Mh.Pinda abaki mpweke !

Mh.Pinda abaki mpweke !

Kwa ujumla serikali ya awamu ya nne iliendekeza suala la udini sana.
Hata ajira za watu mhimu mf Mnikulu, Mawaziri, Usalama, RPCs, na washauri mhimu wa serikali ili lazimu kuwa Waislam. Bila siri hawa jamaa wengi hawajasoma!!

TCRA mnisamehe leo, naomba muanze tarehe 1 July, 2015. Ila ukweli kwa gharama yoyote ni lazima usemwe na ujulikane.
 
Naanza kuona kwanini Pinda hata jimboni kwake hawamkubali
 
Wakati mwingine ni vema kusemaukweli kama jambo haliwezekani kuliko kuwahadaa wananchi na kusababisha mipasuko isiyo na maana. mbona kwenye kupandisha mishahara kwa walimu huwa wanakuja macho meupe nakusema hatuongezi sasa hili wanaogopa nini kuwaita wazee wa muji na kutoa tamko, wanalo mwaka huu.
 
Hahahaha...eti pinda nae aliutaka urais..duh???
 
Hii ni rahisi sana kutatua kuliko lolote

Ningesimamia msimamo wa katiba

serikali haina Dini na kila dini ishughulikie mambo yake ya ibada kwa mujibu wa taratibu za kanisa au msikiti.

Ni rahisi kiasi hicho. Pinda, kikwete na ccm yao inawawia vigum kwasababu wanafanya nje ya jatiba na hivyo kuonekana wanavuruga Taifa kwa kuvunja katiba hadharani.
Walijifanya kutoa ahadi kwamba wataianzisha wakadhani Tz ya leo ni ile ya nyuma sasa linawatokea puani, walizoea tutajenga madaraja, tutajenga lami alafu wasipojenga kinachofuata ni kuwaambia wananchi maneno ya kupendeza kwamba "upembuzi yakinifu umefanyika na mpaka sasa wataalamu wanahangaika kuangalia namna ya kuboresha ili barabara ijengwe pana zaidi hivyo tutatekeleza katika awamu ijayo"-wanapigiwa makofi, lakini hili la kazi issue imekuwa nzito namna ya kuliundia maneno imekuwa ngumu kidogo
 
Tatizo la baadhi ya watanzania hupima urais kwa kigezo kimoja tena kigezo dhaifu kama mahakama ya kadhi. Hata waisilam sio wote wanashadadia mahakama ya Kadhi sembuse wakristo au hata wapagani? Suala sio kusema Pinda anaipenda hoja ya Mahakama ya Kadhi hoja ni namna gani ameishughulikia? Hata kama haijakubalika yeye binafsi kama kiongozi amelishughulikiaje.Hawezi kuacha kulishughulikia kwa sababu tu yeye sio Mwisilamu, la hasha! Yeye siyo kiongozi wa kidini ni kiongozi wa kisiasa. Kiongozi hufanyi jambo lile unalolipenda tu hata usilolipenda lakini kuna wananchi ambao wewe ni kiongozi wao wana jambo wanalolipenda wewe unawasaidiaje kufikia malengo yao. Uraisi ni mambo mengi yanayoshikana kwa pamoja (complex) Kumkataa mtu kwa sababu ya jambo moja tu Mahakama ya Kadhi na huwezi kumkubali mtu kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi tu, tumwangalie mtu in his totallity. Kama vile watu kumjudge mtu kwa jinsi anavyotoa rushwa kwenye vikundi vya dini au kijamii. Hapana uraisi ni mchanganyiko wa sifa nyingi zikijumuishwa kwa pamoja.
Kiongozi yeyote asiyeweza kuilinda, kuisimamia na kuitetea katiba yetu, huyo hatufai. Pinda hafai hata kuwa mwenyekiti a kijii kwa sababu haheshimu haki za binadamu, hajali katiba ya nchi, wala nia ya kujenga taifa imara lenye mshikamano na amani hana.

Amejidhihirisha ni namna gnai anaweza ktumiwa na itikadi yoyote kusaliti nchi na watu wake halafu asijitambue kwamba ana haribu.

Aliamuru majeshi yapige raia wasio na silaha wakitafuta haki zao kikatiba kwa mba amechoka. Leo nguvu ya kuliingiza taifa kwenye mapigano ya kidini amezitoa wapi?

Alisema eti Waziri asipokuwa mbunge hataweza kuwatumikia vizuri wananchi kwa sababu hatajua hali na mahitaji yyao sahihi ikatoa namna gnai kichwa chake kilishaacha kufikri na bila shaka anapoteza kumbukumbu zake haraka.

