Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,535
Waziri Mwakiembe kwa mara kadhaa ameonekana akijitahidi kukabiliana na watu wanao ihujumu nchi hii;
Wakati Fulani akifanikiwa kiasi na wakati Fulani akikwama na mara nyingine kupata madhila kama wote tunavyo fahamu.Kauli ambazo amezitoa Waziri Mwakyembe jana wakati akihojiwa katika kipindi cha "Jenerali On Monday" kinachorushwa na Channel Ten ; zina nisukuma kuamini kwamba mzee wetu huyu (Mwakyembe) anahitaji ushauri makini ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi huku akibaki na hadhi yake ya kisiasa na kibinadamu.
Naamini ni sisi tunao weza kumshauri mzee wetu huyu.Katika mahojiano hayo nimejifunza mambo yafuatayo ambapo binafsi yana nitia woga sana.
Moja.Sio tu kwamba mwakyembe anafahamu na kukubali kwamba watu hawana imani na baadhi ya vyombo vya usalama ikiwemo Polisi; bali pia yeye mwenyewe anaonekana kutokuwa na imani na vyombo hivyo. kwa mfano, alipoulizwa kuhusu jinsi watakavyo washughulikia walio kamatwa na madawa ya kulevya JNIA, alisema ashafikisha kesi zote Polisi na kuongeza "Safari hii wakisema tena ushahidi haujakamilika na wakati kuna video mimi sitawaelewa".
Alipoulizwa kama mtu ana taarifa ya madawa ya kulevya apeleke wapi? Alisema "Apeleke kwa vyombo vya serikali,kama haviamini basi azilete kwangu" aliongeza tena "Safari hii wakileta upuuzi upuuzi wao; nitaleta video hapa channel ten watu waione". n.k Kwa ku yaangalia kwa makini majibu hayo ya Waziri Mwakyembe, ni wazi kwamba sio tu kwamba anafahamu kuwa watu hawa amini baadhi ya vyombo vya serikali ikiwemo Polisi (kwa kuwa ha viaminiki) bali pia hatayeye mwenyewe haviamini sawa sawa. Sasa yeye kama waziri kama haamini vyombo hivyo, na maana yake atakuwa kesha jaribu kuongelea hilo ndani ya Baraza la Mawaziri bila mafanikio, na sasa analisema hadharani;
Swali analopaswa kujiuliza ni je! Hata kama atakuwa anapelekewa taarifa yeye kama yeye huku vyombo vya usalama haviaminiki je! Ataweza kutekeleza majukumu yake kama waziri?
Mbili. Inaonekana kuna hali ya viongozi kuogopana wao kwa wao hata kama mmoja wao ni sehemu ya tatizo, wenzake wana muogopa kwa sababu ambazo sio za wazi sana (Pengine kwa kuwa wako ndani ya chungu kimoja). Kwa mfano Waziri mwakyembe amesema kuna kesi zaidi ya 36 ambazo amezifikisha Polisi ndani ya mwaka mmoja lakini hazina mrejesho.
Anasema kuna Begi lilikamatwa ndani yaEmirates siku nyingi zilizopita,lilikuwa lishaingizwa kwenye ndege huku likiwa na unga na tag iliyoonesha jina la mwenye begi lakini mpaka leo mwenye begi hajaonekana na yeye (Mwakyembe ) hajui kama begi hilo lipo bado, na kama lipo liko wapi.Anatoa mifano mingine kibao ya namna hiyo lakini hatimaye anahitimisha kwa kusema "Waziri wa mambo ya ndani anachapa kazi si mchezo. Namwamini sana nchimbi". Kimantiki mtu huhitimisha alichokiongea.
Sasa tukijiuliza ni kwa nini Mwakyembe Analalamika kwamba kati ya kesi zote 36 alizofikishaPolisi (Wizara ya mambo ya ndani) hazijaleta mrejesho halafu anahitimisha kwa kumsifu Waziri wa Wizara hiyo kwa kuchapa kazi? Ni wazi kuna hali ya kuogopana hivyo hata kama mtu anapigania haki ndani ya serikali hii ya CCM, anatakiwa awe anafanya hivyo huku akiipaka mafuta batili kiujanja sana kitu ambachoni hatari.
Tatu. Inaonekana Mwakyembe ana nia njema lakini kuna vitu vinamfanya kukwama na hivyo kujikuta nafsi ikimsuta. Kwa mfano alipoulizwa kuhusu kiwango cha madawa yanayopita KIA, alisema "Kia wanakamatwa sana na ndio maana wanapenda kupitishia dar" alipoulizwa kwamba kwa hiyo udhaifu uko Dar?Anasema " JNIA sio mchezo; anaetaka ajaribu aone".
Sasa ukiangalia kwa makini unakuta kauli hizi zinagongana zenyewe kwa zenyewe na tafsiri ninayo ipata hapa ni kuwa Mwakyembe angependa JNIA kuwe "Drugs free zone lakini anakwamishwa na wenzake" na hataki kukubali wazi kwamba anakwamishwa kwa sababu yeye ni sehemu ya mawaziri.
USHAURIWANGU KWA MWAKYEMBE.
1. Mimi ningekuwa ndio Mwakyembe; Ninge durusu na kujiridhisha kama bado inafaa kuendelea kufanya kazi na Baraza hili la Mawaziri na nikafanya kazi zangu kwa ufanisi, huku nikiitii dhamira yangu na kulinda hadhi yangu kama binadamu, mwanasiasa na mtanzania mzalendo. Kama nikiona sio ; basi ninge jiuzulu uwaziri .
2. Ninge jipima na kujiridhisha kama bado ninafaa kuendelea kuwa mwanaCCM katika mazingira haya! zaidi ya hapo, namtakia Mwakiembe kila la heri japo mmmh! Sijui...................!