Mh. Dr. Mwakyembe ushauri huu muhimu

Mh. Dr. Mwakyembe ushauri huu muhimu

betlehem
Ndugu helewa somo hapo kuwa kikwazo ni DPP, Itakuwa yeye kila fahili likija Ushahidi hautoshi.
Ukumbuke kwamba watumishi wote wa umma wanaweza kuwajibishwa na viongozi wakuu wa kisiasa , hivyo hata kama tatizo ni DPP; Huyo DPP kuna mtu anayeweza kumuwajibisha lakini hafanyi hivyo, unadhani ni kwa nini? kama Mwakyembe ataendelea kujitahidi kuzuia mambo haya lakini kila akipeleka vielelezo polisi hakuna majawabu unadhani jitihada zake zinaweza kuzaa matunda?
 
Ingekuwa vyema pia kwenda kukagua akaunti za staff wote waliokuwepo siku hiyo km zilijaa mpunga wa ghafla ghafla
Inasemekana kwamba ilikuwa walipwe baadae. Mwakiembe anakuambia video zinaonesha siku hiyo waliokuwa wanabeba mabegi ni polisi badala ya loaders. Anakuambia mtu aliekuwa zamu kwenye screening aliondolewa na mwenzake, na alieingia akapitisha mzigo kisha akamuachia mwenye zamu kuendelea. Anakuambia picha za CCTV, zinaonesha askari polisi na askari wa kiwanja wakiusubiri mzigo kabla hata haujafika. Anaongeza kwa kusema wengi wanaonekana wakiwa wanahaha huku na kule kuhakikisha mzigo unapita salama. Sasa ujiulize kwa nini hakuna mtu alietoa taarifa hizo hadi mzigo ukakamatwa S.Africa! na kama mzigo usingekamatwa maana yake hizo picha zote za CCTV, zingebakia kuwa Movie .
 
Wakati mwingine naona fadhali afanye kazi km yy bila kushirikisha wengine. Jamii hii imeoza, ukimshirikisha mtu huyohuyo anakuwa wa kwanza kutoboa siri na kuivujisha maana mtandao wa mafisadi ni mkubwa sana.

Kwani hao wanaojidai eti mfumo shirikishi walikuwa wapi hadi majanga yatokee ndio eti wajidai ooh wao hawajashirikishwa?

Imefika wakati kwa viongozi jasiri km Dr.Mwakyembe kijitoa mhanga kwa manufaa ya Taifa. Najua kuna wanaokasirishwa sana nautendaji wake wako tayari hata kumtoa roho km walivyofanya kwa marehemu Sokoine. Ila kwa hali ilivyo sasa, unaweza mshirkisha mtu akakugeuka kabla hamjatekeleza mliyopanga.

Dr. endeleza wembe huohuo utapata tu wa kukuunga mkono na Mungu akulinde na akubariki kwa kazi nzuri tunayoiona na sio porojo za kisiasa za kujaza matumbo supu ya utumbo asubuhi na kupiga miayo km kiboko. Tunataka vitendo na siyo porojo porojo tu.
Mkuu kwenye taasisi kubwa kama serikali; mtu mmoja hata awe na nia nzuri kiasi gani na hata awe na uwezo mkubwa kiasi gani hawezi akafanya kazi peke yake na akafanikiwa. Ili nchi iweze kufanikisha jambo ni lazma kuwe na "Team Work". Sasa inapotokea kwamba mmoja anapambana wengine wanakwamisha ni ngumu kufanikiwa. Kadhalika ni kwa nini wanaokwamisha wasikwamishe kama wanaamini kwamba nao wataathirika na operesheni husika? Na kwa upande wa Mwakyembe; ni vipi ataweza kudhibiti hali ikiwa anaokabiliana nao ni watu anaofanya nao kazi na usikute wengene kulingana na hadhi zao, Mwakyembe anajikuta akiwa na "Horizontal relations"? Wewe jiulize tu kwamba kama Rais anasema anawajua wauza unga wakubwa halafu baada ya hapo anawaomba waache, halafu Mwakyembe yuko uwanjani anakaza kamba kukamata, Halafu askati wake wananunuliwa, na wakifanikiwa kukamata; kesi za wahalifu zinakwama halafu hamla la ziada, imagine!
 
mh. Waziri sio mkweli na hivi vita haviwezi kwasababu.

