kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,612
Kwakuwa wewe uko na unaongea nao vizuri ninaomba tafadhali mkikutana uso Kwa uso utusaidie kuwakumbusha na kuwadai yafuatayo.
1. Watulipe fidia Kwa Mali zetu walizotuibia wakati wa ukoloni, biashara ya utumwa na kutulazimisha kupigana Kwa maslahi Yao wakati wa Vita kuu ya Kwanza na pili ya dunia. Fidia hizo ni muhimu kwetu hasa kwenye ujenzi wa demokrasia na uchumi nchini
2. Waruhusu bidhaa zetu ziingie kwenye masoko Yao, vinginevyo demokrasia bila uchumi itashindikana Africa
3. Wapunguze riba kwenye mikopo yao wanayoipatia Tanzania ili kutupunguzia mzigo wa kulipa madeni makubwa.
4. Wasitumie adhabu za kutunyima misaada ili kushinikiza jambo fulani Tanzania kwani wanaoathirika zaidi Kwa ukosefu wa misaada ni wananchi wanyonge watakaokosa hela za madawa, barabara, reli, pembejeo za kilimo, nk badala ya viongozi wanaowakusudia.
5. Wasitulazimishe kuukubali na kuuhalalisha ushoga Kwa nguvu
6. Wasiuze mitumba kwetu kama njia ya kutupa takataka zao kwetu.
7. Wasiwakumbatie viongozi wa Afrika wanaobadili katiba zao ili waendelee kubaki madarakani kama wanavyofanya Kwa baadhi ya nchi.
Mh. TL naomba kila ukiongea nao usisahau kuwachomekea haya japo hata Kwa utani Tu. Wasidhani kuwa wao ni wasafi Sana kuliko Sisi, wasifikirie kuwa Sisi wote hatujitambui na hatutambui kuwa wao ndio chanzo cha Hali zetu hizi.