Mh. Edward Ngoyayi Lowassa: Acha kucheza na akili za Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Edward Ngoyayi Lowassa: Acha kucheza na akili za Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Dec 7, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hakika mtu huyu amepania kuona kama anaweza kuwarubuni kwanza wanaCCM wenzake na hatimaye Watanzania ili awe Rais wa Nchi hii.Ninachukizwa sana na harakati zake za kutafuta uhalali wa kurudi ndani ya serikali akiwa Rais.

  Uko wapi usafi wa Lowassa, ikumbukwe kuwa hakuwahi kuelezea siri ya utajiri wake mbali na ule unaodaiwa kama wa kurithi kutoka kwa Mzee wake.Hivi kweli Lowassa anataka kutuhakikishia kuwa ni muadilifu na hajawahi kutuibia watanzania?.Umiliki wa majumba na mashamba pote hapa nchini amepata kihalali pasipo rushwa ama kutumia madaraka aliyokuwa nayo?

  Lowassa anapishana kabisa na falsafa ya Mwl. Nyerere kuwa anayekimbilia Ikulu "muogopeni kama ukoma".Mtu huyu alikuwa ametulia sana pamoja na purukushani za magazeti (Mwanahalisi & Tanzania Daima) dhidi yake.Kapita mgongo wa nyuma na sasa amekamata vyombo vya habari kama njia ya kujisafisha kwani sasa ndiye "role model" kuliko hata Rais wa Nchi,Pinda ama Mawaziri Wakuu Wastaafu (ambao hawakujiuzuru).

  Tunatambua kuwa Mh. Lowassa alikuwa na miadi na Kikwete kuwa baada yake U-rais utaangukia kwake.Haya ni mawazo na ulevi wa madaraka na kusahau demokrasia ya Wananchi kumchagua nani kuwa kiongozi wao.Hivi Lowassa anadhani wananchi wako nae ama ni WanaCCM (Makada wa Mikoa na Wilaya) wenye manufaa binafsi nae (kifedha na vyeo).Bila shaka anaemuunga mkono Lowassa nitakuwa na mashaka nae kwani huwezi kuwa mchapa kazi huku mwizi.Kazi ili iwe nzuri nimuhimu kuambatana na uadilifu na si "ujanja ujanja".

  Tazama bila aibu anajaribu kutoa utetezi kuwa "Mh. Mwenyekiti nilipokuletea jina la Rostam Aziz kama mtu wa kutusaidia kumpata Mwekezaji (Dowans/Richmond) ulikubali bila kusita".Hapa analaumiwa aliyemleta mwizi (Rostam) ama aliyemkubali mwizi?.Ni dhahiri Lowassa hakuwa mbali na Rostam katika "deal na ndio maana alimpendekeza Rostam kwa Kikwete na sio Mengi wala Said.

  Leo hii Lowassa karudi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa kwa gia ya "ajira kwa vijana ni bomu linalongoja kulipuka"!Itambulike kuwa kati ya shughuli anazozifanya Mkewe zimechangia kupunguza ajira za watu maofisini na kwinginepo.Mke wa Lowassa Bi. Regina ana kampuni ya usafi ambayo imekwapua ajira za watu maofisini kwa kigezo cha ku-outsource na hivyo kufanya vijana wengi ambao wangeweza kuwa ma-office attendants kutokupata ajira hizo, hivyo kubaki kuranda randa mitaani.Ni dhahiri kampuni hii ilikuwa kwa kasi na kupata tenda nyingi Serikalini kipindi ambacho Lowassa alikuwa Waziri MKuu.

  Ni nani asiyejua alifanya nini pindi akiwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, sehemu kubwa ya ardhi nzuri na majumba ya serikali yaligeuka vitega uchumi kwake.Leo Lowassa anatuaminisha nini?.Aihitaji utafiti mkubwa kujua Lowassa ni gamba na wala ulegelege wa Kikwete si sababu ya Lowassa kuwa SAFI.Watanzania hawakumuhitaji Lowassa kuwa Rais wala Waziri Mkuu hata kabla ya Kikwete.Uteuzi wa Lowassa kuwa Waziri Mkuu ulitokana na uswahiba kati yao wawili (hawakukutana barabarani) na si uchapa kazi,wengi hatukuupenda uteuzi huo japo tulijua lazima iwe hivyo.Vile vile wengi tulishangilia sana pindi alipotamka kujiuzuru, sasa leo umaarufu wake wa kupigiwa ama kujipigia chapuo kuwa Rais wa Nchi hii unatoka wapi? kwa TB JOSHUA (SCOAN).

