Mh. Lema aandika historia mpya

Mh. Lema aandika historia mpya

Wa Kwilondo

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2007
Posts
1,081
Reaction score
313
KWA mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mgogoro wa umeya jijini Arusha, mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema (CHADEMA), jana alishiriki kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliongozwa na mwenyekiti wa muda, Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe (CHADEMA).

Mgogoro wa umeya jijini Arusha, ulichukua sura mpya baada ya madiwani wa CCM kuwazunguka wenzao wa CHADEMA mwaka 2010 na kumchagua Gaudence Lyimo kuwa meya, jambo lililozua tafrani kubwa.

Baadaye mgogoro huo ulikua, huku CHADEMA wakiendelea kutomtambua meya huyo, jambo ambalo lilisababisha madiwani wao watano kuvuliwa uanachama baada ya kufikia muafaka hewa na CCM.

Katika uchaguzi mdogo wa kata hizo nne Julai mwaka huu, CHADEMA iliibuka kidedea na hivyo kuzua hofu kuwa huenda ikatumia wingi wake kumng'oa meya, hatua ambayo Lema alisema si ajenda yao kwa sasa bali kuwatumikia wananchi.

Jana wakati baraza hilo lilipokutana, Diwani wa Kata ya Sokon 1, Michael Kivuyo (TLP), alikieleza kikao kuwa Meya Lyimo amesafiri, hivyo amemkaimisha ofisi kutokana na halmashauri hiyo kutokuwa na naibu meya.

Taarifa hiyo iliibua mjadala huku madiwani wakitaka kanuni zifuatwe, ndipo Diwani wa Kata ya Levelos, Ephata Nanyaro (CHADEMA), alimpendekeza Msofe awe mwenyekiti wa muda wa kikao hicho.

Katika kura zilizopigwa, Msofe alipata 13 za kumkubali huku nne zikimkataa.

Kikao hicho kiliibua hoja ya upotevu wa zaidi ya sh milioni 14.8 ambapo kati yake fedha taslimu ni zaidi ya sh milioni 8.6 zilizodaiwa kwisha kutokana na makato ya benki ya kuhudumia akaunti.

Matumizi mengine ni vifaa kwa ajili ya ujenzi wa tarafa ikiwemo saruji na mchanga vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 6.3 ambavyo vilichangwa na wananchi.

Madiwani hao walimuagiza kaimu mkurugenzi wa jiji, Afwilile Lamsy, kuhakikisha kwenye kikao kijacho analeta taarifa za kibenki za akaunti iliyowekwa fedha hizo mwaka 2004 ili kuona namna zilivyokatwa hadi zikaisha. .

"Tunataka kuonyeshwa taarifa za benki tujue namna fedha hizo zilivyotumika, hatutaki kuona barua za mawasiliano ya mkurugrnzi na mkuu wa wilaya, tunataka wale wote waliohusika waletwe hapa hata kama walihamishwa watafutwe waletwe.

"Hii ni fedheha kubwa, haiwezekani wananchi wachange fedha halafu zipotee hivi hivi tu, tunataka tuletewe hapa taarifa za benki na tupelekwe tukaone mchanga na saruji vilivyonunuliwa," alisema Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Doita Isaya (CHADEMA).

Pia madiwani hao waliwaagiza wataalamu kupima maeneo muhimu ikiwemo mito, hifadhi za barabara na maeneo ya milima na kuyawekea alama ili kuyalinda yasivamiwe kama hali inavyoonekana kwenye maeneo mengi ya jiji la Arusha.

SOURCE: Tanzania Daima
 
"Pia madiwani hao waliwaagiza wataalamu kupima maeneo muhimu ikiwemo mito, hifadhi za barabara na maeneo ya milima na kuyawekea alama ili kuyalinda yasivamiwe kama hali inavyoonekana kwenye maeneo mengi ya jiji la Arusham"

Wanataka kuvunjwa hotel ya Kada wa CCM pale 7Up?
 
Nimejaribu kusoma ili kujionea hiyo historia mpya iliyoandikwa na Lema ni ipi?!.

Kwa vile tunatofautiana uelewa, naombeni mlioelewa mnisaidie!.

Tanzania Daima bana!,nalo sometimes...
Pasco
 
Yaani mbunge kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani ambacho yeye ni mjumbe kisheria na ni wajibu wake kuhudhuria ni historia!!!

Ama kweli Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
Impressive!! Natamani uwajibikaji wa namna hii ungeambukizwa kwetu sote,halmashauri zote, wilaya zote, mikoani, na kwa ngazi ya taifa pia.,
Lakini kwetu pia wenyenafasi za usimamizi katika private entities mbali mbali, this is the right spirit!!

Hongera kamanda lema keep up the good works!!
 