1: anajaribu kukata matawi na kuacha mizizi, hili liko wazi kuwa wanaokamatwa ni watu wadogo sana ambao kama waziri angekua na dhamira ya dhati wangetumika kama thread ya kukamata wahusika wakubwa, mfano wanaomfahamu Masogange watakubali kwamba hawezi kuwa na mtaji binafsi wa 6b za kuendeshea boashara ya madawa ya kulevya, so lugha rahisi ni kuwa wanatumwa na watu wenye uwezo. Hili jana kwenye kipindi cha jana alikwepa kulijibu baada ya mama mmoja kutoka morogoro kupiga simu na kumwambia waziri atumie hawa waliokamtwa kutaja wanowatuma, katika majibu yake akasema watu wanoawajua wauza unga wampelekee majina kwa sababu tunaishi nao mitaani tunawajua، haya ni majibu rahisi kwa waziri kutoa, lakini pia kwa nn asitumie majina ambayo rais alisema anayo?

2: kuna baadhi ya wanasiasa wengine bado wako kwenye serikali wengine wastaafu wamekua wakisema kuwa nchi itakuja kuongozwa na wauza unga, kwa tafsiri nyepesi tu ni kuwa either kuna 2015 presidential aspirant anafanya hii biashara au anaungwa mkono na watu wanaofanya biashara hii haramu, waziri hajatuambia kama hao wanasiasa wamehojiwa juu ya kauli zao hizo!!

3: mwakiembe ni mtu wa maneno, mtakumbuka wakati wa ripoti ya Richmond akisema kuna mengine hakusema ili kulinda serikali, juzi tena akasema kesho nitawataja wauza unga na picha zao ili wananchi wawajue, siku ilipofika akataja wafanyakazi wa uwanja wa ndege, sasa inawezekana hakujua vita hivyo ni vigumu kiasi gani.

Mwisho naungana wenzangu hapo juu kuwa waziri kama anadhamira ya kupambana na madawa ya kulevya basi yuko peke yeke, na inavyojulikana ili serikali ifanikiwe kwenye mapambano yoyote ile iwe ya umaskini au uharamia lazima ifanye kazi kama system, sasa kama anapambana peke yeke wenzake wanahujumu hata fanikiwa milele.
Yeah! uko sahihi sana mkuu. Mimi kinachonipa shida kupita vyote; ni pale ninapojiuliza; Ni nani huyu anayeweza kununua vyombo vyote vya usalama tena eneo nyeti kama uwanja wa ndege? Je mtu huyu serikali kuu haimfahamu? Kama inamfahamu, inamfahamu toka lini na imechukua hatua gani hapo kabla? na kama haimfahamu kwa nini? Zaidi ya hapo kuwakamata hawa waliohongwa haisaidii sana maana huyu anayehonga atahonga tena wengine.
 
Waziri Mwakiembe kwa mara kadhaa ameonekana akijitahidi kukabiliana na watu wanao ihujumu nchi hii;

Wakati Fulani akifanikiwa kiasi na wakati Fulani akikwama na mara nyingine kupata madhila kama wote tunavyo fahamu.Kauli ambazo amezitoa Waziri Mwakyembe jana wakati akihojiwa katika kipindi cha "Jenerali On Monday" kinachorushwa na Channel Ten ; zina nisukuma kuamini kwamba mzee wetu huyu (Mwakyembe) anahitaji ushauri makini ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi huku akibaki na hadhi yake ya kisiasa na kibinadamu.

Naamini ni sisi tunao weza kumshauri mzee wetu huyu.Katika mahojiano hayo nimejifunza mambo yafuatayo ambapo binafsi yana nitia woga sana.

Moja.Sio tu kwamba mwakyembe anafahamu na kukubali kwamba watu hawana imani na baadhi ya vyombo vya usalama ikiwemo Polisi; bali pia yeye mwenyewe anaonekana kutokuwa na imani na vyombo hivyo. kwa mfano, alipoulizwa kuhusu jinsi watakavyo washughulikia walio kamatwa na madawa ya kulevya JNIA, alisema ashafikisha kesi zote Polisi na kuongeza "Safari hii wakisema tena ushahidi haujakamilika na wakati kuna video mimi sitawaelewa".