  Lowassa ni Saratani na kimsingi anaombwa kuwaacha watanzania wafikiri nani wa kuwa Rais wao pindi muda muafaka utakapojiri na si vinginevyo.Kutafuta kujiuza kupitia vyombo vya habari tena kwa kutumia pesa ni kujaribu kutuudhi watanzania na isije ikawa ndiye chanzo cha uvunjifu wa amani katika nchi pindi tutakapochoka nae.Wapambe ama wafuasi wake wakubwa ni wenye njaa na tamaa ya madaraka na pilika zao zote si bure bali "quid pro quo".Ni dhahiri nchi yetu yenye watu zaidi ya milioni 45 haiwezi kumkosa kiongozi bora na muadilifu kuwa Rais eti ikamng'ang'ania Lowassa kuwa Rais.Mifano ya Kenya na Afrika Kusini kwetu haina nafasi kabisa kwani tunatofautiana katika mila na desturi pamoja na mafundisho (maadili).

  Nimeandika suala hili kutokana na kuona misururu ya magari na wapambe wengi kila siku hapa nyumbani kwake Mahando (Masaki) utadhani msiba au sherehe ya kifahari.Haiwezekani magari kujaza pande zote mbili za barabara pasipo sababu hasa baada ya kudai "amelipua bomu NEC Dodoma".Bila shaka amekwisha anza kampeni na wapambe wake ama wanafiki wanaomsaidia kucheza na akili za Watanzania.Nasema wanajidanganya kwani zama hizi si zile za chama kimoja.Lowassa atambue kuwa CCM wakimpitisha kwa (hongo na ombwe) Watanzania tuna pengi pa kuchagua na si yeye na chama chake.Maadam alijiuzuru (resigned) (sio kustaafu (retired)) lakini anapata heshima ya retired Prime Minister ashukuru Mungu kwani akituchafua ajue hata hiyo "illegal benefit " anayopata itageuka shubiri.
   
 2. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwaga moyo mkuu hapa ndo JF bana!
   
 3. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wanalipwa fedha nyingi kupromote ufisadi wake humu JF. Tena kaingia hadi makanaisani anahonga fedha za kufa mtu, hajui kuwa huwezi kumhonga Mungu!!!!!!!!!!!

  Ngoja Mungu huyo huyo amgeuke na ufisadi wake ataongelea kwenye pipa!!!!

   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Lowasa anafikiri watanzania wote ni wajinga kama yeye (imenukuliwa Mwl akimwambia Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa). Nashangaa mashairi ya kumtukuza yanajazwa humu.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kuona Edward Lowassa akiteseka kama wakati huu. Analala na vikaratasi vya speech huku na kule na simu za waandishi wa habari na maaskofu ili kutafuta jukwaa la kujijenga. Bahati mbaya sana watanzania wa leo hawapumbaziki kirahisi. Kufika 2015 atakuwa amechakaa na koo kumkauka na bado tutamuadhibu kwa kumnyima kura!
   
 6. ram

  ram JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Anatumia mgogo wa vijana kuingilia ikulu, kila anapofanyiwa mahojiano au anapotoa hotuba lazima aseme "ajira kwa vijana ni bomu linalongoja kulipuka" yeye alifanya nini kuwasaidia vijana akiwa waziri na hatimaye waziri mkuu?
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ndani ya CCM na nje ya CCM hakuna M-TZ wa kupambana na EL.
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa anaelekea kubaya sana....
   
 9. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  masikini wa hii nchi mnawivu sana badala yakuhangaika kujikwamua mnakaa kushutumu watu bila uthibitsho
   
 10. M

  Manyema JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  wacha kujidanganya wewe ni mtu mzima, aliyekwambia hakuna mtu wa kupambana naye ni nani? angekuwa anahangaika hivyo kila siku kubwabwaja bwabwaja hovyo " ajira kwa vijana ajira kwa vijana" yeye alipokuwa waziri mkuu alifanya nn kuhakikisha vijana wanapata ajira. Shame on u......puuuuuuuuuuuuuu atoke hapa na ufisadi wake.
   
 11. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Kwa watanzania wa kawaida Lowassa ni tatizo dogo sana. Ufisadi wa Lowassa ni subset ndogo tu ya ufisadi wa chama chake. Na kama chama chake kikimpitisha kuwa mgombea urais halitakuwa jambo la kushtusha hata kidogo. Atakuwa amepitishwa na wajumbe walio wengi wa NEC ya chama chake ambao kwetu hakitishangazi maana nao ni mafisadi. Chama kimejaa mafisadi, na wale wanaojiita wasafi wanafahamu kuwa si wasafi na Lowassa analijua hilo. Kama wanabisha wajaribu kumfukuza waone. Nilimcheki jana Lowassa TBC akiulizwa swali kuhusu uwajibikaji wa viongozi wasio na maadili serikalini. Na jibu lake lilikuwa fupi tu lakini la kweli. Kwamba, waige mfano wake maana yeye aliwajibika kwa kiwango cha uwaziri mkuu alipotuhumiwa kukosa maadili. Sasa maadui wake wanamtafuta nini tena? Kama wanamwona ni fisadi wanashindwa vipi kumfikisha mahakamani?
   
