Mh Kikwete Kuwa Mkweli, Usidhani Tumesahau! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Kikwete Kuwa Mkweli, Usidhani Tumesahau!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LordJustice1, May 13, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Juzi juzi Mheshimiwa Kikwete alifanya Semina Elekezi kwa Mawaziri wake na katika Semina hiyo alidai kwamba kila Wizara ina Msemaji wa wake na ni vizuri wawe wanajibu kila hoja inayotolewa dhidi yake.

  Alienda mbali kwa kusema kwamba uwongo ukiachwa kwa muda mrefu na kurudiwa mara kwa mara bila kujibiwa utageuzwa kuwa ukweli. Alidai pia kwamba kwa muda wa miaka mitano iliyopita Serikali ilikuwa haijibu hoja za Wapinzani na wananchi wamekuwa wakiwaamini kila wasemayo!


  Mpaka hapo sina tatizo na Mheshimiwa Kikwete!


  Hata hivyo, kama Kikwete anataka hoja zijibiwe aanze na hoja zilizoanzia wakati alipoingia madarakani mwaka 2005 na sio kujibu hoja za sasa akidhani kwamba hoja zilizopita tumezisahau! Kwa hiyo Mh Kikwete akitaka tumwelewe afanye yafuatayo:

  1. Akanushe kuhusu yeye kuitwa fisadi pale ilipotajwa List of Shame!

  2. Atoe maelezo kuhusu aliko Dr Balali.

  3. Aeleze juu ya wizi wa Meremeta na aache visingizio kwamba eti kuna SIRI ZA JESHI!

  4. Aeleze juu ya wizi wa fedha za EPA ambazo ndizo zilizomwingiza Ikulu!

  5. Aombe radhi Watanzania kwa kupitisha kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri Kampuni hewa ya Richmond ili kuja kukwapua fedha zetu!

  6. Aeleze ni kwa nini alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini alisaini mikataba tata ya IPTL na mingineyo inayotafuna uchumi wa nchi yetu mpaka sasa!

  7. Aeleze juu ya wizi wa kutupwa kupitia Makampuni ya Deep Green Finance, TanGold, Mwananchi Gold, Kagoda, nk ambao mpaka sasa hakuna majibu ya kueleweka!

  8. Aeleze jinsi Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ulivyonunuliwa kwa fedha za maandazi (70m/-) na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa!

  9. Aeleze jinsi alivyochakachua kura halali za Dr Willibrod Slaa na kuingia Ikulu kibabe kupitia Tume ISIYO HURU ya Uchaguzi!

  10. Aeleze zilipo TSh 74bn/- ambazo zilirudishwa na wezi wa EPA ambao hakuwataja hata majina baada ya kutolewa toka Benki ya TIB!

  11. n.k.


  Kikwete akijibu hoja hizo kwa ukamilifu atakuwa amefanya la maana na kama ni muungwana anatakiwa ajiuzulu ili awapishe watu wenye uchungu na nchi hii waingie Ikulu!
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Tunasikia balali katulia mahali fulani anakula bata,huwezi kuwa mwongo milele lazima mambo yatakuwa hadharani siku moja
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Aeleze kwa nini aliamua kuleta hoja ya udini kama kumpunguzia kura wakati ukweli anaujua ni wananchi kumchoka kwa sababu ya ufisadi (refer alipokuwa anamjibu Sofia simba -Raia mwema)
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi jamani babu seya bado yupo garezani?
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Yaani we acha tu, Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
   
 6. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bado mzee!
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  CCM=Mafia Mob
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,634
  Trophy Points: 280
  mpunguzie mzigo wa maelezo angalau aeleze alivyomkwepa Tajiri wa Richmond ambaye anadai hamjui sura, wala anakotoka wakati kaja mwenyewe huyu Mwarabu wa Zenj
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati mimi huwa najiuliza kama haya yote yanatokana na mtu kukosa shughuli za kufanya au ni nini? Kwa muelekeo huu pengine sasa napata picha ya namna tatizo la ajira lilivyo kubwa hapa nchini na ndiyo maana unaona watu wako busy kuunga unga maneno na kutafuta trivialities na kuziweka kwenye lensi na hatimaye kuzigusa. At times, mengi yanayoandikwa, kama hii thread ni irrelevancies. Rais amesema kwamba kila wizara iwe na wasemaje ambao watakuwa na jukumu la kujibu hoja mbalimbali na kutoa msimamo wa dhahiri kuhusu hoja mbalimbali zinazopandikizwa na watu ambao wana bifu lao. Sasa unajiuliza hayo yaliyozungumzwa yana uhusiano gani na upuuzi huu ulioandikwa wa kumtaka Rais akanushe kama hajatajwa kwenye list of shame. Hivi kuna ubishi gani kwamba kweli ametajwa? Kwani kutajwa na watu wasiomtakia mema, wazushi na watu ambao nia yao ni kuharibu jina lake ndiyo ukweli? Kwani nani hajui kwamba haya yanafanyika kwa nia mbaya na huyu mlipuaji wa mabomu hayo sasa hivi ni wakala wa mafisadi na sasa anatumika ku-confuse watu juu ya adui yao halisi? Je kwa kutajwa kwenye purported list of shame ndiyo kuna-invalidate vipi wito au agizo lake la kuwa na wasemaji wa wizara?

