Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamii01, Jan 12, 2012.

 1. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Najiuliza na kukosa majibu Mh. Lowassa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge, nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa. Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?

  Je, alikwisha tangaza mali zake hadharani? Na kipato chake kiko vipi? Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo? Na alipokuwa Waziri Mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwanini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?

  ===============
  Utetezi wa Lowassa:
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Lowassa ni Tajiri sana hata kabla hajawa waziri mkubwa. Nitashangaa kama tajiri anaulizwa kuwa pesa anatoa wapi. Tatizo la Lowassa na baadhi ya viongozi wengine matajiri ni pale wanaposhindwa ku declare interests zao in time. EL anamiliki ma estate nyingi hapa Arusha, ana Shares kubwa kwenye makampuni ya utalii kama vile Leopard nk.
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  kundi genge nyuma yake linajiita "friends of lowassa" ndio linalowezesha hayo mamilioni ya lowassa makanisani,cha kujiuliza kama kweli Lowassa ana nia ya kugombea urais then (mungu apishie mbali)akaupata,hawa jamaa atawalipa vipi?atafanya biashara gani pale ikulu itakayomuwezesha kuwalipa hawa marafiki zake????
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  swali ngumu majibu mepesiii...hiii ndio bongo tambarare
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,194
  Trophy Points: 280
  Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.

  Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.

  Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.

  Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.

  Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.

  Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.

  Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,194
  Trophy Points: 280
  Mungi, asante kwa hili, Lowassa ni mkweli!. Umiliki wake ni halali ndio maana anatumia majina yake!. Kule CCM kuna mijizi kibao iliyokwapua mali ya umma na kujimilikisha kwa kutumia majina ya ndugu na jamaa zao hivyo Lowassa kuonekana kama ndio fisadi!.

  CCM kuna vifisadi, mafisadi na mifisadi!. Kati ya wote hao, Lowassa ndio mtakatifu wao pekee atakayeikomboa Tanzania na ule "ukombozi wa pili"!.
   
 7. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aisee, nimekumbuka sredi moja ya MS ulipokiri kuwa weye u-mutu ya bahasha bin mishiko!!! teh teh.................... aisee, kweli hapa mujini, kila mutu itie akili yake kumukichwa!!!!....................... but, jamani, mbona 2015 bado mbali???....................... tutafika kweli???.........................
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,152
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Lowassa ni Tajiri sana----ALPHA
   
 10. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Most of the Tanzanians can not wait to see this happen.
  By the way, why EL Ikulu? Kwani hakuna watu wengine? kwani asipopata huo urais itakuwaje?
  Kama ni mtu safi hakuna haja ya kumsafisha, hana haja ya kutafuta symphy ya makanisa. Akae Kimya then CCM will pick him.
  Kama ni mtu safi kama unavyosema, kwa nini hakuwa na guts za kumjibu Nyerere?
  Mind you, EL alirudi kwenye cabinet badala ya kumpeka JKM kwenye safari yake ya Mwisho kule Butiama.
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Wana JF, kwa nini watu hawatilii mashaka utajilli wa BAKHRESA, DEWJI, na kila kukicha wanazungumzia wa Lowassa? hao wengine, hata kama waliongeza utajili kwa njia nyingine, basi chanzo chao kinaeleweka. Hivi Baba yake Lowasaa alikuwa mfanya biashara wa nini vile? Naomba mnikumbushe.

  Hivi mnakumbuka nani vile aliagiza zile LAND CRUISERS (za mara ya kwanza, (yaliyokuwa yanaitwa mashangingi ya wabunge) kwa wabunge wote)???? Kumbukeni kwamba wakati ule serikali iliknunua magari na kwuakopesha wabunge, kabla ya hapo walikopeshwa LAND ROVER 110.
  Ni kiongozi gari alisimamia hili deal? Ile 10% ilikwenda wapi? Imagine 10% of all the Land cruisers???

  Wakati ule Lowasa alikuwa ana madaraka gani kule kwenye ofisi waziri Mkuu?

  Hiii inaweza kusadia kuelezea, kwa kiasi fulani, utajili wa ajabu kwa mtu ambaye almost maisha yake yote amekuwa mfanyakazi wa serikali.
   
 12. P

  PATALI Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unapumuliwa kisogoni ww kanjanja njaa!!!
   
