TANAPA yaingizwa mkenge, yatumiwa kugawa rushwa kwa Wajumbe wa CCM Bunda Vijijini

chuki

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,715
533
Katika hali isiyo ya Kawaida tarehe 17/01/2020 TANAPA na TAWA wameingizwa mkenge na Mbunge wa jimbo la Bunda Vijijini Bonifasi Mweta Getere kwa kulipa wajumbe wa ccm ambao walikuwa wameitwa kwa kampeni za mbunge huyo.

Katika shughuli hiyo Rushwa ilikuwa wazi kwani Wajumbe zaidi ya 500 wamelipwa shilingi 50,000/- na 100,000/- kwa kigezo kuwa wamehudhuria usomaji wa utekelezaji wa Ilani.

Pesa hizo zote zimelipwa na TANAPa kwaajili ya kumpendelea mbunge huyo ili apitishwe kura za maoni.

Alipoulizwa kwanini anatumia mashirika ya umma vibaya alisema hakuna wa kumfanya kitu kwani yeye ni mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na anajuana nao kwani kuna madili mengi '' wanakula" wote.

Katika mkutano huo baadhi ya viongozi wa mkoa na wilaya wa ccm wamealikwa na kugawiwa 'posho' nono ili kubariki 'ubatili' huo.

Kwani hakuna kikao cha namna hiyo cha kusoma Ilani na hakuna utaratibu huo kikanuni na kikatiba.

Katika maelezo yake mbunge amekiri kuwa amealika kikao cha 'kuwafurahisha' wajumbe ili wamkumbuke hapo baadae.

Upande wa Tanapa wanadai walikuwa wanatoa semina, hivyo kuhitimisha kuwa ni mkakati wa Rushwa ya wazi kwaajili ya kumbeba mbunge.

My take: Kwakuwa hii ni Rushwa na Uhujumu Uchumi, Vyombo vya Dola wawahoji Tanapa kwanini wanatumia vibaya Mfuko huo wa umma kwa manufaa ya mtu.

Chama cha Mapinduzi kiwahoji viongozi kwa kupokea malipo batili na kanuni ipi imeongoza kuitisha mkutano ukijumuisha wapiga debe na watu wasio wana ccm kusoma Ilani katika jimbo moja .

Rushwa Bunda ni kama samaki na Maji.
 
Rushwa imekomaa Sana ndani ya CCM sasa hawaoni aibu mpaka wanatumia fedha ya umma kulipa rushwa
 
Ni majungu tu. Chama chetu hakijapuliza kipyenga cha uchaguzi. Mkutano huo ulikuwa kuputia utekelezaji wa ilani, pia TANAPA na TAWA wanatekeleza ilani ya CCM
 
Hakuna tatizo kwani wajumbe hawa waliitwa ghafla na kushindwa kuacha hela ya mboga majumbani mwao hivyo kuwapa hela hiyo ya mboga ni utaratibu wa kawaida ambao sisi kama taifa tumejiwekea kwa watu wote salio na wasio na vyama, hata wewe ungetaka ungepewa.
 
Waziri mwenye dhamana analijua hili? Vinginevyo inaweza kuwa ni majungu,chuki,wivu na uzandiki
 
Wacha kuchafua watu elfu 50 Ni rushwa kweli? Au posho ya kikao?
 
Back
Top Bottom