  Hizi fikra chanya na mtindio za kudhani kwamba lolote linalozungumzwa na Rais au na serikali basi ni baya kwa vile tu linakwenda kinyume na matakwa ya CDM au linabainisha uongo na uzushi wa CDM ni upuzi ambao hatutaukubali hata kama mtapiga kelele kwamba humu jamvini mmeingiliwa kwa sababu tu ya tofauti za mitazamo na fikra.
   
 10. b

  banyimwa Senior Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mbopo huachi kunifurahisha japokuwa umekuwa unaitwa kila jina la kejeli lakini kwa kweli upotoshaji humu JF umegeuka dili na hasa unapopotosha mambo kwa kuiua CCM. Mimi siiungi mkono CCM na kuna mengi yanayotia kichefuchefu ambayo ni lazima yaondolewe ili hiyo dhana ya kujivua gamba itimie. Lakini lililo wazi hapa ni kwamba wale wanaodhani wanaipigania CDM wamejikuta wanatetea mafisadi kwa kujua au kwa kutokujua. Lakini kinachoudhi ni kudhani kwamba huyo Dr. Slaa ndiyo muarobaini wa matatizo ya nchi hii wakati wote tunajua kwamba hata uendeshaji wa hicho chama unaacha maswali mengi sana na wakati ukifika tutayajua mengi.

  Unapodai uonyeshwe alipo Ballali ambaye ni marehemu ni uhitimu wa hali ya juu wa uhuja na ni kufikiria kwamba muovu hana haki ya kuonja umauti wakati hata Iddi Amin na mijizi na mijahili mingi imekufa. Ukisoma maswali hayo kumi utagundua kwamba ni marudio ya upuuzi ule ule ambao tumeusikia muda mrefu na ambao ufumbuzi wake hauko katika mfumo huo wanaouzungumzia hawa jamaa. Tukizungumzia watu waliofadika na EPA basi wataumbuka wengi ambao kila siku wanaonekana wakipanga foleni kwa mafisadi na wengine wakigeuka kuwa matarishi na vikaragosi vya kuwasemea na kuwatetea kwenye vikao vya kamati za bunge. Wakati muafaka ukifika watawekwa peupe halafu tuone kama wana moral authority ya kuzungumzia masuala ya ufisadi. Na ni vizuri watu wakajua EPA haijaanza 2005 na hata baadhi ya michango ya CDM kwenye kampeni zilizopita ni proceeds za EPA.
   
 11. m

  mudavadi Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi hakuna issue ya maana iliyoelezwa hapa.

  Kashfa zote za EPA, scandal ya Meremeta, Deed Green, Tangold, Mwananchi Gold, IPTL na Kiwira zilitokea kabla ya Kikwete hajawa Rais na hicho kinachoitwa IPTL ni mkataba ambao uliingiwa na Tanesco tena wakati huo ukiwa umeshapitiwa na Baraza la mawaziri. Wanaotaka ajibu maswali hayo wanachotaka kujua kutoka kwake badala ya kwenda kwa Mkapa ni nini? Hawa hawa kwa kushirikiana na Marando ndiyo sasa wanaodai wizi wa fedha za ununuzi wa nyumba ya ubalozi Italia ni wa kutungwa kwa nia ya kumkomoa Mahalu wakati wanajua kwamba huyu Profesa kaiba kweli na ushahidi uko bayana. Ndio sasa wako busy kutayarisha nyaraka za kushinikiza mashtaka yafutwe.

  Ukweli ni kwamba baadhi ya watu humu kama aliyepost thread hii ni watu waliovikwa kitambaa cheusi usoni na kukosa ufahamu wa jinsi viongozi wao walivyo na uhusika mkubwa katika yale wanayoyapiga vita.
   
 12. T

  Tiote Senior Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnahangaika bure na huyu jamaa. Hajui analolisema ndiyo maana anachanganya chumvi, sukari na pilipili. Anataka Ballali afufuliwe? Kweli akili ni nywele!
   
 13. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Anahusika na EPA 100%

  yeye na wanamtandao wake Akina RA CH* EL ndo vinara walio fanya master mind.