 13. e

  enoah JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Mie sio shabiki wa El ila napenda ukweli mbona watu huwa wanasema tu Nyerere alimwambia hizo mali ulizipata wapi hawamalizii yote mengine,labda niwakumbushe swali hilo aliulizwa baada ya kukodi ndege wakati wa uchaguzi 1995 na mtu wa kwanza kuulizwa mmekodi ndege mmepata wapi hela alikuwa Jk akasema sio mimi mwl ni El ndio akamwambia El hivi utajiri wako hauendani na umri ulionao na kazi ufanyazo japo kweli baba yako alikuwa tajiri sana wa ng'ombe yawezekana ni urithi lakin haiwezi kukufikisha kwenye utajiri huu kiongozi anaetumia mali kuingia ikulu hatufai, tofauti ya El na mwalimu haikuanzia hapo bali tangia huko nyuma kuna wakati mwalimu alimuomba awe katibu wa Ccm akakataa. El ni tajiri sana na utajiri wake haukuanza juzi tangia kwa baba yake amekuwa akiuendeleza tu japo inaweza ikawa kachanganya na za ufisadi kwani Ccm hakuna ambaye sio fisadi,El ni bora mara 300 ya JK
   
 14. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ndani ya CCM, Lowassa namlinganisha na Messi wa Barcelona! Mimi sijali kama ni fisadi ama siyo fisadi. Ninaangalia uchapa kazi wake na umahiri wake wa uongozi. Huyu jamaa angeendelea kuwa PM naamini CDM tungekuwa ktk wakati mgumu 2015 kuingia Magogoni.
   
 15. samito

  samito JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  imani yangu kuhusu ENL inazidi kushuka kwa kasi, alikua poa sana lakini tangu ajeruhiwe amekuwa mpole na mnyenyekevu ili kutafuta upenyo wa kulipiza kisasi. sijui akishika hatamu itakuaje.
   
 16. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Kama Lowassa ni msafi

  1.Kwa nini alifukuzwa ukurugenzi wa AICC kwa kujilimbikizia mali ?,alifukuzwa na Juliasi Nyerere.

  2.Kwa nini alijiuzulu kwa sakata la Richmond ambalo nyie mnadai hakuhusika,na kwa nini ameendelea kuficha ukweli hadi sasa kama ni mtu anayetakia mema taifa hili? mbaya zaidi kwa unafiki wake alidai anajiuzulu kwa sababu watu wanautaka uwaziri mkuu wake.

  3.Atakuwaje mkombozi wa pili na wakati amekuwapo kwenye serikali kwa miaka mingi sana na hatujaona "something so special" from him?.Afadhali hata magufuli tunaona impact kila sehemu anayoenda.

  4.Ni maamuzi magumu gani ambayo mnasema Lowassa ameyafanya? Usitaje kujiuzulu kwa sababu hayo pia ni maamuzi magumu kama ya jambazi anayeenda kuvunja nyumba ya mtu.Amejiuzulu ili kuendelea kulindana na aidha wezi wenzake au wazembe wenzake

  Until unijibu maswali haya kiufasaha,ntahamia rasmi kwenye kambi ya Lowassa.
   
 17. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,110
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Mbona unauliza jibu kwani kikwete anawalipa vp. Kuna mbuga, kuna madini, kuna mafuta na hata ww yuko tayari kukuuza
   
 18. bht

  bht JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Pasco huu uswahiba wa kubebeana zigo lote lile, kweli?
  Binafsi kama kweli alimbebea swahiba wake zigo la dhambi basi hatufai...
  Ndio maana kuna concept za reward and punisment; huwezi kuwa rewarded kwa kukosea au kuwa punished kwa kufanya kwa usahihi! Ningemuona wa maana kama tu angemwacha anayestahili adha u ajibebee adhabu yake, angekuwa katusaidia saaana watanzania...
   
 19. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,442
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeamini sasa kuwa Elimu ya Uraia ata hapa Jf inatakiwa kupewa kipaumbele. Unawezaje kusema eti EL alibebeshwa zigo la RICHMOND?Jiulize swali hili hapa,wakati wa sakata hilo EL alikuwa na nafasi gani serikalini na nini yalikuwa majukum yake?
  Unatuambia EL kabla ajawa PM alikuwa tayari tajiri..mh kwani mtu kuwa tajiri kwa njia zisizo halali mpaka awe mwanasiasa? Wakati ni PM aliwai tangaza mali zake kwenye public?
  Watu kama nyie ambao mnaishi by looking and on depending the layers of the events sioni ata aja ya kuwaruhusu kupiga kula maana ukipewa vizawadi basi unauza utu wako.
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  AK 2015 si mbali kama udhaniavyo, in just a twinkling of an eye 2012 will be right before you, na ukumbuke maandalizi yanahitajika ili 'uonekane' kwa hiyo usishangae watu walianza kupigana vikumbo mara tu baada ya 'uteuzi' wa 2010
   
Loading...