlaka tajwa ktk katiba

Mkuu mbona Rais anatajwa na Tume lakini anakuwa Rais mteule hadi aape? Na kumbuka Rais akishatajwa na Tume hakuna wa kwenda kupinga hilo popote pale lakini hawezi kushika madaraka ya Urais hadi aape!
 
engmtolera naona Jaji Werema amekuunga mkono. Kwenye taarifa ya habari ya TBC1 amesema kwamba Rais hajavunja katiba. Ila hakuingia kwenye vifungu vya kuapa. Anasema unakuwa mbunge baada ya Tume kukutambua (wale wa kuchaguliwa ama maalumu), baada ya kupitishwa na baraza la wawakilishi (wale wa kutoka baraza la wawakilishi) na baada ya kuteuliwa na Rais (wale wa kuteuliwa).

KIMBUNGA

Inabidi sasa tujiandae kutoa maoni yetu ktk mchakato wa katiba hii ijayo,ili tuweze kupata katiba itakayo jibu hoja na matakwa yetu

kwa mfano ni kwanini hatutakiwi kupeleka mahakamani jambo lolote lile lililotokana na ushauri mbaya ama mzuri uliotolewa na mawaziri kwa raisi,hii inaweza kuleta madhara makubwa sana,kama mawaziri watamshauri vibaya raisi na ushauri huo ukaleta MAAFA kwa wananchi husika
 
Kama kweli kesho wataapishwa kuwa mawaziri, itabidi tuandae maandamano ya peoples power kuwatoa ofisini. Je kulikuwa na ulazima gani wa kumteua Mbatia muda mrefu kabla ya bunge wakati hajapew hata uwaziri?

hivi haiwezekani kufungua kesi kesho asubuhi kabla hawaja apishwa au raisi yuko juu ya sheria
 
crashwise

ktk tanzania yetu hakuna hilo jina,tunaita kwa mazoea tuliyonayo,lakini hakuna kitu kama hicho hata ktk katiba huwezi kuta neno mbunge mteule ama rais mteule hiyo haipo

naomba uelewe kuwa mbunge ama rais akisha tangazwa na mamlaka husika iliyowekwa kisheria basi huyo atakuwa ni mbunge na rais isipo kuwa hawezi kufanya kazi za uraisi ama ubunge hadi ale kiapo husika

na asipokula kiapo ataendelea kuwa mbunge/raisi
 
Mkuu mbona Rais anatajwa na Tume lakini anakuwa Rais mteule hadi aape? Na kumbuka Rais akishatajwa na Tume hakuna wa kwenda kupinga hilo popote pale lakini hawezi kushika madaraka ya Urais hadi aape!

tena umejijibu wewe mwenyewe,kuwa akisha tangazwa tu huna ruhusa ya kupinga matokeo hayo,ikimaanisha kuwa aliyetangazwa ni ndiye rais aliyetokana na matakwa ya wengi na hata baada ya kutangazwa ulinzi unaanza hapo hapo,kula kiapo ni kumpa rungu sasa la kufanya kazi na kuto kuapa hakumwondolei mhusika kuitwa RAIS na si kama msemavyo RAISI MTEULE (BIG NO) ni wapi ktk katiba kuna neno RAISI MTEULE?
 
Kuna mawili. Kama rais hakuvunja Katiba Spika wa bunge alivunja kwa kukataa swali la mtu aliyetangazwa mbunge ambalo lilitumwa in advance kabla hajaapishwa.
 
Ni kweli kabisa Mh rais kakosea na akubali marekebisho.Si unajua hata Rais akichaguliwa kama kuna Rais mwingine ni mpaka kwanza aapishwe ndio atapishwa na yule mtangulizi wake kushika madaraka ya Uraisi,otherwise kabla ya kuapishwa sio Rais ila aliyemtangulia ndiye Rais hadi aapishwe.
Nawasilisha.
 
Katiba imevunjwa na jambo hili liko wazi hata kwa ambaye hajasoma sheria akisoma hapa anajua kuwa katiba imevunjwa. Ila kwa vile mnataka kulazimisha mambo hii itakula kwenu

Mbunge kabla ya kuapishwa na spika yeye ni mbunge mteule anakuwa mbunge pale ameapishwa kiapo cha uaminifu. Ebu tuangalie: Baada ya uchaguzi hatujawahi kuona rais amekurupuka kuchagua PM, na baraza lake la mawaziri kabla ya speaker wa bunge kuwaapisha wabunge wote. Ni mara ya kuapishwa ndio mchakato wa rais kuunda baraza lake unaanza

Hivo hapo hakuna ujanja rais amekosea ni vyema tu asiapishe hao mawaziri ni busara tu za kawaida, hata yeye anaweza kupitiwa ni mwanadamu akubali yaishe asisababishe mguu kuota tende

Mbunge kabla ya kapishwa ni Mbunge halali aliye chaguliwa au kuteuliwa kihalali,ila tu ili ashiriki shughuli za kibunge atatakiwa ale KIAPO CHA UAMINIFU.

Kwani wapi katika katiba imetamka Mbunge mteule? Hii ni lugha tuliyoizoea kuisema lakini haikutamkwa kwenye katiba na hakuna mtu anayeitwa mbunge mteule katika katiba tunayoitumia sasa, kuna Mbunge.
Kuhusu kumchagua PM ni zoezi ambalo lazima lihusishe shughuli za kibunge ikimaanisha lazima wabunge wapige kura ya kumkubali au kumkataa aliyeteuliwa kuwa PM. ndio maana lazima asubiri wabunge waapishwe ndio zoezi liendelee na si vinginevyo.