Alipoulizwa kama mtu ana taarifa ya madawa ya kulevya apeleke wapi? Alisema "Apeleke kwa vyombo vya serikali,kama haviamini basi azilete kwangu" aliongeza tena "Safari hii wakileta upuuzi upuuzi wao; nitaleta video hapa channel ten watu waione". n.k Kwa ku yaangalia kwa makini majibu hayo ya Waziri Mwakyembe, ni wazi kwamba sio tu kwamba anafahamu kuwa watu hawa amini baadhi ya vyombo vya serikali ikiwemo Polisi (kwa kuwa ha viaminiki) bali pia hatayeye mwenyewe haviamini sawa sawa. Sasa yeye kama waziri kama haamini vyombo hivyo, na maana yake atakuwa kesha jaribu kuongelea hilo ndani ya Baraza la Mawaziri bila mafanikio, na sasa analisema hadharani;

Swali analopaswa kujiuliza ni je! Hata kama atakuwa anapelekewa taarifa yeye kama yeye huku vyombo vya usalama haviaminiki je! Ataweza kutekeleza majukumu yake kama waziri?

Mbili. Inaonekana kuna hali ya viongozi kuogopana wao kwa wao hata kama mmoja wao ni sehemu ya tatizo, wenzake wana muogopa kwa sababu ambazo sio za wazi sana (Pengine kwa kuwa wako ndani ya chungu kimoja). Kwa mfano Waziri mwakyembe amesema kuna kesi zaidi ya 36 ambazo amezifikisha Polisi ndani ya mwaka mmoja lakini hazina mrejesho.

Anasema kuna Begi lilikamatwa ndani yaEmirates siku nyingi zilizopita,lilikuwa lishaingizwa kwenye ndege huku likiwa na unga na tag iliyoonesha jina la mwenye begi lakini mpaka leo mwenye begi hajaonekana na yeye (Mwakyembe ) hajui kama begi hilo lipo bado, na kama lipo liko wapi.Anatoa mifano mingine kibao ya namna hiyo lakini hatimaye anahitimisha kwa kusema "Waziri wa mambo ya ndani anachapa kazi si mchezo. Namwamini sana nchimbi". Kimantiki mtu huhitimisha alichokiongea.

Sasa tukijiuliza ni kwa nini Mwakyembe Analalamika kwamba kati ya kesi zote 36 alizofikishaPolisi (Wizara ya mambo ya ndani) hazijaleta mrejesho halafu anahitimisha kwa kumsifu Waziri wa Wizara hiyo kwa kuchapa kazi? Ni wazi kuna hali ya kuogopana hivyo hata kama mtu anapigania haki ndani ya serikali hii ya CCM, anatakiwa awe anafanya hivyo huku akiipaka mafuta batili kiujanja sana kitu ambachoni hatari.

Tatu. Inaonekana Mwakyembe ana nia njema lakini kuna vitu vinamfanya kukwama na hivyo kujikuta nafsi ikimsuta. Kwa mfano alipoulizwa kuhusu kiwango cha madawa yanayopita KIA, alisema "Kia wanakamatwa sana na ndio maana wanapenda kupitishia dar" alipoulizwa kwamba kwa hiyo udhaifu uko Dar?Anasema " JNIA sio mchezo; anaetaka ajaribu aone".

Sasa ukiangalia kwa makini unakuta kauli hizi zinagongana zenyewe kwa zenyewe na tafsiri ninayo ipata hapa ni kuwa Mwakyembe angependa JNIA kuwe "Drugs free zone lakini anakwamishwa na wenzake" na hataki kukubali wazi kwamba anakwamishwa kwa sababu yeye ni sehemu ya mawaziri.

USHAURIWANGU KWA MWAKYEMBE.

1. Mimi ningekuwa ndio Mwakyembe; Ninge durusu na kujiridhisha kama bado inafaa kuendelea kufanya kazi na Baraza hili la Mawaziri na nikafanya kazi zangu kwa ufanisi, huku nikiitii dhamira yangu na kulinda hadhi yangu kama binadamu, mwanasiasa na mtanzania mzalendo. Kama nikiona sio ; basi ninge jiuzulu uwaziri .

2. Ninge jipima na kujiridhisha kama bado ninafaa kuendelea kuwa mwanaCCM katika mazingira haya! zaidi ya hapo, namtakia Mwakiembe kila la heri japo mmmh! Sijui...................!


Kama siyo Mwakyembe, nani mwingine atawaokoa watanzania. Hata kuupata huu uhuru ulionao mkubwa haikuwa kazi dogo. Kaza buti na wewe Betelehemu, Acha kukata tamaa. Hakuna vita rahisi duniani.
 
Ingekuwa vyema pia kwenda kukagua akaunti za staff wote waliokuwepo siku hiyo km zilijaa mpunga wa ghafla ghafla

Wanalijua hilo soo kitambo sana.
Hawa maharamia huwa hawaweki pesa benki <<Nadhani umeona picha ya Agness 'Masogange' Gerald>>. Huwa wanawekeza katika majengo na magari. Hawaweki benki kwa sbb ni rahisi sana kuwa tracked.
 
Ushauri wako kwamba angejiuzuru haufai, nahisi umetumwa!

Acha mambo yako bna,wewe mtu akitoa mawazo yake ametumwa..kwani wewe hujawahi kumtaka kiongozi ajiuzuru. Au unafikri kujiuzuru matusi?
 
Sijaanza kwa kusema ajiuzulu. Hujanielewa vizuri. Nimesema ajifikirie kama anaweza kuendelea kufanya kazi na watu anaofanya nao sasa. Ukumbuke kwamba kama unafanya kazi na watu ambao unatofautiana nao misimamo, fikra, hisia na malengo kwa kiwango kikubwa; ni vigumu kufanikiwa hata kama una nia njema. Ukumbuke kuwa kwa mfano anakuambia kapeleka kesi zaidi ya 36 polisi zenye ushahidi wa wazi lakini mpaka leo hamna feedback. wewe unadhani ni kwa nini? je katika mazingira ya namna hiyo; si ataendelea kupeleka kesi huku wenzake wanamzunguka?

anakupotezea muda huyo jamaa,yeye kama ana mawazo yake si ayaandke
 
Kama unamshauri ahame chama basi wewe hufai. Abaki huko huko apigane nao
Mkuu; unaweza kupambana na mtu unaekula nae na kulala nae chumba kimoja? Unaweza kupambana na mtu ambaye siku ya kupanga utekelezaji mtapanga namna ya kutekeleza kumbe mwenzako ndio ana mfadhili mnae taka kumthibiti? hivi wakati mkiwa kwenye kikao cha siri cha kumthibiti muhalifu unaweza ukaamini kwamba miongoni mwa washiriki( miongoni mwenu ) hawezi kuvujisha siri katika hali hii tunayoiona na kukuunga mkono kinafiki kumbe nyuma ya pazia anakung'ong'a? katika mazingira hayo ni rahisi kutoboa? any way ni mawazo yangu tu; na mimi pia nina uthaifu wangu na ndio maana nikasema tumshauri. Inawezekana kuna ushauri mwengine bora zaidi.
 
Acha mambo yako bna,wewe mtu akitoa mawazo yake ametumwa..kwani wewe hujawahi kumtaka kiongozi ajiuzuru. Au unafikri kujiuzuru matusi?
Halafu watu hawaelewi vizuri kitu kimoja; Haina maana kwamba mtu kujiuzulu ni lazma mpaka awe na kashfa. Hivi ni kwa nini Mwl. Nyerere alijiuzulu? wakati fulani pale inapotokea ukajikuta unawajibika kutekeleza majukumu yako lakini unaofanya nao kazi wanakukwamisha na wewe huna nguvyu ya kutosha ya kuwasukuma watekeleze, basi unaweza kujiuzulu ili kusukuma mamlaka husika ichukue uamusi mgumu. Si mnakumbuka Kujiuzulu kwa Nyerere kulisaidia na baadae Nyerere akapata heshima zaidi!
 
Tatizo baraza la mawaziri limelala,inabidi hiyo kampeni iwe ya mawaziri wote,sasa jana anamsifia Nchimbi halafu anawasema polisi ndio nini sasa..? Unaweza kumtenga Nchimbi na polisi kweli?
 
Kama siyo Mwakyembe, nani mwingine atawaokoa watanzania. Hata kuupata huu uhuru ulionao mkubwa haikuwa kazi dogo. Kaza buti na wewe Betelehemu, Acha kukata tamaa. Hakuna vita rahisi duniani.
Mkuu sijakata tamaa. Nataka tupate mbinu bora kabisa ya kuweka mambo sawa ambayo inaweza ikawa na ufanisi mkubwa. Hata askari wanapopigana, kuna muda hupeleka mashambulizi lakini wakiona mbinu haijakaa sawa wanarudi nyuma kidogo halafu wakija sasa usiombee kichapo chake.pia wanaweza wakatumia mbinu ya kuzunguka na kuzingira kabla ya kushambulia.Sio woga ni mbinu mkuu.
 
Hatajiuzulu....akisha sema wengi serikalini wananuka
Rushwa na walioko chini yake ATAWASHUGHULIKIA... sijaona point yako....ushauri upi...huna...many words...so akiwa hana imani na vyombo vya usalama AWAACHEEE...?? huna point...
Mkuu ninachosema kwa ujumla wake ni kwamba tutafute mbinu ya kushinikiza mabadiliko ya mfumo mzima kwa ujumla la sivyo Mwakyembe yeye tu kama yeye hawezi kufanikiwa hata kama ana nia nzuri ikiwa waliomzunguka (anaofanya nao kazi) ni tatizo.
 
