Mh. Edward Ngoyayi Lowassa: Acha kucheza na akili za Watanzania

Hakika mtu huyu amepania kuona kama anaweza kuwarubuni kwanza wanaCCM wenzake na hatimaye Watanzania ili awe Rais wa Nchi hii.Ninachukizwa sana na harakati zake za kutafuta uhalali wa kurudi ndani ya serikali akiwa Rais.

Uko wapi usafi wa Lowassa, ikumbukwe kuwa hakuwahi kuelezea siri ya utajiri wake mbali na ule unaodaiwa kama wa kurithi kutoka kwa Mzee wake.Hivi kweli Lowassa anataka kutuhakikishia kuwa ni muadilifu na hajawahi kutuibia watanzania?.Umiliki wa majumba na mashamba pote hapa nchini amepata kihalali pasipo rushwa ama kutumia madaraka aliyokuwa nayo?

Lowassa anapishana kabisa na falsafa ya Mwl. Nyerere kuwa anayekimbilia Ikulu "muogopeni kama ukoma".Mtu huyu alikuwa ametulia sana pamoja na purukushani za magazeti (Mwanahalisi & Tanzania Daima) dhidi yake.Kapita mgongo wa nyuma na sasa amekamata vyombo vya habari kama njia ya kujisafisha kwani sasa ndiye "role model" kuliko hata Rais wa Nchi,Pinda ama Mawaziri Wakuu Wastaafu (ambao hawakujiuzuru).

Tunatambua kuwa Mh. Lowassa alikuwa na miadi na Kikwete kuwa baada yake U-rais utaangukia kwake.Haya ni mawazo na ulevi wa madaraka na kusahau demokrasia ya Wananchi kumchagua nani kuwa kiongozi wao.Hivi Lowassa anadhani wananchi wako nae ama ni WanaCCM (Makada wa Mikoa na Wilaya) wenye manufaa binafsi nae (kifedha na vyeo).Bila shaka anaemuunga mkono Lowassa nitakuwa na mashaka nae kwani huwezi kuwa mchapa kazi huku mwizi.Kazi ili iwe nzuri nimuhimu kuambatana na uadilifu na si "ujanja ujanja".

Tazama bila aibu anajaribu kutoa utetezi kuwa "Mh. Mwenyekiti nilipokuletea jina la Rostam Aziz kama mtu wa kutusaidia kumpata Mwekezaji (Dowans/Richmond) ulikubali bila kusita".Hapa analaumiwa aliyemleta mwizi (Rostam) ama aliyemkubali mwizi?.Ni dhahiri Lowassa hakuwa mbali na Rostam katika "deal na ndio maana alimpendekeza Rostam kwa Kikwete na sio Mengi wala Said.

Leo hii Lowassa karudi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa kwa gia ya "ajira kwa vijana ni bomu linalongoja kulipuka"!Itambulike kuwa kati ya shughuli anazozifanya Mkewe zimechangia kupunguza ajira za watu maofisini na kwinginepo.Mke wa Lowassa Bi. Regina ana kampuni ya usafi ambayo imekwapua ajira za watu maofisini kwa kigezo cha ku-outsource na hivyo kufanya vijana wengi ambao wangeweza kuwa ma-office attendants kutokupata ajira hizo, hivyo kubaki kuranda randa mitaani.Ni dhahiri kampuni hii ilikuwa kwa kasi na kupata tenda nyingi Serikalini kipindi ambacho Lowassa alikuwa Waziri MKuu.

Ni nani asiyejua alifanya nini pindi akiwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, sehemu kubwa ya ardhi nzuri na majumba ya serikali yaligeuka vitega uchumi kwake.Leo Lowassa anatuaminisha nini?.Aihitaji utafiti mkubwa kujua Lowassa ni gamba na wala ulegelege wa Kikwete si sababu ya Lowassa kuwa SAFI.Watanzania hawakumuhitaji Lowassa kuwa Rais wala Waziri Mkuu hata kabla ya Kikwete.Uteuzi wa Lowassa kuwa Waziri Mkuu ulitokana na uswahiba kati yao wawili (hawakukutana barabarani) na si uchapa kazi,wengi hatukuupenda uteuzi huo japo tulijua lazima iwe hivyo.Vile vile wengi tulishangilia sana pindi alipotamka kujiuzuru, sasa leo umaarufu wake wa kupigiwa ama kujipigia chapuo kuwa Rais wa Nchi hii unatoka wapi? kwa TB JOSHUA (SCOAN).

