Mgonjwa wa nne aliyepona UKIMWI

May 13, 2014
90
100
Habari gani ndugu zangu wanajamvi la Habari Mchanganyiko.

Habari zetu zinaanzia huko carlfonia, Marekani ambako mgonjwa wa HIV ambaye ametumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI, almaarufu kama ARV, kwa muda mrefu takribani miaka 30 sasa amekutwa hana Virusi hivyo.

Hiyo imetokea baada ya Mgonjwa huyo kufanyiwa matibabu ya vipandikizi kwenye Uboho baada ya kukutwa na Saratani ya Damu ijulikanayo kama Leukemia.

Madaktari waliokuwa wakimhudumia, wamedai kuwa mgonjwa huyu baada ya kimpandikiza na Uboho (Bone Marrow) hali ya mgonjwa ilizidi kuimarika na baada ya kufanya vipimo vikaonesha kuwa vijidudu hivyo havipo. Na hii imetokea baada ya kujiridhisha kuwa Mchangiaji(Donor) wa Uboho anavinasaba ambavyo haviruhusu mashambulizi ya VVU kwa chembe chembe hai nyeupe za Damu (WBC).

Je, Ni nini hasa kinachomfanya huyu Mchangiaji asishambuliwe na VVU?

Kwa asili, chembe chembe hai nyeupe za mwili huwa na viini kwa juu viitwavyo CCR5 (CC Chemoreceptor 5) ambavyo kazi yake kubwa ni kuratibu mikusanyiko na mashambulizi yanayofanywa na Chembe chembe hai za mwili zinazoulinda mwili dhidi ya vimelea vinasbabisha maradhi mwilini.

Viini hivi viitwavyo CCR5 pia hutumiwa na VVU kama mlango (door) kuingia kwenye Chembe chembe hai Nyeupe za Damu (WBC). So kukiwa na mabadiliko kwenye viini hivi kirusi huyu hawezi kuingia ndani Seli za mwili hivyo hubaki nje akiwa hana madhara yoyote na hatimaye huharibiwa na Seli walinzi wa Mwili kama T - helper Cells, Microphages, dentritic cells na wengineo. Hatimaye mgonjwa anakua huru (remission) bila virusi hivyo.

Je, Nini huyu ni mtu wa Ngapi kutangazwa kupona?
Aaah huyu ni mtu wa nne kupona. Mtu wa Kwanza kabisa kabisa ni Bw. Timothy Ray Brown mwaka 2011 ambaye alijulikana kama Berlin Patient. Ambapo kuna watu wengine wawili ambao walikataa majina yao kutajwa na watatu akiwa ni huyu ambaye anatengenza jumla ya watu wanne kupona UKIMWI tangu ugonjwa huu uibuke miaka ya 1980.

Je, matibabu haya ya kupandikizwa yanaweza kutumika kama njia ya kutibu ugonjwa huu sugu?
Jibu ni ndio ila kwa masharti kuwa Chanzo cha Uboho kiwe ni mtu ambaye anamabadiliko kwenye viini viitwavyo CCR5 ambavyo ndio vitaenda kuwa mbadala wa Seli zinazoshambuliwa. Lakini pia, matibabu haya sio rahisi kufanyika kama inavyoweza kudhaniwa japo tafiti za kutumia vinasaba vya CCR5 vinaweza kutafitiwa kuweza kujua kama kuna namna ya kuvitumia ili kutumika kama dawa kwenye matibabu ya gonjwa hili Sugu.

Hivyo, nikusihi ndugu yangu mtanzania, endelea kuchukua tahadhari UKIMWI upo. Ahsanteni kwa kusoma uzi huu.

Karibu kwa Maoni maswali na Napongezi pia 😄

Chanzo cha Taarifa: BBC News Health.

41EE632F-F144-4BA0-95AB-EF506B5AF0CE.jpeg

📸: www.cdc.gov
 
Thank you very much for the research findings, it gives a good hope. However, I suggest, there should be an alternative word of bone marrow for its Swahili version. The current one does't sound good.
 
Thank you very much for the research findings, it gives a good hope. However, I suggest, there should be an alternative word of bone marrow for its Swahili version. The current one does't sound good.
Indeed, We need such changes though seahili misses vocabularies for Medical Terminologies.
 
Back
Top Bottom