Amekusanya kusanya viongozi kadhaa wa dini kulazimisha maridhiano ya kadhi, pamoja na kukataa kwao akaibuka na taariga kwamba wameafiki. Hii ni tabia ya udanganyifu na ulaghai inayoangamiza taifa kwa kufanya maamuzi yasiyo sahihi yanayojengwa kwenye taarifa za kupikwa.

Ameendelea kuishauri serikali itumie ubabe katika masuala yote yenye utata kuazia kura za mitaa, BMk, unandikshwaji wa wapiga kura, kura za maoni na miswada mbali mbali inayoelekea kutusababishia shida hata kabla ya uchaguzi mkuu.

Huyu anatahili kupumzika kwa sababu amechoka. Bila hivyo, tutegemee majanga makubwa kama hli la kadhi kwenye katiba, unless watu watumienguvu kubwa kudhibiti nyendo zake.

LAKINI URAISI ASAHAU, INGAWA ANATAKIWA KUAGALIWA KWA UKARIBU SANA KWA KIPINDI HIKI CHA LALA SALAMA KWA SABBU NINAONA WAMEJIZATITI KUMALIZIA HUJUMA WALIZOZIANZA KWA TAIFA YEYE NA MKUU WAKE.

SAFARI ZA ARABUNI NINAOMBA NGUVU YA MUNGU IMFUNGIE KUANZIA SASA HADI ATAKAPOACHA UONGOZI.
 
Pinda kwenye urais asahau,na kikwete anamtumia kwenye gvt yake kama ngao, kakini pinda yuko hoi bora ya lowassa yuko,kimya,kimya lakini kikwete ni msanii sana.
 
huyu mzee akigombea urais akiulizwa swali na waislam mahakama ya kadhi iko wapi ataanza kudosha chozi tu
 
Hakuna waziri mkuu atayekuja kuwa rais wa Tanzania.

"Waziri mkuu wa kwanza tanganyika ni Mwl. Julius Nyerere baadae akawa Rais."....somo la siasa primary enzi hizo.

Pinda hafai kwa lolote....
 
Kusema ni rahisi. Shughuli ni kutenda.

Ungekuwa kwenye kiti cha waziri mkuu na changamoto (controversial issuues) kama haya yanatokea sijui ungefanya nini zaid ya anachokifanya Pinda muda huu.

Uongozi si lelemama kama udhaniavyo..
kensh , @vuta nkuvute , stabilaza na wengineo

Uongozi sio lelema iwapo ukiwa kiongozi utaweka mbele fitna, unafiki, uongo na ulevi wa madaraka.
 
Last edited by a moderator:
Mie tangia mwanzo nimewahi kusema kuwa Pinda hana sifa za kuwa Rais wa nchi yetu Tanzania, hata uwaziri mkuu aliipata bila ya washauri wa Rais kufanya vetting kwa umakini.

Ukiangalia utendaji wake amechangia sana hata hali ya maisha kwa wananchi kuwa ngumu kiuchumi, sasa huyu akiwa Rais nchi itakaaje hapa?
 
Kama kuna watu wanadhani wataendelea kutawala kwa propaganmda na mabavu katika dunia ya leo pamoja hila wameoza kifikra. Watanzania wnahitaji ukweli, haki na kuacha unafiki, najua wengi hamtakubaliana nami lakini ukweli ni kuwa watanzania wanasubiri Oktoba ili kuamua.
 
Bantulile, tunaungana kuwafanyia thathmini pana viongozi wetu katika wingi na ukubwa wa mazuri na mabaya yao.

Kiongozi mtumia rushwa na fisadi, ameshajiengua wala hana nafasi ya kupimwa tena kwa uhudhriaji wake misibani, kutoa michango kwa makundi au propaganda. Kosa la ufisadi na rushwa linafunika wema na uzuri wowote wa kiongozi.

Kiongozi anayesaliti katiba, anasaliti uma. Hata angejaribu kujitabasamisha namna gani huyo hafai kuongoza umma kwa sababu hatasimamia maslahi ya umma.

Ninakubaliana na wewe kabisa kwamba kiongozi ni mdau wa masuala yote yanahusu jamii anayoiongoza na anapaswa kuyashughulikia. Tatizo linakuja namna gani anashughulikia? Kujaribu kuvuruga amani ya nchi kinyume na misingi ya katiba na utaifa eti unashughulikia tatizo la kundi moja? Unashughulikia tatizo la kundi moja kwa gharama ya uhai wa taifa? Hapo ndipo sifa ya Pinda ilipoondoka na mahakama yake ya kadhi.

