Wanasiasa si Watawala wetu, usitumike

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Tanzania kama yalivyo mataifa mengine duniani, ni jamii ya mfumo wa Kibepari. Mfumo ambao, endapo unakomaa miongoni mwa watu wake, basi maslahi ya mtu mmoja huwa na nguvu dhidi ya maslahi ya watu wengi. Muda mwingine maamuzi ya wachache, hutawala mifumo ya maisha ya wengi.

Demokrasia imetupandikizia imani ya kudhani kuwa, viongozi tunaowachagua kupitia uchaguzi, ndio Watawala, La hasha! Tunajidanganya, kwa sababu, Demokrasia ya Utawala wa watu, haina uhai kwenye Jamii ya Kibepari.

Kwanini Demokrasia inakosa nguvu kwenye mfumo wa Kibepari?

Jibu
: kwa sababu, Demokrasia ni mfumo wa Kisiasa zaidi kuliko kiuchumi, na Ubepari ni mfumo wa Kiuchumi zaidi kuliko Kisiasa. Hivyo, nguvu ya uchumi, inaweza kununua nguvu ya Siasa ambayo ndio inatawala. Hii ina maana kuwa, watu wenye nguvu ya Uchumi wanainunua Siasa, ndio mana nahitimisha kwa kusema, Wanasiasa si Watawala wetu.

Watawala wetu ni nani?

Kuna makundi ya watu ambao wanamiliki shughuli za Uchumi zinazochangia uchumi ambao ndio nguvu ya taifa. Hawa ni Wafanyabiashara na Wawekezaji wakubwa, ambao, Wanasiasa hufanya kazi ya kushawishi umma ukubaliane na maslahi yao.

Mfumo huu, upo dunia nzima, na ikiwa jamii inasalia kwenye muundo wa Kibepari, basi mfumo huu hauepukiki.

Tufanyeje?

Kwa kuwa hatuwezi kuepuka muundo huu wa Kijamii, ambao ni muundo fair kwenye jamii ya Kibepari, ushauri wangu kwako, hasa kijana ni mambo matatu yafuatayo.

  1. Ondoa dhana ya kudhani Siasa haikuhusu; ikiwa unadhani kujihusisha na Siasa ni kwa ajili ya watu wachache, basi utaacha hata kundi la Wanasiasa wenye Elimu na Ujuzi kutekeleza maslahi ya kundi la watu wenye nguvu ya Uchumi hata yakiwa hayana tija kwako kama raia. Zingatia mabadiliko ya Sera, kanuni na sheria. Kemea kama jambo halina tija kwako.
  2. USITUMIKE: kwa kawaida, ikiwa lipo kundi la Wanasiasa/Wafanyabiashara, ambao kwa akili yako unaona wakitumia Utashi wako kupenyeza maslahi yao, basi jifunze kanuni moja ya kitu chochote kitumiwacho. Ikiwa Mtumiaji atakidhi maslahi yake, hivyo, wewe kama kijana hautakuwa na kazi tena, na thamani yako haitaonekana tena. Zaidi, manufaa pekee utakayokuwa umepata, ni yale ya kukidhi mahitaji yako ya muda mfupi. Na kama utashtuka, utakuwa umeshachelewa. Hutahitajiki tena.
  3. Tanguliza maslahi ya nchi kabla ya chama au dini yako: ikiwa umezoea kupitia kwenye majukwaa mbali mbali ya mitandao ya kijamii, mijadala mingi inajadiliwa zaidi kwa milengo ya Vyama vya Siasa na Dini. Tafakuri za vijana zimeelemewa na hizo Taasisi mbili kiasi kwamba hawajiwezi tena. Hapa ndipo Wanasiasa wakiwa kama expert manipulators wanapotupatia vijana, na wanapoweza kuzitawala akili zetu.

Tusitengane, UMOJA NI NGUVU.

Mwl. Diwani
 
Back
Top Bottom