Lowassa ni Saratani na kimsingi anaombwa kuwaacha watanzania wafikiri nani wa kuwa Rais wao pindi muda muafaka utakapojiri na si vinginevyo.Kutafuta kujiuza kupitia vyombo vya habari tena kwa kutumia pesa ni kujaribu kutuudhi watanzania na isije ikawa ndiye chanzo cha uvunjifu wa amani katika nchi pindi tutakapochoka nae.Wapambe ama wafuasi wake wakubwa ni wenye njaa na tamaa ya madaraka na pilika zao zote si bure bali "quid pro quo".Ni dhahiri nchi yetu yenye watu zaidi ya milioni 45 haiwezi kumkosa kiongozi bora na muadilifu kuwa Rais eti ikamng'ang'ania Lowassa kuwa Rais.Mifano ya Kenya na Afrika Kusini kwetu haina nafasi kabisa kwani tunatofautiana katika mila na desturi pamoja na mafundisho (maadili).

Nimeandika suala hili kutokana na kuona misururu ya magari na wapambe wengi kila siku hapa nyumbani kwake Mahando (Masaki) utadhani msiba au sherehe ya kifahari.Haiwezekani magari kujaza pande zote mbili za barabara pasipo sababu hasa baada ya kudai "amelipua bomu NEC Dodoma".Bila shaka amekwisha anza kampeni na wapambe wake ama wanafiki wanaomsaidia kucheza na akili za Watanzania.Nasema wanajidanganya kwani zama hizi si zile za chama kimoja.Lowassa atambue kuwa CCM wakimpitisha kwa (hongo na ombwe) Watanzania tuna pengi pa kuchagua na si yeye na chama chake.Maadam alijiuzuru (resigned) (sio kustaafu (retired)) lakini anapata heshima ya retired Prime Minister ashukuru Mungu kwani akituchafua ajue hata hiyo "illegal benefit " anayopata itageuka shubiri.

pambaf... Mod futa upupu na unafki... Mnafki mkubwa wewe.. Si kamati kuu ya chama mlikuwa na vikao ddm, mlishindwa nini kumwajibisha... Maji ya shingo sasa, unakuja jf kutafuta huruma ya watz... Hamna hata mmoja aliye msafi ndani ya CCM, kama mnaweza mfukuzeni..
 
Alimwambia mwenyekiti JK hivi:kuna jambo ambalo nimelifanya kuhusiana na richmond ambalo wewe hukulijua?

mwenyekiti JK hakuwa na jibu

Kwa hiyo wote walihusika ila kwa mujibu wa EL yeye alijiuzulu kwa heshima ya serikali na CCM

Je anaweza kuwa msafi tu kwa sababu walihusika wengi? jibu ni hapana
 
chuki binafsi!kwa mtazamo wako, inamaana hata microsoft alaaniwe kwa kuua ajira za vijana wengi ma-messenger na ma-typist! Na yahoo/gmail walaaniwe kwa kuua ajira za vijana wetu kule posta na simu! Kwa mtazamo huu, sioni wa kumgusa lowassa (ndani ya ccm), maana kila mara wimbo ni ule ule "richmond", "ni fisadi", "nyerere alisema ana mali nyingi", ....
wewe utakuwa auelewi, yanini kung'ang'ania ajira za vijana wakati ameshiriki kuangusha ajira za vijana dat's point, kwan bill gate nae anapita akihubili ajira?? Acha hizo wewe, nyie ni vikaragosi tu izo mia mia mnazopewa za ufisadi zinawavuruga vichwa,in short nalaumu sana misikiti pia makanisa aliowaona easy kupitia kujisafisha, tafadhali huko ni paala patakatifu tunapaheshimu uko jamani, msitumiwe na hili fisadi kujisafishia, jamani ata kama ni njaa paheshimuni huko msikaribishe mafisadi kuwamwagieni pesa walizoiba bado hizo ni haramu, fisadi lowasa anatumia misikti pia makanisa kuosha ela zake chafu alizokwapua serikalini, chonde chonde sie wahumini hatupendezwi na tabia za fisadi lowasa katika makanisa pia misikitiki. Tafadhali tumuogope mungu muumba
 
