kensh
JF-Expert Member
- Jul 19, 2012
- 527
- 113
Hoja ya mahakama ya kadhi tumeiona jinsi ilivyoibua hisia kali na hali ya sintofahamu ktk jamii.Ilipelekea Mh.Mtikila kuwahi mahakamani kuipinga isizungumzwe bungeni.
Maaskofu na watu wasio na maslahi na mahakama ya kadhi,waliipinga kwa hoja na hata kuionya serikali isithubutu kuinzisha mahakama hiyo.
Waziri mkuu na mwanasheria mkuu waliikomalia na kushawishi sana kuwa haina madhara endapo ikijadiliwa na hata kupelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya kadhi.Huenda ilikua janja ya nyani kula indi bichi ili kushawishi kundi linalodai mahakama hiyo na kupata kuungwa mkono kwa mambo fulani yanayotakwa na wapenda madaraka.
Sasa ni wazi kuwa mswada wa mahakama ya kadhi umetoswa baada ya kuona jinsi hali ya hewa ilivotaka kuchafuka huko bungeni na baadaye ingekua huku uswazi(MUNGU aepushie mbali)
Hivyo,endapo Mh.Pinda alitaka kuwafurahisha waislamu,sijui sasa atawaambia nini? Na huko kwa wakristo nako sijui atawaeleza nini? Atagombea urais kweli,au amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe?
Wanasiasa huwa hawana aibu,ngoja tumsubiri !