Mh. Livingstone Lusinde Under Microscope?

Mh. Livingstone Lusinde Under Microscope?

Mbabe wa matusi Livingstone Lusinde anatinga kortini lini.
Matusi dhidi ya CHADEMA na viongozi wake hayavumiliki.
 
Kuendelea kumjadili Lusinde humu ndani lazima uwe na moyo wa mwendawazimu!
 
Mbabe wa matusi Livingstone Lusinde anatinga kortini lini.
Matusi dhidi ya CHADEMA na viongozi wake hayavumiliki.

Atatinga Kortini mpaka siku atakapo shitakiwa. Lakini nadhani hajafanya kitu chochote kibaya maana mpaka sasa hatujasikia hata mwenyekiti wa chama chake akiwataka radhi Watanzania na mbaya zaidi yeye ndiye aliyemtuma kufanya kile alichokifanya.
 
Sidhani kama CCM wanaweza kumtuma Lusinde kuwatukana wananchi Arumeru.
Mi ninadhani tatizo liko kwake yeye mwenyewe Lusinde kutokana na makuzi aliyolelewa tangu akiwa mtoto.
Ambacho ningemshauri NAPE pamoja na wakuu wake ni kumchulia hatua kali huyu jamaa kwakuwa ameki-underlet chama kwa Watanzania na yeye mwenyewe.

Ni wazi kwamba mitusi ile ya nguoni wameisikia na inachefua, hili halina mjadala abadani! Napata shaka pia mbinu zilizotumiwa mpaka huyu jamaa akapita NEC na kuliwakilisha jimbo la Mtera katika nafasi aliyonayo.

Huyu jamaa ameonyesha ujuha mkubwa sana katika medani za siasa hapa Tanzania, tukubali kuwa huwa kuna vijembe na utani katika siasa lakini si MATUSI yale! Lakini pia tukipitia CV yake, elimu yake ni kipimo cha ujuha aliouonyesha.

Kama mtakuwa makini, angalieni michango yake awapo bungeni, si ya kutetea na kutatua kero za wananchi wa jimbo lake la Mtera.
Awapo bungeni maranyingi ni kusifia serikali na kuponda wapinzani as if ameenda mjengoni kutalii.

NAPE, pamoja na sababu nyingine mtazozigundua wakati mnafanya tathmini yenu, LUSINDE ni mmojawapo aliyewapunguzia kura kule Arumeru( Zingatia hili kwa kuwa nimdau mzuri humu ndani JF,washirikishe wakuu wako).

CDM anzeni mikakati mapema kulikomboa jimbo la Mtera mikononi mwa wanyang'anyi. Lusinde si kosa lake, tatizo ni shule! Nape mpelekeni shule huyo kijana. Mitusi ile inatisha mpaka masikio yanawasha ukisikia, cjui hao watoto wake alio zaa wanajifunza nini.
 
Ha ha haaaa alisema eti wenzake watakuwa na twins ifikapo tarehe 1 april kumbe hakujua yeye ndo alikuwa na irresistible abortion! Lusinde wala hafai hata kuongoza Kaya wacha jimbo!
 
Mleta hoja, ingependeza zaidi kama title yako ingekuwa na kiulizi (?)
kwani kwa jinsi ilivyo na mada uliyoleta ni vitu viwili tofauti. Hata hivyo,
tunapaswa kuangalia jinsi ya kuikomboa nchi badala ya kumfikiria mtu
mropokaji...
 
Tuwaachie Cheap politics zao CCM, kortini wapi haki itatendeka kama mkuu wa nchi na mwenyekiti wake yuko kimya.
 
Nikimwangalia Dr Slaa halafu nikikumbuka maneo ya Lusinde....navunjika mbavu tu!!
Hongereni CDM kwa kushinda Arumeru....its my first time naingia kwenye hili jukwaa!! Hope mmesheherekea ushindi salama salmini!!
Angalizo: Dont quote!!:shut-mouth:
 
Kwa kweli Wadau wenzangu, yaani hapa nipo nasubiria kuona Serikali na Chama Tawala watafanya nini baada ya Mh.Lusinde kada wao kutoa Sera za Chama chake.
 
mweshimiwa ulie towa hoja umesahau kuweka elimu yake ya sekondari na chuo
 
04_11_4s6769.jpg




Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na watoto Levina Lusinde (kushoto) na Isaya Lusinde kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma juzi. Hawa ni watoto wa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Je hawa watoto wanajua lolote kuhusu baba yao? Na malezi yao yakoje?
.........Duh....
 
Inawezekana watoto wasijue matendo mabaya ya mzazi wao Livingston Lusinde unawaona wapo smart na PM wamevalia nadhifu sijui wakitoka shule au kumpokea baba yao akitokea mjengoni bila kujua baba yao anafanya nini Bungeni,anazungumza nini na walipa kodi ambao ndio waliompa kibali cha kwenda kuwatetea matatizo yao.Lusinde sio mwanasiasa kuna uwezekano wananchi wa mtera walimpa kura kumuondoa Ndugu Mallechela ambaye naye walishamchoka kwa maana alitaka uongozi wa kifalme wananchi wakampumuzisha.Lusinde alishawahi kusema jukwaani kwamba endapo CCM ingeshidwa uchaguzi wa Igunga angekunywa Sumu afe wananchi wanaoifahamu Siasa na waliompima akili yake kwa kumuangalia wakaona wasikipe chama pinzani asije akafa kwa sumu,uchaguzi wa Arumeru akayarudia yaleyale sasa tunamuomba anywe sumu Afe na tutamzika au aachane na siasa kwa vile anachafua uwanja wa siasa.
 
Sidhani kama Lusinde ndiye yuko under microscope. Otherwise, utakuwa una-narrow tatizo na kufanya solution isipatikane. Tatizo hapa ni Watanzania wenyewe. Kama walikuwa tayari kuwa pale kusikiliza na kushangilia kwa yale waliokuwa wanayasikia, basi wao ndio wanatakiwa kuwa under microscope. Labda na wale waliomchagua pia. Kumbuka Lusinde ni mwakilishi wa watu na possibly ata-reflect waliomchagua.

Kama hao Watanzania wangekataa kusikiliza matusi, angeyasemea wapi? Ndio maana hata chama chake kinaweza kisimchukulie hatua zozote kwa sababu kinajua wazi walio na tatizo ni akina nani.

Kwa hiyo, badala yake, hotuba yake ya matusi ingekufanya binafsi upende kujua kwa undani baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Watanzania waliokuwa wanamsikiliza na kumshangilia kama:

1. Wanazo akili timamu kweli?
2. Kama hawana akili sheria inasemaje kwa mtu asiye na akili?
3. Kama wanazo kwa nini walishangilia matusi yale?
4. Je historia yao ikoje?
5. Malezi yao yalikuwaje?
6. Na mengine ambayo wadau mtapenda kuongezea.


maneno yamenikosha haya n ni points tupu
 
Back
Top Bottom