Hivi leo wafanyabiashara wanagoma kulipa kodi, halafu kiongozi anaanza kushirikiana nao kuboresha mgomo ili kodi walipe wafanyakazi peke yao. Ni sahihi? Kwamba kwa kuwa hawataki basi atafute lugha ya kuwashawishi wafanyakazi wakubali klipa kodi peke yao kuwaridhisha wafanya biashara waiogoma? Hapana ndugu. Huo si uongozi.

Migogor yote inatatuliwa kwa kurejea kwenye constitution. Hivi kulikuwa na haja gani Pinga kulazimisha hasi muswada wa kuvuanja sheria za nchi na kuvuruga amani? Hajui kama katiba inasemaje? Huyu Pinda na wenziye wa ccm (wanafiki wachache), wangekuwa wakweli, na wana uchungu na taifa, walishindwa nini kuwapa elimu ya uraia na katiba hao waliotka dini yao iwe ya seriakli? Kilichowafanya hadi waingize kwenye ilani ni nini kama si unafiki, na woga wa kuitetea katiba ya Jamhuri?

Hapo ndipo Pinda na ccm fisadi, wamethibitisha hawawezi ama kwa hiyari ama kwa mfumo wa chama chao, ama kwa kundi dogo lenye nia ovu na taifa, kuitetea na kuisimamia katiba na hivyo hatuhitaji tena kuwapima kwa vitu vingine ingawa hata hivo yak mengi sana waliyopwaya.

Kwa ufupi, Mahakama ya kaedhi alivyoishughulikiapinda, hafai kuwa kiongozi wa umma.

Lowasa kwa wizi, rushwa , ufisadi na uwongo uwongo wake wa kuhadaa, hafai kuwa kiongozi wa umma na hatuna sababu ya kuwaupima kwa namna nyingine kwa sababu makosa yana constitute major constitutional offences na actually wanastahili kushitakiwa.

Hatuhitaji watu wenye usafi wa kutafutiza kwenye nafasi zoe za uongozi.

Hope umenielewa kiongozi.

Tatizo la baadhi ya watanzania hupima urais kwa kigezo kimoja tena kigezo dhaifu kama mahakama ya kadhi. Hata waisilam sio wote wanashadadia mahakama ya Kadhi sembuse wakristo au hata wapagani? Suala sio kusema Pinda anaipenda hoja ya Mahakama ya Kadhi hoja ni namna gani ameishughulikia? Hata kama haijakubalika yeye binafsi kama kiongozi amelishughulikiaje.Hawezi kuacha kulishughulikia kwa sababu tu yeye sio Mwisilamu, la hasha! Yeye siyo kiongozi wa kidini ni kiongozi wa kisiasa. Kiongozi hufanyi jambo lile unalolipenda tu hata usilolipenda lakini kuna wananchi ambao wewe ni kiongozi wao wana jambo wanalolipenda wewe unawasaidiaje kufikia malengo yao. Uraisi ni mambo mengi yanayoshikana kwa pamoja (complex) Kumkataa mtu kwa sababu ya jambo moja tu Mahakama ya Kadhi na huwezi kumkubali mtu kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi tu, tumwangalie mtu in his totallity. Kama vile watu kumjudge mtu kwa jinsi anavyotoa rushwa kwenye vikundi vya dini au kijamii. Hapana uraisi ni mchanganyiko wa sifa nyingi zikijumuishwa kwa pamoja.
 
