Mh. Mbunge Maselle na atoa bingo kwa wapiga debe

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Imekuwa ni desturi yetu na ndo tumezoeshwa na wabunge wa chama cha magamba,ili wakubalike kwa wananchi lazima watoe vijipesa.sitaki kuamini pesa ni kigezo kwa kiongozi kukubalika ndani ya jamii.Leo hii mida ya saa nne asubuhi kwa macho yangu nimethibitisha yanayosemwa juu ya viongozi wetu kujikomba kwa wapiga kura wao kwa kutumia vijisenti.Ni fedheha kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini anayejiita kipenzi cha watu kuwashawishi vijana kwenda kusikiliza mkutano wake wa hadhara kwa kuwapa vijisenti.Upofu huu umepelekea kujenga hoja zisizo na mashiko za kutaka kuongezewa posho kwasababu miongoni mwa posho hizo huzipeleka kuwasaidia wapiga kura wao.Kitendo hiki cha mheshimiwa huyo hakikubali hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali inajaribu kuwazuia wapiga debe katika vituo vya mabasi.Na kama kuna viongozi wanaodhani pesa ni kigezo cha kukubalika wajue wanapoteza wakati wao bure.naomba kuwakilisha
 
Huyu bwana ndogo anapoteza muda kweli na pesa zake,najua watachukua pesa na hawataenda.anacheza na wanashinyanga?
 
Mbona kama unasitasita vile, kuwa wazi alikuwa wapi,lini,na akina nani, akafanya nini,kwa mtindo upi?...........
 
We Ng'wana sweke usichoelewa ni nini hapo? umeshaambiwa ameonekana akitoa pesa, kwa vijana leo asubuhi ukiwambiwa wapi na kwa mtindo gani wewe itakusaidiaje? kama ni Ngokolo au Nguzo nane bado haitabadili ujinga wa huyo mbunge. Au ni anko wako? coz hili jina lako lenyewe ni la huko huko! am doubted....!
 
Ningekuwa mshauri wa masele ningemsihi asipoteze muda wake pale shy mjini. Ukweli kwamba kama kuna ngome ambayo cdm wanaweza kujivunia basi shy ni mojawapo. Magamba hawana chao pale.
 
We Ng'wana sweke usichoelewa ni nini hapo? umeshaambiwa ameonekana akitoa pesa, kwa vijana leo asubuhi ukiwambiwa wapi na kwa mtindo gani wewe itakusaidiaje? kama ni Ngokolo au Nguzo nane bado haitabadili ujinga wa huyo mbunge. Au ni anko wako? coz hili jina lako lenyewe ni la huko huko! am doubted....!

Taratibu mkuu samahani kama nimekukwaza,inabidi uniombe radhi kwa kunifikiria mie ni ndugu na huyo kilaza wa magamba.
 
Nimemuona kwa macho yangu mkabala na benki ya NBC sehemu marufu kwa jina la lumambo kituo kidogo cha mabasi yaendayo Kahama,kiasi cha kutaka kusababisha tafrani kwa wapiga debe hao kwa kugombea mgawo wa mh. huyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom