engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
baada kujiridhisha mwenyewe kwa kusoma katiba ya jamuhuri wa muungano wa tanzania,nimeona kuwa Mh Rais hakuvunja katiba ya nchi yetu kama baadhi ya watu wanavyo dai
mnaweza pia kujionea wenyewe hapa chini,kwani nimeweka vifungu vinavyomruhusu raisi kumteua waziri pasi ya kuvunja katiba ya nchi
katiba inasema:-
54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais waZanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa
mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.
55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada
ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.
56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.
KWA MANENO MENGINE mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa na bado hawa pata kiapo cha uaminifu bungeni,hatafanya kazi za kibunge ama kujibu hoja za wabunge bungeni mpaka pale atakapo pata kiapo cha uaminifu ndani ya bunge.
lakini ataendelea kufanya kazi za serikali kama waziri baada ya kuapishwa na Mh raisi kama inavyojielekeza hapo juu
nawasilisha(tusome na tuelewe tusikurupuke)