Anaandika Godbless Lema: Dhihaka dhidi ya Ukatoliki

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
51,917
Reaction score
101,412
Nina uhakika kinachoendelea dhidi ya Katoliki si mzaha wala burudani, bali ni dharau, dhihaka na kejeli ya wazi dhidi ya Katoliki na Imani ya Kikristo kwa ujumla. Hii ni hatua hatari sana kwa Taifa.

Mzaha wa aina hii hauwezi hata kufikiriwa kufanywa na vijana wa Kikristo dhidi ya taasisi za dini ya Kiislamu.

Hebu jaribu kufikiria, hata kwa sekunde moja, vijana wa Kikristo wajifanye Waislamu halafu waandamane hadi BAKWATA. Je, hali ingekuwaje? Jibu lake liko wazi, mambo yangechukua mwelekeo mwingine kabisa.

Leo watu wanaandamana hadi Ubalozi wa Vatican bila kizuizi chochote, huku vyombo vya dola vikitazama kana kwamba hakuna tatizo. Halafu bado mtu anataka kutuambia kwamba hili sio kazi ya dola wala uzembe wa makusudi?

Huu ni ukimya unaohatarisha Taifa. Serikali, kwa kuruhusu hali hii, mnafungua mlango mpana wa uharibifu wa amani na mshikamano wa kitaifa. Mnasahau jambo moja muhimu sana, ndani ya vyombo vya dola kuna Polisi, Usalama wa Taifa, na Jeshi na ndani yake kuna Wakristo wengi, wakiwemo Wakatoliki.

Kuendelea kudharau imani yao hadharani ni kuchezea hisia za hao . Hili ni jambo la hatari kubwa. Mkiendelea hivi, mtakuwa mnaandaa mazingira ya mgongano wa kijamii na kidini ambao matokeo yake yatakuwa mabaya mno kwa Taifa.

Onyo hili si la kejeli wala si la vitisho, ni mwito wa akili na busara. Acheni mara moja. Acheni kabisa. Rudisheni upumbavu huu nyuma kabla haujageuka janga la kitaifa.
 
Naona Inchimbi huko aliko anaona kwa macho yake mawili bila kumsahau mkuu wa majeshi sisi wengine hatuoni
 
Huyu Lema ni mpuuzi sana yaani yeye haoni makafiri wanavyoutukana uislamu huku mitandaoni BLADFAKEN...
 
Samia na Mwigulu wanatapatapa
 
Likikua ni swala la muda tu ukishajiingiza kwenye siasa na kufungamana na wanaharakati utadharaulika na watakukebehi tu hususan kwa kundi hasimu. Ndivyo ilivyo na ndio ukweli. KANISA likubali dhihaka mana limekubali kujiweka wazi kwa kila mtu.

Waliowatuma sio kwamba hawajui ni ujinga wanafanya ila imefanywa MAKUSUDI KABISA na matokeo yalitegemewa mwisho wa siku viongozi wa dini, wanasiasa, wanaharakati wote wamebaki kujadili na kuandika upuuzi siku zinaenda.

On the other side ni ujumbe serious unaotumwa kwa njia ya kijinga. Now Kanisa hata kama sio ndani ya nchi lazima litajiuliza imefikiaje kwenye huu ujinga na upuuzi linaofanyiwa na hapo busara itakua ni kutafuta walipojikwaa.
 
Huyu Lema ni mpuuzi sana yaani yeye haoni makafiri wanavyoutukana uislamu huku mitandaoni BLADFAKEN...
kenge we! Ngoma ya mtandaoni huishia mtandaoni, huoni hiyo ni vurugu? Watu wanajiendea tu ubalozini, mind kuwa hao si wakatoliki
 
Nyinyi Bakwata mnatukanwa kwa sababu ya njaa zenu na kujipendekeza kwenu kwa watawala ili mpewe ubwabwa. Usiwahusishe Waislam wote na Uislam kwa ujumla!

Mimi watu wangu wengi wa karibu ni Waislam! Ila hawaungi mkono huu ujinga wenu.
 
Chadema imeipeleka siasa chafu kwenye dini
 
Mungu turehemu sisi waja wako, tumeyasikia, tumeyaona, tutajibiwa nawe kabla ya majira na nyakati kutimia
 
Back
Top Bottom