MPAMBANAJI.COM
JF-Expert Member
- Mar 2, 2011
- 712
- 332
Mimi kanifurahisha jinsi anavyokwenda na mahitaji ya wakati. anapotakiwa kuongea kwa utulivu anafanya hivyo. katika mikutano ya hadhara anaweza kuongea kwa sauti kali inayohamasisha na kusisimua. anaweza kujenga hoja polepole na kuacha nguvu ya hoja isimame. anaposhambuliwa kwa matusi bungeni, mfano kuna wakati nilimsikia mbunge mmoja wa CUF anamuita mcheza disko, anakuwa mtulivu na ku-ignore, with maximum impact. anajua wapi akae kimya, wapi atoe tamko. kila la heri kamanda!!
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa
Kwa kuongezea tu uliyoyasema,
Ni kamanda mbunifu wa matumizi ya ndege, ccm wakamzomea, mwisho nao wakalazima kuiga ubunifu wake.
Ni kamanda aliyeanzisha M4C arusha na sasa zinatikisa nchi nzima.
Ni kamanda wa aliyeanzisha sare za chama.
Kwa ujumla ubunifu wake ndio imekuwa nguzo muhimu kwa ukuaji wa chadema. Bravo.
Kwani sio mtu? Mbona yule wa Madagascar anaongoza nchi vizuri kuliko wengi wengine? Kila kitu na wakati wake!!
Andry Nirina Rajoelina (Malagasy: [ˈjandzʲ nʲˈrinə radzoˈel]), born May 30, 1974, is the President of the High Transitional Authority of Madagascar. He became president on March 21, 2009, during the 2009 Malagasy political crisis, after holding the office of Mayor of Antananarivo for one year prior. Before entering the political arena, Rajoelina launched several successful enterprises, most notably including a printing and advertising company called Injet in 1999 and the Viva radio and television networks in 2007. Over the course of his teens and early twenties, he gained popular recognition in Antananarivo as a DJ at local clubs and parties, and later for organizing and promoting musical events in the capital.
Kwa kuongezea tu uliyoyasema,
Ni kamanda mbunifu wa matumizi ya ndege, ccm wakamzomea, mwisho nao wakalazima kuiga ubunifu wake.
Ni kamanda aliyeanzisha M4C arusha na sasa zinatikisa nchi nzima.
Ni kamanda wa aliyeanzisha sare za chama.
Kwa ujumla ubunifu wake ndio imekuwa nguzo muhimu kwa ukuaji wa chadema. Bravo.
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa
Mhe Aweda,
Hakika umenena. CHADEMA kinaendelea kudhihirisha kuwa kina watu makini ambao kweli wako tayari kuchukua uongozi wa Taifa hili ambalo kwa kweli sasa limepoteza kabisa heshima na maadili ya kiuongozi.
Mhe.Freeman Mbowe amejizolea umaarufu kwa kujenga hoja zenye mashiko nje na ndani ya Bunge letu. Mhe. Mbowe amekuwa akitoa hoja ambazo ni makini na msumari kwa serikali ya Magamba. Sote ni mashahidi jinsi alivyokuwa anampiga maswali PM Pinda akawa anaishia kuyajibu kihunihuni na kiubabaishaji zaidi. Kama kawaida ya magamba Maswali magumu kwa majibu rahisi yaliyojaa kebehi na dharau kwa upinzani!
Watanzania wa sasa wamekuwa werevu,wasomi na wachambuzi wa maswala kwa hiyo wanajua kila kitu kinachoendelea nje na ndani ya Bunge. Nani anayezungumza pumba na utumbo Bungeni na nani anazungumza hoja zenye mashiko na kuleta tija kwa Watanzania bila ya kubagua kama wanavyofanya chama Twawala-CCM.
Kuna haja ya Watanzania wote kwa ujumla wao kuungana pamoja kwa umoja ili kuipa CHADEMA ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kinachoanzia 2015-2020. Kuna haja ya Watanzania kufanya mageuzi na mabadiliko ya lazima kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia katika mataifa ya wenzetu ambako kuna Demokrasia ya kweli. Hatuwezi kuongozwa na chama kimoja milele kama wanavyojidai CCM kana kwamba hii nchi ni yenye sera ya chama kimoja. Hili lisipewe nafasi katika Uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Kila lakheri CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.