 12. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nimetokea 'kuvutiwa' na EL kwa sababu licha ya kuwa anatuhumiwa ni Fisadi lakini ni mchapakazi. Mkapa aliingia Ikulu sio Fisadi na akatoka Fisadi( hakuna ubishi) .......JK nae kaingia 'FISADI' tena kwa kura nyingi na si mchapakazi kuna uwezekano mkubwa akatoka na 'FISADI' wa kupindukia. Kuna uwezekano 'Mkubwa' EL akaingia ni 'FISADI' na akatoka kama alivyoingia au akaongeza kidogo tu ka 'UFISADI'. NI mawazo tu.

  'NIMEZALIWA CDM NITAFIA CDM'
   
 13. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unataka uthibitisho gani?
  Mbona hakukanusha Richmond akakubali kwa kujiuzuru kuliko kukanusha maana angepelekewa ushahidi ambao ungempeleka jera!
  Hana mpya Fisadi papa huyo!

  Na nilazima ajadiliwe kwa mstakali wa Taifa maana amepania sana na campaign amezianza mapemaa!
   
 14. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna kama Hon Luteni Edward Ngoyai Lowassa ndani ya ccm.Nitajie mmojawapo.wote mafisadi afadhali Huyu.
   
 15. t

  think BIG JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  chuki binafsi!
  Kwa mtazamo wako, inamaana hata Microsoft alaaniwe kwa kuua ajira za vijana wengi ma-messenger na ma-typist! Na Yahoo/GMail walaaniwe kwa kuua ajira za vijana wetu kule Posta na Simu!

  Kwa mtazamo huu, sioni wa kumgusa Lowassa (ndani ya CCM), maana kila mara wimbo ni ule ule "Richmond", "ni Fisadi", "Nyerere alisema ana mali nyingi", ....
   
 16. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Jamani usihukumu bila uthibitisho wowote, hayo majumba na mashamba yako wapi acha uwongo na kufata mkumbo. Mimi Mtanzania siwezi kupandikizwa chuki binafsi na hukumu kwa mtu bila uthibitisho wowote huko ni kujitafutia dhambi na hukumu kijinga. Kama ni kweli kwanini usitoe huo uthibitisho wa majumba na mashamba kama unavyo. Huyo EL ninayajua maisha yake na familia yake, na sijauona huo utajiri unaosema anao. Mke wake masikini na kikampuni chake cha usafi nae unamuhukumu, mbona mjomba wangu anayo kampuni ya usafi na inapata kazi kuliko hicho cha Mke wa EL. Kuanzishwa kwa kampuni za usafi, kunaetwa na serikali na makampuni kuamua kubinafsisha baadhia ya kazi ambazo wanaona wanashindwa kuzifanya kwa ufanisi, sio unaamua kuwalaumu watu kwa kupoteza ajira za watu. Wewe kwa mawazo yako, huoni kwamba hizo kampuni za usafi zinatoa ajira kwa watu wengi kuliko zisinge kuwepo. EL hana utajiri wowote ukipenda waulize matajiri wa nchi hii kama kina Mengi, Baharesa, Manji, Pateli n.k, watakuambia mwacheni huyo bwana mdogo hana lolote ana hela ya kuishi. Wengine hawampendi EL kwasababu ya ukali, kwamfano swala la Jairo ingekuwa ni yeye Waziri Mkuu ndiyo ungemjua vizuri EL. Jamani madini yanaendelea kuibiwa yanapelekwa nje, ardhi nzuri inapewa makaburu kwa kutumia jina la uwekezaji, wananchi wananyang'anywa hamuoni na kuandika, mnakalia kutoa shutuma feki tu kwa EL kama mwanamke mwenye gubu. Kitu cha ajabu ni kwamba wengi wanaomuhukumu EL ni kutoka chama chake, inaonekana kampeni zitakuwa kali kama ataamua kugombe. Wasiwasi ni mkubwa kweli ndani ya chama chake lakini si ajabu wala hana mpango wa kugombe uongozi. USIHUKUMU, USIJE KUHUKUMIWA.
   
 17. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  wewe!!!!!
   
 18. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  TOA UTHIBITISHO wa watu waliolipwa fedha nyingi kupromote ufisadi wa EL kama upo humu JF. Vinginevyo tunaomba ufungiwe maisha kwa kutuhumu watu uongo.
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Nafikiri Lowassa ana watu ambao akiwaambia shikeni ukuta basi mara moja watashika, acheni upuuzi wenu na baba yenu Lowassa atuambie kwanza je alifanya nini wakati akiwa ndani ya serikali wakati ule, aseme kwa nini utetezi wake unakuja baada ya kutia inchi hasara ? pia atoe majibu yanayojitosheleza kwa utajiri wake, vingenevyo mchukueni Lowassa mkanywe naye Kahawa Buguruni kwa malapa,

  Nyerere alishasema mkimwona mtu anakimbilia ikulu basi muogopeni kama Ukoma

   
 20. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kudadadekiii nitashika mtutu akiwa raisi huyu FISADI
   
Loading...