LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 530
- Thread starter
- #21
Nijuavyo mimi hakuna issue ya maana iliyoelezwa hapa.
Kashfa zote za EPA, scandal ya Meremeta, Deed Green, Tangold, Mwananchi Gold, IPTL na Kiwira zilitokea kabla ya Kikwete hajawa Rais na hicho kinachoitwa IPTL ni mkataba ambao uliingiwa na Tanesco tena wakati huo ukiwa umeshapitiwa na Baraza la mawaziri. Wanaotaka ajibu maswali hayo wanachotaka kujua kutoka kwake badala ya kwenda kwa Mkapa ni nini? Hawa hawa kwa kushirikiana na Marando ndiyo sasa wanaodai wizi wa fedha za ununuzi wa nyumba ya ubalozi Italia ni wa kutungwa kwa nia ya kumkomoa Mahalu wakati wanajua kwamba huyu Profesa kaiba kweli na ushahidi uko bayana. Ndio sasa wako busy kutayarisha nyaraka za kushinikiza mashtaka yafutwe.
Ukweli ni kwamba baadhi ya watu humu kama aliyepost thread hii ni watu waliovikwa kitambaa cheusi usoni na kukosa ufahamu wa jinsi viongozi wao walivyo na uhusika mkubwa katika yale wanayoyapiga vita.
Hata kama kuna masuala yalitokea kabla ya JK kuwa Rais, issue ni kwamba alipogundua kuna uozo mkubwa namna hiyo alichukua hatua gani kama Rais? Hivi Rais mzima anapowapa wezi kurudisha fedha walizoiba muda wa kuzirudisha na baada ya kuzirudisha mambo yakawa shwari kwa wezi ambao mpaka leo majina yao yako kapuni, unafikiri hiyo ni sahihi? You can fool people for sometimes but not always! By the way, hizo fedha zilizorudishwa na wezi, TSh 74bn/- zilifanyiwa nini? Si afadhali wezi wangeendelea kujinafasi nazo tukajua moja badala ya kutufanya mbumbumbu kiasi hicho? Oh, wake up, please!