........napata shida na wanaoteseka na ama Lowassa au kivuli chake, kama hajaweka nia yake wazi kwa nini msimpuuze mpaka hapo atakapofanya hivyo? Naamini wapo wengi ambao aidha wana nia kama ya Lowassa (kama anayo) ama inayofanana na ya Lowassa, wawekeni wazi na hao (naamini wapo, mojawapo Membe), tuwachambue pia. kama kweli Lowassa hana mashiko kivile, mpuuzeni, subirini wakati ufike (kama utakuwa upande wetu), watajitokeza na wengine naamini wenye magamba pia, suala litakuwa ni kulinganisha ugumu wa magamba yenyewe, acheni kuteseka na kivuli cha Lowassa kwa anaowapa shida;
 
TOA UTHIBITISHO wa watu waliolipwa fedha nyingi kupromote ufisadi wa EL kama upo humu JF. Vinginevyo tunaomba ufungiwe maisha kwa kutuhumu watu uongo.

jamaa yako aliwagalamia wamasai wote tz wafike arusha hili wakamtakase unayo habari ?
 
pambaf... Mod futa upupu na unafki... Mnafki mkubwa wewe.. Si kamati kuu ya chama mlikuwa na vikao ddm, mlishindwa nini kumwajibisha... Maji ya shingo sasa, unakuja jf kutafuta huruma ya watz... Hamna hata mmoja aliye msafi ndani ya CCM,

kama mnaweza mfukuzeni..

Hongo mbaya sana maake humfanya mtu kuwa kama ''pepo'' mchafu popote aelekezwapo huenda.
 
Nadhani watu tunajua ya kuwa ni ushabiki na chuki binafsi za akina Sita, Ninauye, Membe, Kikwete, Nyalandu na wengine wengi ambao wamezijenga kwa Lowassa. Na pia tukubali ya kuwa uwezo wa Lowassa kikazi unawapa taabu hawa jamaa. Yupi kati ya hawa ni msafi? Membe ambaye amechukua pesa kutoka kwa Quaddafi ili kujikuza kisiasa hapa Tanzania, Sitta ambaye anasafarisha magogo nje ya Tanzania, Kikwete ambaye anachakachua nchi kupitia kijana wake Ridhwani? Nyalandu ambaye amejenga jumba kwenye kiwanja kichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa dispensari? Yupi anaweza kumtupia mawe akisema mikono yake ni ya haki? Nadhani baadhi ya watanzania tumekuwa wanafiki sana, chuki hii kwa Lowassa imeanza kufifia na hakuna mwaka mmoja zaidi wimbo huu wa kumchafua Lowassa utakuwa unakubalika tena na watanzania. Yaliyopagwa na mungu binadamu hawezi kutegua, kama Mungu anataka Lowasa kuwa rais wa nchi hii atakuwa, wala siyo hao wenye kuvaa ngozi ya kondoo wakipita wakisema huyu hafai, huyu hivi, yule vile, kama ni fisadi toeni ushahidi. Msije mkakuta mnatoa hukumu pasipo haki....Msihukumu msije mkahukumiwa kwa kukosa kiongozi thabiti...Msidanganyike na hawa wenye hila binafsi akina Sitta, Membe na kundi lake?
 
Lowassa anacheza na akili ya wana CCM wenzake na anajua namna ya kucheza na akili yao kwa kuwa alishacheza mchezo kama huo wakati akipiga debe la JK.

Mfumo wa CCM ndio ambao unamruhusu Lowassa kucheza na akili ya wana CCM na pia wanaompinga wote wakiingia kwenye vikao hawasemi, ila wakienda kwenye magazeti na kwenye redio mbao wanapaisha sauti haswa. Je, ni kwanini wanamuogopa?