Mheshimiwa Tabby umechangia vizuri. Awali nilisema tuangalia kwa namna alivyolishughulia swala la mahakama ya Kadhi. Kwa CCM kuliweka swala hilindani aya kilani yao ya uchaguzi lilikuwa kosa. Maana tayari iliishaingiza maswala ya dini ndani ya serikali ambayo wangeuunda. Kwa muji wa katiba ya CCM Kiongozi ni yule anayeielewa siasa ya Chama, anayeweza kuieleza na kuitetea. Katiba ziko mbili hapa Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya CCM.Panapokuwa na Katiba mbili tunaangalia katiba kubwa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini viongozi wetu wote, iwe ni Rais Waziri, Mbunge na hata baadhi ya watumishi wanaangalia maslahi ya kichama kwanza kuliko ya Kitaifa. Hii ni kwa sababu moja kubwa ili uhudumia maswala yote ya kitaifa sharti ukubalikena chama kwanza. Kinachomfikisha Peter Kayanza Pinda kwenye Uwaziri Mkuu ni chama anayemteua Peter Kayanza Pinda ni Rais na Mwenyekiti wa CCM.Anapotekeleza majukumu yake Pinda ni lazima angalie kwa macho ya makengeza wale wote wanaomfikisha hapo. Mara nyingi matendo yake yaweza kuwa taswira ya anayemteua. Amlipaye mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo.
Pinda ameonyesha udhaifu mkubwa katika maswala ya Delegation. Katika swala la kutumia wataalam Pinda amenichefua sana. Mosi swala na usimamizi wa uzito mizigo barabarani, wataalam wakataka kusimamia uzio unaorusiwa kisheria na magari ya mizigo. Wenye magari wakagoma, Pinda akaenda kuzungumza nao, akawaruhusu wafanaya biashara wafanye wanavyotaka. Leo tena serikali kupitia TRA (Wataalam) inataka wafanya biashara walipe kodi kwa kutumia kiafaa maalum cha kisasa cha kukusanyia kodi, wafanya bashara wanagoma, Pinda tena anaingilia utaalam wa kodi anaenda kuzungumza na wafanya biashara. Pinda si mtaalam wa kodi wala wa barabara. Kuwa Waziri Mkuu sio kuwa mtaalam wa kila fani bali ni kuwatumia vizuri wataalam wa fani husika waliopo. Siyo kila mpango mkakati unaopangwa na wataalam wa fani husika wewe Waziri Mkuu unaenda kupangua. Utafanya wewe katiaka taaluma zote. Kodi ni fani barabara ni fani sio siasa.
Bantulile, tunaungana kuwafanyia thathmini pana viongozi wetu katika wingi na ukubwa wa mazuri na mabaya yao.

Kiongozi mtumia rushwa na fisadi, ameshajiengua wala hana nafasi ya kupimwa tena kwa uhudhriaji wake misibani, kutoa michango kwa makundi au propaganda. Kosa la ufisadi na rushwa linafunika wema na uzuri wowote wa kiongozi.

Kiongozi anayesaliti katiba, anasaliti uma. Hata angejaribu kujitabasamisha namna gani huyo hafai kuongoza umma kwa sababu hatasimamia maslahi ya umma.

Ninakubaliana na wewe kabisa kwamba kiongozi ni mdau wa masuala yote yanahusu jamii anayoiongoza na anapaswa kuyashughulikia. Tatizo linakuja namna gani anashughulikia? Kujaribu kuvuruga amani ya nchi kinyume na misingi ya katiba na utaifa eti unashughulikia tatizo la kundi moja? Unashughulikia tatizo la kundi moja kwa gharama ya uhai wa taifa? Hapo ndipo sifa ya Pinda ilipoondoka na mahakama yake ya kadhi.

Hivi leo wafanyabiashara wanagoma kulipa kodi, halafu kiongozi anaanza kushirikiana nao kuboresha mgomo ili kodi walipe wafanyakazi peke yao. Ni sahihi? Kwamba kwa kuwa hawataki basi atafute lugha ya kuwashawishi wafanyakazi wakubali klipa kodi peke yao kuwaridhisha wafanya biashara waiogoma? Hapana ndugu. Huo si uongozi.

Migogor yote inatatuliwa kwa kurejea kwenye constitution. Hivi kulikuwa na haja gani Pinga kulazimisha hasi muswada wa kuvuanja sheria za nchi na kuvuruga amani? Hajui kama katiba inasemaje? Huyu Pinda na wenziye wa ccm (wanafiki wachache), wangekuwa wakweli, na wana uchungu na taifa, walishindwa nini kuwapa elimu ya uraia na katiba hao waliotka dini yao iwe ya seriakli? Kilichowafanya hadi waingize kwenye ilani ni nini kama si unafiki, na woga wa kuitetea katiba ya Jamhuri?

Hapo ndipo Pinda na ccm fisadi, wamethibitisha hawawezi ama kwa hiyari ama kwa mfumo wa chama chao, ama kwa kundi dogo lenye nia ovu na taifa, kuitetea na kuisimamia katiba na hivyo hatuhitaji tena kuwapima kwa vitu vingine ingawa hata hivo yak mengi sana waliyopwaya.

Kwa ufupi, Mahakama ya kaedhi alivyoishughulikiapinda, hafai kuwa kiongozi wa umma.

Lowasa kwa wizi, rushwa , ufisadi na uwongo uwongo wake wa kuhadaa, hafai kuwa kiongozi wa umma na hatuna sababu ya kuwaupima kwa namna nyingine kwa sababu makosa yana constitute major constitutional offences na actually wanastahili kushitakiwa.

