Mh! Aunty amekua auntiii

Anita Kajembe

JF-Expert Member
Jun 29, 2021
215
485
Baba Jayrose na mama Jayrose waliona 2005. Wakati huo mama Jayrose amemaliza form six lakini changamoto za maisha zilikua nyingi na alikubali kuolewa. Baba Jayrose ni muajiriwa wa kampuni ya Umma.

Baada ya mama Jayrose kupata watoto wawili, waliamua aende chuoni. Pale kazini kwa Baba Jayrose kuna mama Kukuku ambae mtoto wake Kikuku anasoma Afrika ya Kusini. Kikuku alimsaidia uncle kupata admission ya aunty ambae ni mama Jayrose.

Siku ya safari ilipowadia baba Jayrose alimfahamisha Kikuku ujio wa aunty, alikubali kumpokea airport. Baada ya kupokelewa Airport, Kikuku alimpeleka aunty ghetto kwake huko aliandaa chakula ná vinywaji kwaajili ya mgeni.

Inavyosemekana baada ya kula na kunywa aunty Kikuku na aunty walilala pamoja mpaka asubuhi. Baada ya hapo aunty na Kikuku waliishi pamoja kama mke na mume.

Baba Jayrose ghafla aliamua kufunga safari. Mama Kikuku alizipata habari kutoka kwa Oga Kwatakwata kwamba Baba Jayrose ameomba likizo. Alimstua aunty na haraka aunty alitafuta apartment na kumsubiri mgeni.

Baada ya ugeni kuishi, baba Jayrose alitudi nyumbani. Likizo ilipofika mana Jayrose alirudi nyumbani. Akitegemea anarudi chuo kuendelea na mwaka wa pili. Kwa taharuki baba Jayrose alimfahamisha kuwa hakuna safari yeyote zaidi ya kufunguliwa duka kujengewa banda la kuku.

Aunty aligeuka kuwa auntii wa Kikuku.
 
Mtoa mada
IMG-20210708-WA0013.jpg
 
Oga Kwatakwata is like a quantum level virtual particle that pops from nowhere and diappears to nowhere in an instant.
 
Back
Top Bottom