Tatizo lolote lile namna ya kulitatua ni kuhakikisha unakwenda kwenye kiini chake, bila kufanya hivyo utaishia kuhangaika na same problem siku zote. Kinachowahangaisha wana CCM na uongozi wao ni kwamba ni wanafiki au hawataki kukubali ukweli.

Mzee Mukama aliongoza kamati iliyochunguza kwanini CCM kwenye uchaguzi uliopita ilifanya vibaya? Katika findings za kamati hiyo, baadhi zilikuwa sahihi na nyingine zilikuwa ni uongo, kubuni au hisia.

Hoja ya ufisadi ilikuwa na ukweli, lakini tatizo la ufisadi ni mfumo mzima wa serikali ya kifisadi, kishikaji na kulindana ndio iliyofanya wananchi wakapoteza imani na CCM au serikali ya CCM. Kuna ufisadi mwingi sana ambao umefanyika, ushahidi upo lakini serikali hiyo hiyo inapeleka kesi kishikaji kama ushahidi wa kupiga vita ufisadi lakini haina dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi. Bado CCM hiyo hiyo iliteua wagombea ambao walikuwa na tuhuma za ufisadi na ikawapigia debe kwamba hata kesi zilizoko mahakamani ni ndogo so wangeshinda tu. Mkapa mmoja wa wajumbe wa CC na NEC, anajua wazi kashfa ya Kiwira ilikuwa na ushahidi wa wazi, ikija hoja ya ufisadi unategemea atafungua mdomo kukemea kwa nguvu zote?

Hoja nyingine ilikuwa ni mfumo wa uchaguzi wa ndani wa CCM ambao unatoa nafasi kwa wenye fedha kuweza kupanga safu ya uongozi. Hoja hii ina ukweli, lakini hata mfumo mwingine ukija kama Azimio la Zanzibar bado liko hai bila miiko ya uongozi na bila kutenganisha biashara na siasa, bado wenye nazo wataendelea kuitesa CCM maana hata wajumbe wa mikutano ya huko chini wanajua kwamba wakati wa uchaguzi ndio kipindi cha kupata rushwa japo ya shilingi alfu kumi. Kwa hiyo akitokea mgombea mwenye nazo bado atawahonga wapiga kura. Kwa hiyo hapa sio swala la kubadilisha mfumo wa uchaguzi wa wajumbe wa NEC bali ni swala la kurudi kwenye kiini ambacho ni kurekebisha Azimio la Zanzibar na kurudisha miiko ya Uongozi.

Mukama na kamati yake walisingizia kwamba JF na mitandao mingine inatumika kukipaka matope chama, lakini ufisadi uliokuwa unaongelewa hapa ni huo huo ambao serikali inaujua na ndio huo huo ambao CCM imekubali kwamba kuna mafisadi ndani ya chama. Chama kinapotoa a blanket statement kwamba wajipime na kujitafakari then wachukue hatua bila ya kuwataja, ni dalili ya kwamba watu wanaogopana au wana waogopa mafisadi.

Baada ya hiyo report kujadiliwa ndipo Mukama akapewa utendaji ukuu wa CCM [Katibu Mkuu] ili atekeleze yale aliyoyaona wakati Kamati yake ikifanya uchunguzi. Mpaka sasa sijaona lolote la maana lililofanyika zaidi ya sarakasi na kubadilisha statement kila kukicha. Kwa ujumla ni kwamba serikali na CCM hawana dhamira ya dhati ya kupiga vita ufisadi. Uongozi wa Chama unawagwaya mafisadi, ndio maana wanahangaika kutafuta njia muafaka ya kuwaondoa ambayo sioni kama kuna dalili za kupatikana.

Mfumo mzima wa CCM una matatizo na ndio maana wanayumba katika kufanya maamuzi. EL atawayumbisha sana kwa kuwa hatakubali kuondoka kirahisi. Wapinzani wakae mkao wa kula maana vyovyote itakavyokuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuvuna.
 
Lowassa anajichezea ingawa anaamini anawachezea watanzania. Siku ikifika atajua ukweli mchungu ingawa itakuwa too late for such a kicking ass so to speak.
 