Nimejaribu kusoma ili kujionea hiyo historia mpya iliyoandikwa na Lema ni ipi?!.

Kwa vile tunatofautiana uelewa, naombeni mlioelewa mnisaidie!.

Tanzania Daima bana!,nalo sometimes...
Pasco

Mkuu PASCO mbona imejieleza vizuri au we ulitaka historia ya namna gani?
 
Yaani mbunge kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani ambacho yeye ni mjumbe kisheria na ni wajibu wake kuhudhuria ni historia!!!

Ama kweli Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...[/QUOTE

Kwa nyinyi CCM mtaona si kitu kwa kuwa alipokuwa nje ya vikao mlikuwa mnapeta tu sasa karudi imekuwa moto kwenu na mahesabu lazima yafanyike kama mligawana na meya wenu wa kuchonga ndiyo mtamjua Lema ni nani!!
 
Speed yetu ile ile 120 na 2014/15 tunaipeleka mpk 180 naikibidi 220 ili wakae kabisa, lazima tuhakikishe wananchi wanapata huduma muhimu zote24/7 na hii system niya ku upgrade yote kiujumla na sio mafungu mafungu kama ilivyo sasa
 
Hiyo ni moja ya sababu,,kwanini tanzania tunakuwa masikini eventhogh tuna rasilimali zakutufanya tuwe vizuri kiuchumi.....sababu kubwa ni kuwa na viongozi ambao sio wazalendo bali wanajali maslai yao kwanza alafu taifa baadae,,,,,,wakibainika watimuliwe tuuu
 
Nimejaribu kusoma ili kujionea hiyo historia mpya iliyoandikwa na Lema ni ipi?!.

Kwa vile tunatofautiana uelewa, naombeni mlioelewa mnisaidie!.

Tanzania Daima bana!,nalo sometimes...
Pasco

Nadhani kama ni kweli kuwa kwa muda wote wa ubunge wa mh. Lema kama mbunge wa Arusha mjini hajawahi kuhudhuria kikao hicho cha madiwani isipokuwa kwakuandaa harakati zakipinzani nje ya utaratibu wa vikao rasmi vya halmashauri, na kama sasa kwa Mara ya kwanza anafika mahali anajiridhisha kuwa haki inaweza kutendeka ka vikao hivyo vya madiwani na anahudhuria sasa kwa Mara ya kwanza kabisa katika kikao rasmi - nadhani hii ndiyo historia mpya inayoelezwa na mwandishi wa taarifa hii kama sijaielewa vibaya na kama hizi facts ni sahihi.
 
Yaani mbunge kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani ambacho yeye ni mjumbe kisheria na ni wajibu wake kuhudhuria ni historia!!!

Ama kweli Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
😛eace: mh. Lema kaweka historia kubwa kikwete hamfiki 😛eace:
 
Kwa sasa CDM Arusha tumejipanga na tuna support kubwa toka kwa baadhi ya madiwani wa ccm wenye uchungu na nchi yao so ccm wakae chonjo...Big up kamanda LEMA
 
Nadhani kama ni kweli kuwa kwa muda wote wa ubunge wa mh. Lema kama mbunge wa Arusha mjini hajawahi kuhudhuria kikao hicho cha madiwani isipokuwa kwakuandaa harakati zakipinzani nje ya utaratibu wa vikao rasmi vya halmashauri, na kama sasa kwa Mara ya kwanza anafika mahali anajiridhisha kuwa haki inaweza kutendeka ka vikao hivyo vya madiwani na anahudhuria sasa kwa Mara ya kwanza kabisa katika kikao rasmi - nadhani hii ndiyo historia mpya inayoelezwa na mwandishi wa taarifa hii kama sijaielewa vibaya na kama hizi facts ni sahihi.
Kwa hiyo ameweka historia ya kugundua upumbavu wake mwenyewe?
 
Speed yetu ile ile 120 na 2014/15 tunaipeleka mpk 180 naikibidi 220 ili wakae kabisa, lazima tuhakikishe wananchi wanapata huduma muhimu zote24/7 na hii system niya ku upgrade yote kiujumla na sio mafungu mafungu kama ilivyo sasa
Acheni kumwagia watu tindikali na kuwalisha sumu
 
Hawa watu wanaoongoza magenge ya kujilipua kwenye mikutano yao ni wa kulaaniwa milele
 
nimejaribu kusoma ili kujionea hiyo historia mpya iliyoandikwa na lema ni ipi?!.kwa vile tunatofautiana uelewa, naombeni mlioelewa mnisaidie!.tanzania daima bana!,nalo sometimes...pasco
hayo ni matatizo ya kulelewa ki propaganda,kila kitu mnaweka propaganda.
 
Back
Top Bottom