Hatuhitaji watu wenye usafi wa kutafutiza kwenye nafasi zoe za uongozi.

Hope umenielewa kiongozi.
 
Pinda alifaa kuwa waziri mkuu wa mashambani au wakulima wa nyanya chungu

Umenichekesha sana hadi mbavu zinauma. Wakulima wa nyanya chungu(ngogwe kama wanavyoita kaskazini) wangemnyoosha na asingekuwa amepinda tena.
 
Kwa ujumla serikali ya awamu ya nne iliendekeza suala la udini sana.
Hata ajira za watu mhimu mf Mnikulu, Mawaziri, Usalama, RPCs, na washauri mhimu wa serikali ili lazimu kuwa Waislam. Bila siri hawa jamaa wengi hawajasoma!!

TCRA mnisamehe leo, naomba muanze tarehe 1 July, 2015. Ila ukweli kwa gharama yoyote ni lazima usemwe na ujulikane.

Unaposema waislam hawajasoma uweke na takwimu,
tuwekee idadi yao kiujumla,idad ya waliosoma na wasiosoma.
Na pia tupatie idadi ya wasio waislam kwa ujumla,na idad ya waliosoma na wasiosoma.Then tufanye analysis

Kusifia kama wakristo wamesoma,then kwenye kashfa za wizo serikalin wao ndo wengi ni ujuha.Haya Mtoto wa Mkulima kasoma mbona anavurunda?AG wa Mkapa,ma-AG QA JK WOTE WAKRISTO NA HAPA WANACHAMBWA KUWA NI EMPTY HEADS,ILA WAO HAMUWASEMI KWA DINI ZAO,AKINA S@ad@ mnawajadili kwa dini zao.Hapo hakuna u-great thinker mdau
 
Hakuna PM boya kama pinda dunia hii
Kama kufungwa na nifungwe tu nimechoka sasa
 
Unaposema waislam hawajasoma uweke na takwimu,
tuwekee idadi yao kiujumla,idad ya waliosoma na wasiosoma.
Na pia tupatie idadi ya wasio waislam kwa ujumla,na idad ya waliosoma na wasiosoma.Then tufanye analysis

Kusifia kama wakristo wamesoma,then kwenye kashfa za wizo serikalin wao ndo wengi ni ujuha.Haya Mtoto wa Mkulima kasoma mbona anavurunda?AG wa Mkapa,ma-AG QA JK WOTE WAKRISTO NA HAPA WANACHAMBWA KUWA NI EMPTY HEADS,ILA WAO HAMUWASEMI KWA DINI ZAO,AKINA S@ad@ mnawajadili kwa dini zao.Hapo hakuna u-great thinker mdau

Pole. Tulia dawa iingie vzr. Hapa sio udini ila ni Fact tu.
Mf Chuo chochote ulichosoma kuna Ma Prof. wangapi wa Kiislam? pia mf mzr ni Bunge kuna Ma Prof. na Ma Dr. wangapi wa Kiislam?
 
Hoja ya mahakama ya kadhi tumeiona jinsi ilivyoibua hisia kali na hali ya sintofahamu ktk jamii.Ilipelekea Mh.Mtikila kuwahi mahakamani kuipinga isizungumzwe bungeni.

Maaskofu na watu wasio na maslahi na mahakama ya kadhi,waliipinga kwa hoja na hata kuionya serikali isithubutu kuinzisha mahakama hiyo.

Waziri mkuu na mwanasheria mkuu waliikomalia na kushawishi sana kuwa haina madhara endapo ikijadiliwa na hata kupelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya kadhi.Huenda ilikua janja ya nyani kula indi bichi ili kushawishi kundi linalodai mahakama hiyo na kupata kuungwa mkono kwa mambo fulani yanayotakwa na wapenda madaraka.

Sasa ni wazi kuwa mswada wa mahakama ya kadhi umetoswa baada ya kuona jinsi hali ya hewa ilivotaka kuchafuka huko bungeni na baadaye ingekua huku uswazi(MUNGU aepushie mbali)

Hivyo,endapo Mh.Pinda alitaka kuwafurahisha waislamu,sijui sasa atawaambia nini? Na huko kwa wakristo nako sijui atawaeleza nini? Atagombea urais kweli,au amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe?

Wanasiasa huwa hawana aibu,ngoja tumsubiri !
Silaha ni moja tu nayo ni kulia
 
Back
Top Bottom