Hapana kujiuzuru, nafikiri sisi kama watanzania tunahitaji kumlinda kwa udi na uvumba waziri huyu, nimependa ulivyochambua majadiliano ya jana kati ya dr na mtangazaji. Kitu kinachoniuma mimi ni kuwa hivi viongozi wengine hawayaoni haya mabaya yanayo yotokea? hivi hakuna hata kiongozi mmja toka ccm mzalendo ambaye angejitokeza hadharani kumuunga mkono dr? Hivi ccm na viongozi wote toka uhuru wa tanzania hakuna hata mmoja ambaye ana uchungu na taifa hili? Jamani huyu raisi wetu hivi ni raisi kweli? mi mbona naona kama nchi haina viongozi? inauma sana kwa nchi kama hii watu tumenyamaza tu,,watu wanawafahamu waovu wametulia tu.

NACHELEA KUSEMA KUWA BORA YA MISRI YATOKEE TANZANIA KULIKO HALI INAVYOENDELEA TANZANIA.
 
Hapana kujiuzuru, nafikiri sisi kama watanzania tunahitaji kumlinda kwa udi na uvumba waziri huyu, nimependa ulivyochambua majadiliano ya jana kati ya dr na mtangazaji. Kitu kinachoniuma mimi ni kuwa hivi viongozi wengine hawayaoni haya mabaya yanayo yotokea? hivi hakuna hata kiongozi mmja toka ccm mzalendo ambaye angejitokeza hadharani kumuunga mkono dr? Hivi ccm na viongozi wote toka uhuru wa tanzania hakuna hata mmoja ambaye ana uchungu na taifa hili? Jamani huyu raisi wetu hivi ni raisi kweli? mi mbona naona kama nchi haina viongozi? inauma sana kwa nchi kama hii watu tumenyamaza tu,,watu wanawafahamu waovu wametulia tu.

NACHELEA KUSEMA KUWA BORA YA MISRI YATOKEE TANZANIA KULIKO HALI INAVYOENDELEA TANZANIA.
Mkuu kwa hilo la kuombea ya Misri yatokee Tanzania Sikuungi mkono. Kinachofuatia sasa nchini Misri ni Kwamba Nchi ile inaenda kuwa nchi iliyokufa.Kuna hatari ya kuwa kama Somalia. Huo sio mfano wa kuigwa na watanzania hata kidogo. Tutafute mbinu nyengine ila kwa hiyo tutakuwa tunapambana na adui feki. Tukirudi kwenye hoja; Kuna kitu kinaitwa "State Capture" katika hali hiyo nchi hushikiliwa kwa remote control na makundi ya watu yenye maslahi flani. Makundi hayo yanaweza yasiwe yanaonekana ila matokeo yake yawe yanaonekana dhahiri. Miongoni mwa dalili zinazoweza kuonesha kwamba nchi imekumbwa na mkasa wa namna hiyo; ni pale unapoona yanatokea matukio yasiyokuwa ya kawaida, kwenye mazingira ambayo yasingetakiwa wala kufikiriwa kutokea, na ushahidi uko wazi lakini serikali haichukui hatua za wazi na za uhakika. Katika mazingira hayo ndipo unapoona hata wale wachache wenye nia nzuri kwenye system wanapata woga.Imagine mtu mmoja anaweza je kuwahonga wanausalama wa uwanja wa ndege na wakahongeka na hata wakasindikiza mzigo wa hatari badala ya kuukamata? ina maana huyo mtu anakuwa na nguvu kuliko serikali? Sasa nini Cha kufanya? ndo hapo sasa.
 
Pamoja na hayo yote aliyofanya ni muhimu wataalam wapitie mikanda iliyohifadhiwa katika computers wanaweza kugundua madudu mengi zaidi ya watu ambao wamekuwa wakipitisha madawa ya kulevya kabla hawajachoma moto JNIA
 
Mkuu, kuna watu huwa wanakurupuka sana. Usikute pia aliyempa taarifa hizo ni Polisi FEKI maana siku hizi wamejaa kweli mitaani. zamani tulikuwa tu tunasikia habari za maafisa usalama feki kumbe siku hizi mpaka mapolisi wapo feki, ma JWTZ nao wapo feki, si mnamkumbuka yule jamaa alipiga picha na GODBLESS LEMA?

Umesahau na yule traffic feki kule kinyerezi?
 
Back
Top Bottom