  Ndo maana kamwe hawezi kuwagusa kuwapeleka mahakamani.

  Kagoda mbona kimya mpaka leo?
   
 14. fige

  fige JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna siku tunweza kuja sikia Balali kafa mara ya pili sijui itakuwa picha kama ya The second chance
   
 15. p

  plawala JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo itakuwa ngumu rosemarie,ni sawa na kusema Osama bado anakula bata somewhere
   
 16. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haaaa haaa!
  JK najua kwamba ni mzee wa kujitoa! Kwa mfano:
  1. Alidai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini,
  2. Haijui kabisa Dowans,
  3. Hakuweka mambo ya Kadhi kwenye Ilani ya Uchaguzi, 2005 - 2010,
  4. nk
  Hata hivyo jambo lolote linalofanyika katika nchi hii linamhusu yeye espicially masuala ya EPA, Richmond, Dowans, Meremeta, TanGold, Deep Green Finance, Mwananchi Gold, Kagoda, nk kwa kuwa yananyonya uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa sana! Otherwise, yeye ni Rais wa nini sasa kama masuala makubwa yanayosibu uchumi wetu anayafumbia macho na badala yake kuongelea hofu yake ya kuondolewa Ikulu kwa nguvu ya umma?
  Vile vile suala la EPA alilisema mwenyewe Bungeni, kwamba wezi wanapewa miezi kadhaa kurudisha fedha ili zifunguliwe Akaunti katika Benki ya TIB! Hata hivyo fedha hizo TSh 74bn/- zilipopokelewa baadaye zilitolewa na kupelekwa kusikojulikana! Sasa hilo tukiuliza kuna dhambi gani wandugu?

  Na wewe Mbopo fungua macho ya ufahamu wako, toka usingizini, otherwise na wewe nadhani utakuwa beneficiary wa ufisadi, maana watu wawili (mafisadi na wewe) hawawezi kwenda njia moja wasipopatana!
   
 17. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiki nacho ni KIWAVI sema kina upeo kidogo tofauti na viwavi wengine, sema kimeharibu kusema eti Mkwèré kazushiwa kuwekwa kwenye list of shame, unadhani yeye anapenda kuzushiwa? Kama kazushiwa kwanini asiwapandishe kizimbani waliomzushia?! I need :ban: so that I can enjoy :majani7:
   
 18. fige

  fige JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hata mimi nashangaa, kwa nini Raisi wetu anasingiziwa sana, hebu fikiria haya mengine wanayomsingizia ;

  1.Eti Raisi amewahi sema Uraisi ni wa familia ?

  2.Wanasema Raisi amewahi kuwasamehe wezi wa fedha za EPA bila kuwapeleka mahakamani,je kweli hiyo ?
  3.wanasema eti Raisi hajui chanzo cha umasikini wetu,kwani ukiwa Rahisi lazima ujue kwa nini sisi unaotuongoza ni masikini ? Hayo ni baadhi tu anayosingiziwa ila yapo mengi sana
   
 19. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani Ballali alikufa?
   
 20. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  1. Akanushe kuhusu yeye kuitwa fisadi pale ilipotajwa List of Shame!

  2. Atoe maelezo kuhusu aliko Dr Balali.

  3. Aeleze juu ya wizi wa Meremeta na aache visingizio kwamba eti kuna SIRI ZA JESHI!

  4. Aeleze juu ya wizi wa fedha za EPA ambazo ndizo zilizomwingiza Ikulu!


  5. Aombe radhi Watanzania kwa kupitisha kupitia kikao cha Baraza la Mawaziri Kampuni hewa ya Richmond ili kuja kukwapua fedha zetu!

  6. Aeleze ni kwa nini alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini alisaini mikataba tata ya IPTL na mingineyo inayotafuna uchumi wa nchi yetu mpaka sasa!

  7. Aeleze juu ya wizi wa kutupwa kupitia Makampuni ya Deep Green Finance, TanGold, Mwananchi Gold, Kagoda, nk ambao mpaka sasa hakuna majibu ya kueleweka!


  8. Aeleze jinsi Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ulivyonunuliwa kwa fedha za maandazi (70m/-) na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa!

  9. Aeleze jinsi alivyochakachua kura halali za Dr Willibrod Slaa na kuingia Ikulu kibabe kupitia Tume ISIYO HURU ya Uchaguzi!

  10. Aeleze zilipo TSh 74bn/- ambazo zilirudishwa na wezi wa EPA ambao hakuwataja hata majina baada ya kutolewa toka Benki ya TIB!


  Wana mpunguzie maswali mpeni haya 5 ayajibu akufaulu ndiyo tumuongeze hayo mengine si unajua kuwa ana kazzi nyingi tusimtwishe zigo la maswali
   
Loading...