Mh. Lipumba kaonyesha ukomavu wa kisiasa

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836


Tutoe sifa pale sifa inapobidi itolewe. Mh. Lipumba kaonyesha uongozi wa kweli kwa kwenda kumtembelea Mbowe central kwa nafasi yake ya mwenyekiti wa Tanzania Centre for Democracy inayounganisha vyama vyote vya upinzani vyenye wabunge.

Kaongea kwa busara sana.
 
Last edited by a moderator:
nimemsiki hata mimi safi sana na ametoa tahadhali kwa serikali kuwa watu wa arusha awataki mchezo je polisi watatumia usafiri gani kwenda mahakani kesho arusha kwa sababu watu wa arusha awatabiriki
 
HONGERA SANA MH.lipumba...NI MFANO WA KUIGWA NA VIONGOZ WOTE WA CHAMA TAWALA NA UPINZANI.....:madgrin:
 
Nimesikiza hizo comments za Lipumba na ninamshukuru Lipumba lakini kwa kutumia caution kubwa. Ameongea vitu vya maana sana na kitu ambacho amekigusia kikubwa ni kwamba ccm na katiba yao kweli wanaonekana wazi nia zao za kuleta umwagaji wa damu Tanzania. Sasa sisi watanzania tuchukue sheria zetu mikoni kwa sababu kikwete anachukua sheria anazojua yeye na familia yake. Kifupi ni kwamba hakutakuwa na bunge dodoma na nchi itasimama wiki hii thats it, mpaka tutoe fundisho kwa kikwete na ccm watambue kwamba wananchi ndio wanaongoza nchi hii sio ccm...
 
CDM mmeshikwa makalio hadi lipumba mna muona kwa sasa si ndio huyu huwa mnamuita mwenyekiti wa CCM-B?

Amegundua kuwa alikuwa anapotea. Halafu nae si walishawahi kumvunja mkono na kumuweka ndani kwenye moja ya chaguzi huko miaka ya nyuma kwa hiyo anajua uchungu wake
 
Polisi wetu nao wakati mwengine watumie busara kuliko nguvu, intelejensia yao pia iwaongoze kujuwa hasila ya wananchi kutokana na mambo yao wanayoyafanya. Wanasifika kwa rushwa, matumizi ya risasi yasiyokuwa na sababu za msingi.
 
Amegundua kuwa alikuwa anapotea. Halafu nae si walishawahi kumvunja mkono na kumuweka ndani kwenye moja ya chaguzi huko miaka ya nyuma kwa hiyo anajua uchungu wake

Palipo na sifa tusifie.Prof Lipumba kaonesha ni namna gani amekomaa kisiasa.Acheni porojo hazisaidii,tuwe waungwana.Ukiona unakerwa basi don't contribute.
 
Lipumba ni mwenyekiti wa kituo cha demokrasia tz hivyo ilimpasa aende
 
Sasa asingekwenda pale central angeandikwa kwenye gazeti kwa story ipi? anatafuta media coverage tu hana lolote mnafki mkubwa huyu, mbona akwenda Tabora ambako mbunge wa chama chake Sakaya mpaka leo yuko lupango? this is too low to me.
 
Palipo na sifa tusifie.Prof Lipumba kaonesha ni namna gani amekomaa kisiasa.Acheni porojo hazisaidii,tuwe waungwana.Ukiona unakerwa basi don't contribute.


Nampongeza Professa kwa kuonyesha SOLIDARITY na ukomavu wa hali ya juu bila unafiki. Kwa umoja wa namna hii ni dhahiri safari ya kwenda tunakotaka kuelekea imewadia kwani tayari tumegundua tuna COMMON ENEMY na lazima tupigane kama jeshi la pamoja ili kumtoa huyu adui fedhuli
 
Kwa hakika anastahili pongeze, lakini asimsahau Magdalena Sakaya kule Tabora, aende akamuwekee dhamana. Umoja ni Nguzu. Hongera Lipumba. Umegundua kosa lako sasa uko kwenye mstari ulionyooka.
 
naamini seriali imemsikiliza nasikia kuna video imewekwa humu najaribu kui search sijaipata naomba mnisaidie na mie niione pliz
 
Nampongeza sana Mh. Prof. Lipumba, kitendo chake kina maana sana kwa siasa za Tanzania
 
Back
Top Bottom