Mgomo wa wahadhiri, ... any updates?

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Leo jumanne tarehe 27/4/2010 ndiyo siku ambayo wahadhiri wote wa vyuo vya umma nchini wanaanza mgomo wao wakiwa na madai mbali mbali. Kulikuwa na wasiwasi kwamba hawa jamaa wanatingisha kiberiti. Pia nasikia serikali ilifanya juhudi haramu kuwahujumu ikiwemo kufunga mitandao ya internet katika vyuo. Je, mgomo umefanyika kama ilivyopangwa? Na je, serikali itawasikiliza?
 
watakuwa wanagoma, si leo ndo wanaanza?!

gonja tusubiri updates hapa
nilio nao wasi wasi ni 2kta, wale wanaweza kulowanisha msimamo!
 
watakuwa wanagoma, si leo ndo wanaanza?!

gonja tusubiri updates hapa
nilio nao wasi wasi ni 2kta, wale wanaweza kulowanisha msimamo!

Nasikia SUA wamegoma na saa 4 asubuhi wanakutana na Mwenyekiti wa baraza la chuo ndugu Nicolaus Kuhanga. Agenda za mkutano hazijawekwa wazi.

Nilisikia kuwa hata Muzumbe nao walikubali kugoma. Haya ngoja tuendelee kusubiri.
 
Hawa wahadhiri si ndio walioponda mgomo wa TUCTA, nini kimewapata!
 
Ni kweli internet haiko poa hasa upande wa E-mail ndani ya website za vyuo.Hapa SUA kikao kinaendelea.Kuna nidhamu ya uoga inayoonyeshwa na maprof wetu hapa Tz, Kenya na Uganda hawani hio kunapokuja swala la maslahi yao wanaingia kwa mgomo.But ngoja tuone kama wanabeep au wataufanya kweli.
 
Ni kweli internet haiko poa hasa upande wa E-mail ndani ya website za vyuo.Hapa SUA kikao kinaendelea.Kuna nidhamu ya uoga inayoonyeshwa na maprof wetu hapa Tz, Kenya na Uganda hawani hio kunapokuja swala la maslahi yao wanaingia kwa mgomo.But ngoja tuone kama wanabeep au wataufanya kweli.

Ila nimeshangaa sana. Kama wamegoma si wangekaa home tu?. Kama kuna kikao si wakawatume wawakilishi wao?. Sina hakika kama hawa jamaa walikuwa wanajua hasa maana ya mgomo.

Anyway, ngoja tusubiri tuone nini kitatokea.
 
Aah walikuwa wanawapinga tucta, wakifikiri serikali itawapa ulaji. Sasa baada ya kuona serikali ikikwepa wajibu wake kwa waajiri wa umma na kulisukumia tatizo kwa waajiri binafsi, ndio wakashtuka. Ama kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu haramu. Nawashauri wahadhiri hawa wa vyuo vya umma katika mgomo wenu ongezeni na kipengele cha kutokumwalika kiongozi yeyote wa serikali kuwa mgeni wa heshima katika mahafali yenu ya kuhitumu, kuanzia na rais wa nchi. Hapo watatia akili!!
 
Hata wasomi hawa hawana msimamo katika kudai haki zao???????????
What about wakulima wenzangu ambao hutetema pale tu wamuonapo polisi????????????
Inafedhehesha kwelikweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mgomo bado upooooo ama walimtishia nyau mtu mzima??

Ni kweli wamegoma. Mgomo unahusisha vyuo vikuu vyote na vyuo vikuu vishiriki vya umma isipokuwa Muhimbili na Open University. Swali ambalo limebaki ni kama wataweza kuhimili vitosho vya dola na kuendelea na mgomo wao. Na je, utakuwa wa muda gani? Na je, wanafunzi wataamua kuwaunga mkono ingawa wao (wahadhiri) huwa mstari wa mbele kuwanyanyasa wanapogoma? Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom