Mh. Lisu tusaidie haya huko

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,222
2,000
Kwakuwa wewe uko na unaongea nao vizuri ninaomba tafadhali mkikutana uso Kwa uso utusaidie kuwakumbusha na kuwadai yafuatayo.
1. Watulipe fidia Kwa Mali zetu walizotuibia wakati wa ukoloni, biashara ya utumwa na kutulazimisha kupigana Kwa maslahi Yao wakati wa Vita kuu ya Kwanza na pili ya dunia. Fidia hizo ni muhimu kwetu hasa kwenye ujenzi wa demokrasia na uchumi nchini

2. Waruhusu bidhaa zetu ziingie kwenye masoko Yao, vinginevyo demokrasia bila uchumi itashindikana Africa

3. Wapunguze riba kwenye mikopo yao wanayoipatia Tanzania ili kutupunguzia mzigo wa kulipa madeni makubwa.

4. Wasitumie adhabu za kutunyima misaada ili kushinikiza jambo fulani Tanzania kwani wanaoathirika zaidi Kwa ukosefu wa misaada ni wananchi wanyonge watakaokosa hela za madawa, barabara, reli, pembejeo za kilimo, nk badala ya viongozi wanaowakusudia.

5. Wasitulazimishe kuukubali na kuuhalalisha ushoga Kwa nguvu

6. Wasiuze mitumba kwetu kama njia ya kutupa takataka zao kwetu.

7. Wasiwakumbatie viongozi wa Afrika wanaobadili katiba zao ili waendelee kubaki madarakani kama wanavyofanya Kwa baadhi ya nchi.

Mh. TL naomba kila ukiongea nao usisahau kuwachomekea haya japo hata Kwa utani Tu. Wasidhani kuwa wao ni wasafi Sana kuliko Sisi, wasifikirie kuwa Sisi wote hatujitambui na hatutambui kuwa wao ndio chanzo cha Hali zetu hizi.
 
master09

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
787
1,000
Umetoa ushauri mzuri sana ila sidhani kama yeye TL amefocus kwa hilo .....sisi waafrica hasa watanzania bado hatujui nia na lengo hasa la hawa wazungu ..... kuna msemo flani nikiwa masomoni huko asia nilipata kuambiwa ........
"Mtu mweupe (Mzungu,Mwarabu,Muhindi) hawezi kuwa rafiki yako tuu unless kuna kitu anapata kutoka kwako au kupitia kwako" ......
Hii kitu ni ukweli kabisa na nimeshuhudia ....Wazungu watampapalikia kila kona na hata accommodation ndogo ndogo atapewa but wazungu wanafaidika zaidi kupitia yeye ila yeye amefocus kwenye ubinafsi ....utumwa bado upo katika ukimwengu huu ...

Ukitaka Lissu aongee hayo hatapata coverage au support ya hao wazungu kama hii ya sasa anayo pata ....

Cc:kavulata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,222
2,000
Hakuna umaskini mbaya Sana duniani kama wa umakini wa fikra. Wazungu siku zote wanaomba Mungu waafrika wafe wooote ili waje kuishi Africa, wazungu wanatafuta kila sababu ya kurudi tena Africa, wazungu wanatafuta kila sababu ya kutuuzia silaha toka mwenye viwanda vyao.

Watawala wetu wengi hawalijui hili, right kama wangelifahamu hili wangeshiriki kwenye kufanya chaguzi za haki, wangeunda serikali za umoja, wangehubiri amani na upendo Kwa watu wao ili kuwanyima wazungu nafasi ya kuingia tena Africa. Maana Africa hakuna mtawala ambaye anaweza kuzuia machafuko kama machafuko hayo yataungwa mkono na wazungu. Tunajidanganya kutegemea mkono wa chuma kuzitangulia mbele siasa zetu. Ni upendo, majadiliano na haki Kwa woteTu Kwa watu wetu vitakavyoweza kuwachelewesha wazungu kurudi Afrika tena. Sio ubabe wa viongozi wa Africa wala majeshi ya Africa.
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,308
2,000
Hataweza kufanya hivyo kwakuwa ziara yake ni ya kutafuta support ili awe Rais kisa tu kapigwa risasi.

Sasa sijui wale waliopigwa Risasi kwenye vita ya Uganda nao wangerudi hapa na kuanza kudai kuwa marais wote.
 
Towned

JF-Expert Member
Aug 7, 2018
226
500
Hataweza kufanya hivyo kwakuwa ziara yake ni ya kutafuta support ili awe Rais kisa tu kapigwa risasi.

Sasa sijui wale waliopigwa Risasi kwenye vita ya Uganda nao wangerudi hapa na kuanza kudai kuwa marais wote.
Sasa akipata Urais kwa support yao si watakuwa wanampelekesha kama mzoga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,605
2,000
Umetoa ushauri mzuri sana ila sidhani kama yeye TL amefocus kwa hilo .....sisi waafrica hasa watanzania bado hatujui nia na lengo hasa la hawa wazungu ..... kuna msemo flani nikiwa masomoni huko asia nilipata kuambiwa ........
"Mtu mweupe (Mzungu,Mwarabu,Muhindi) hawezi kuwa rafiki yako tuu unless kuna kitu anapata kutoka kwako au kupitia kwako" ......
Hii kitu ni ukweli kabisa na nimeshuhudia ....Wazungu watampapalikia kila kona na hata accommodation ndogo ndogo atapewa but wazungu wanafaidika zaidi kupitia yeye ila yeye amefocus kwenye ubinafsi ....utumwa bado upo katika ukimwengu huu ...

Ukitaka Lissu aongee hayo hatapata coverage au support ya hao wazungu kama hii ya sasa anayo pata ....

Cc:kavulata

Sent using Jamii Forums mobile app

Maguful kazi take nini?
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,605
2,000
Hataweza kufanya hivyo kwakuwa ziara yake ni ya kutafuta support ili awe Rais kisa tu kapigwa risasi.

Sasa sijui wale waliopigwa Risasi kwenye vita ya Uganda nao wangerudi hapa na kuanza kudai kuwa marais wote.

Mwambieni pombe ndiye mhusika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom