Mgomo waalimu jumatano

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
SOURCE:Majira

CWT:Waalimu mgomo Jumatano
BARAZA la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) limeridhia mgomo usiokuwa na kikomo wa walimu nchi nzima uanze Jumatano ijayo, kutokana na Serikali kushindwa kuwalipa madai yao ndani ya kipindi cha notisi ya siku 90 waliyotoa.

Uamuzi wa kubariki mgomo huo ulifikiwa na kikao cha Baraza hilo kilichokutana mkoani Morogoro jana na kuhudhuriwa na wajumbe 80 kati 82 ambao wanaunda chombo hicho.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Rais wa CWT, Bw. Gratian Mkoba, alisema kikao cha jana kilibariki rasmi mgomo huo na watarudi kazini baada ya kulipwa.

Alisema kutokana na maandalizi yaliyofikiwa, kuanzia Jumatano nchi nzima itazizima kwa mgomo huo.

Alisema ni wajumbe wawili tu wa Baraza la Taifa ambao hawakuhudhuria mkutano huo, ambao ni wa kutoka mikoa ya Rukwa na Singida kwa sababu maalumu.

"Wajumbe waliobaki walitoka mikoa iliyobaki na ndio wanakwenda kuwatangazia wanachama wetu waanze mgomo huo," alisisitiza Bw. Mkoba na kuongeza kuwa kuanzia leo, watakuwa wakifanya mawasiliano wa viongozi wa CWT ili kusuka mkakati ya kufanikisha mgomo huo.

Bw. Mkoba alionya kuwa katika kipindi cha mgomo Serikali isithubutu kuacha kuwapelekea mishahara yao benki, vinginevyo itakuwa haijipendi.

"Kama Serikali itaacha kuwapelekea walimu mishahara yao benki kwa sababu ya kuwa kwenye mgomo, itakuwa haijipendi na ndipo itakapoona nguvu zao (walimu)," alisisitiza Bw. Mkoba.

Alisisitiza kuwa walimu ndio wanaozalisha wataalamu, hivyo ni lazima waheshimiwe.

Katika kikao hicho, wajumbe wa Baraza la Taifa la CWT walilaani vitendo vya wizi wa mitihani ambavyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara.

Hata hivyo, walisema vitendo hivyo vinachangiwa na Serikali kutowatendea haki walimu. Walishauri watakaohusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Alipoulizwa kuhusiana na kuwapo taarifa za kutofautiana baina ya viongozi wa CWT, Bw. Mkoba alisema suala hilo nalo lilijadiliwa na wajumbe na kubaini kuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa, alisaini taarifa hiyo kwa ajili ya utekelezaji, lakini hiyo haizuii mgomo.

Wakati walimu wakiendelea na msimamo wao, juzi Serikali ilitoa taarifa ya kuunda Kamati ya Kuhakiki malimbikizo ya walimu ambayo itafanya kazi hiyo kwa kushirikisha CWT.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alisema Serikali imefikia hatua hiyo kutokana na madai ya walimu kuongezeka siku hadi siku.

Madai ya walimu yamegawanyika katika vipengele sita, lakini kikubwa zaidi ni kutaka kulipwa malimbizo yao na fedha za likizo, ambazo wamekuwa wakidai kwa muda mrefu.

Mara kwa mara CWT imekuwa ikivutana na Serikali kuhusu madai ya walimu, hatua iliyokilazimu chama hicho kutoa notisi ya siku 90 kwa Serikali kuwa imewalipa walimu madai yao. Notisi hiyo inamalizika Jumanne ijayo.

Haya wajameni, hali ndiyo hiyoooo
 
Last edited:
Hakuna lolote hawa walimu tangu mwaka jana wantishia kugoma lakini wakidanganywa kidogo na serikali mgomo unafutwa
 
Hakuna lolote hawa walimu tangu mwaka jana wantishia kugoma lakini wakidanganywa kidogo na serikali mgomo unafutwa

Lakini i believe Belo, mwaka huu they will for sure make it.We wait and see
 
Back
Top Bottom