Na ndio Maana Mhe Raisi kwanza amewatuewa kuwa wabunge, na baadae akafuata kuwateuwa kuwa Mawaziri, na hakuanza kuwateuwa kuwa Mawaziri then afuate kuwateuwa kuwa Wabunge.

 
Kuna mawili. Kama rais hakuvunja Katiba Spika wa bunge alivunja kwa kukataa swali la mtu aliyetangazwa mbunge ambalo lilitumwa in advance kabla hajaapishwa.

nadhani elimu bado inahitajika hapa

ile siku mbunge husika hakuelezwa kuwa yeye si mbunge hapana,yeye ni mbunge na ndio maana ulimwona bungeni lakini hakuwa na uhalali wa kufanya kazi za kibunge kwanini? kwa kuwa labda (1)hakula kiapo na (2) hakufuata taratibu nyingine za upelekaji wa maswali kama mbunge mpya

kama kuapa ndio kuwa mbunge basi hata bungeni wasingekuwa wanaruhusiwa kuingia kuchagua spika,ilitakiwa waape kwanza ndio waingie bungeni kama tunataka kiapo ndio kiwe kina mpa mtu ubunge
 
ni hivi hao ni mawaziri lakini hawataruhusiwa kujibu chochote au kuwakilisha popote pale mpaka Semamba na Dodoma wawatambue!! Hiyo ndio tafsiri halisi ya hivo vifungu hapo!!

Ukipindisha ukweli huo hakuna wa kukuhukumu kwani ni kawaida kwa viongozi na wananchi hapa nchini!! Unasemaje kuhusu hao watu 'mawaziri' kukutana na kamati za bunge hivi karibuni kabla ya kikao cha bajeti?? Hapo katiba inawaruhusu??
 
Kuna watu kwa makusudi hupenda ubishi usiishe kwa sababu tu ya kupachika neno "tafsiri" hata kwa terms zilizo obvious.

Msipojikita kwenye Sheria za viapo (Oaths) na Sheria za Kutafsiri Sheria (interpretations) basi mtakaa mbishane kila kukicha.
 
ni hivi hao ni mawaziri lakini hawataruhusiwa kujibu chochote au kuwakilisha popote pale mpaka Semamba na Dodoma wawatambue!! Hiyo ndio tafsiri halisi ya hivo vifungu hapo!!

Ukipindisha ukweli huo hakuna wa kukuhukumu kwani ni kawaida kwa viongozi na wananchi hapa nchini!! Unasemaje kuhusu hao watu 'mawaziri' kukutana na kamati za bunge hivi karibuni kabla ya kikao cha bajeti?? Hapo katiba inawaruhusu??

kesho wana kula kiapo na watakutana na wabunge wenzao bila shaka wakiwa ktk magwanda ya uwaziri rasmi
 
kesho wana kula kiapo na watakutana na wabunge wenzao bila shaka wakiwa ktk magwanda ya uwaziri rasmi

Mkuu Injinia M...
Mimi nimesema hao watu 'mawaziri' wanaruhusiwa kufanya shughuli zao za uwaziri ila hawaaruhusiwi kujibu chochote ama kuwakilisha popote pale mpaka wale kiapo bungeni hayo mengine ni yako!!

Wacha katiba ivunjwe, ni kawaida!!
 
Kingine Raisi alicho kosea kabisa niku mteua Husseni mwinyi kua waziri wa Afya,akati kikatiba wizara ya Afya haipo kwenye Muungano na Husseni Mwinyi sio mbunge wa bara.Husseni mwinyi alikua waziri wa Ulinzi sababu wizara iyo ipo kwenye mkataba wa Muungano.Raisi wetu kama yeye hafaamu je ata wanae mzunguka hawafaamu?je mwana sheria Mkuu wa Serekali ana fanya kazi gani?ukweli Raisi wetu ana mizigo na yeye mwenyewe nimzigo aachie ngazi.
 
Jamani labda sijafuatilia vizuri mada hii. Hivi hawa wabunge walioteuliwa na rais (nominated MPs) na kuwa mawaziri watafanyaje ile michakato ya kuandaa budget na mielekeo yake katika kamati za Bunge ambazo zitaanza kukutana hivi punde? Chukulia wizara ya fedha kwa mfano -- wote watatu -- yaani Waziri (na manaibu wake wawili) ni nominated MPs na wizara hiyo ndiyo wizara mama katika masuala ya kuandaa budget.

Watajibizana vipi na wajumbe wa kamati au hizo hazichukuliwi kama ni shughuli za Bunge? AG Werema afafanue hapo!
 
56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.


68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.


Duh.. Hapo kwenye red.. Hicho kiapo kingine kinachozungumziwa hapo na kitakachohucika na utendaji wake kazini ni kipi..?
 
Hebu tuijadili na hii Ibara ya 56.isemayo:Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo KINGINE chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

My take: hapa kiapo kingine ndio hicho sasa ambacho ni cha Nafasi ya Ubunge ever since Ibara ya 68 imewajumuisha na kuwatambua wote kuwa ni wabunge ingawa watahitaji kiopo cha utii ili waweze kusit for vikao vya bunge vya ndani"
 
Back
Top Bottom