Watanzania tunataka mtu wa kututoa hapa tulipokwama, kama EL anaweza hilo apewe.. swala la ufisadi ninalitazama kwa mtazamo tofauti kidogo. Mwaka 1995 Nyere alituletea mr clean na kwakweli alikuwa clean lakini katoka hafai, uchafu mwili mzima. 2005 akaja mkware hakuwa na kitu lakini sasa ni balaa (kijiji chake pale lugoba tu kwanza kinatisha, hizo biashara za R1 nk) wizi unafanyika kazi zimelala. Kwa mtazamo huo ni kwamba tunaweza kumweka mwana ccm mwingine madarakani ikawa hivyo kila mara, kibovu ni mfumo mzima wa ccm na katiba ya nchi yetu.

Kama tuna uchungu na nchi hii hatuna budi kuiondoa ccm madarakani na pia kubadili katiba tuliyonayo

Ufisadi ni mfumo lakini haimaanishi tumweke poster boy wa ufisadi kuwa Rais wa jamhuri...NO NO NO
 
Upuuzi mtupu. Yote uliyoandika ni kama riwaya ya kubuni. Umetumia muda mwingi kuandika bila kuthibitisha madai yako. Tumesubiri idara zinazohusika zichukue hatu dhidi ya tuhuma zake mpaka leo hakuna kinachoendelea. Kumbe tatizo ni utajiri, hata wewe hukatazwi kuwa tajiri. Mtapiga sana kelele lakini mwisho wa ubaya ni aibu. Utajiri wa Lowassa wa kawaida sana kama wanasiasa wengine tofauti na unavyofikiri. Kwani wale wa upande wa pili wenye kumudu kumiliki hadi helkopta wao pesa wamekwiba wapi. Majungu hayajengi.
Kutochukua hatua kwa idara za usalama na sheria haina maana kuwa EL ni msafi. Hii ni katika kulindana kama ilivo kawaida ccm.wote wachafu wa kumnyooshea kidole mwingine nani? EL namwomba Mungu ccm wafanye kosa kumteua kuwa mgombea wao 2015 ili iwe talaka ya kuiaga hiki chama cha mafisadi kinachowafuga wezi kama EL, JK, Samwel Sita, Magufuli, EC , Rostam na wengine.
 
Nadhani watu tunajua ya kuwa ni ushabiki na chuki binafsi za akina Sita, Ninauye, Membe, Kikwete, Nyalandu na wengine wengi ambao wamezijenga kwa Lowassa. Na pia tukubali ya kuwa uwezo wa Lowassa kikazi unawapa taabu hawa jamaa. Yupi kati ya hawa ni msafi? Membe ambaye amechukua pesa kutoka kwa Quaddafi ili kujikuza kisiasa hapa Tanzania, Sitta ambaye anasafarisha magogo nje ya Tanzania, Kikwete ambaye anachakachua nchi kupitia kijana wake Ridhwani? Nyalandu ambaye amejenga jumba kwenye kiwanja kichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa dispensari? Yupi anaweza kumtupia mawe akisema mikono yake ni ya haki? Nadhani baadhi ya watanzania tumekuwa wanafiki sana, chuki hii kwa Lowassa imeanza kufifia na hakuna mwaka mmoja zaidi wimbo huu wa kumchafua Lowassa utakuwa unakubalika tena na watanzania. Yaliyopagwa na mungu binadamu hawezi kutegua, kama Mungu anataka Lowasa kuwa rais wa nchi hii atakuwa, wala siyo hao wenye kuvaa ngozi ya kondoo wakipita wakisema huyu hafai, huyu hivi, yule vile, kama ni fisadi toeni ushahidi. Msije mkakuta mnatoa hukumu pasipo haki....Msihukumu msije mkahukumiwa kwa kukosa kiongozi thabiti...Msidanganyike na
hawa wenye hila binafsi akina Sitta, Membe
na kundi lake?
Wote uliowataja akiwemo EL wezi. Akili zenu za ccm pelekeni hukohuko kwenu. Hata mkisema fulani mwizi kidogo naye ni mwizi tu. We want clean person n clean system. that will never come from ccm.
 
Back
Top Bottom