sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Imekuwa ni desturi yetu na ndo tumezoeshwa na wabunge wa chama cha magamba,ili wakubalike kwa wananchi lazima watoe vijipesa.sitaki kuamini pesa ni kigezo kwa kiongozi kukubalika ndani ya jamii.Leo hii mida ya saa nne asubuhi kwa macho yangu nimethibitisha yanayosemwa juu ya viongozi wetu kujikomba kwa wapiga kura wao kwa kutumia vijisenti.Ni fedheha kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini anayejiita kipenzi cha watu kuwashawishi vijana kwenda kusikiliza mkutano wake wa hadhara kwa kuwapa vijisenti.Upofu huu umepelekea kujenga hoja zisizo na mashiko za kutaka kuongezewa posho kwasababu miongoni mwa posho hizo huzipeleka kuwasaidia wapiga kura wao.Kitendo hiki cha mheshimiwa huyo hakikubali hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali inajaribu kuwazuia wapiga debe katika vituo vya mabasi.Na kama kuna viongozi wanaodhani pesa ni kigezo cha kukubalika wajue wanapoteza wakati wao bure.naomba kuwakilisha