Mgomo wa wafanyakazi

Ticha

Senior Member
Aug 26, 2007
135
8
Naomba tuwe na mshikamano katika hili kwani wafanyakazi wengi hasa walimu wana mafao finyu sana wengine hata malimbikizo yao hawajapata.
 
Mie natamani Tanzania Nzima tugome ..itasaidia sana kusolve matatizo yetu ..
 
mwaka huu lazima kieleweke
hasa suala zima la PAYE
na mifuko ya pensheni

unyonywaji tumechoka
 
Juzi yule m'babu wa chama cha waajiri amepinga mgomo na watu kibao wamemsapoti!...Kuna uwezekano wa mafanikio kwenye hili kweli?....Otherwise mgomo ni hatua ya muhimu sana kwa mfanyakazi, kama njia zinginezo muafaka zote zimeshindikana!!
 
Mazingira yasiyo salama ya kazi, tija pia (manake mie nalalamika kwamba sijisikii kama natumiwa ipasavyo atii!).
Pamoja kwa sanaaaaa! Tukimaliza wa maslahi tuanzishe wa kugomea wanasihasa!
 
Juzi yule m'babu wa chama cha waajiri amepinga mgomo na watu kibao wamemsapoti!...Kuna uwezekano wa mafanikio kwenye hili kweli?....Otherwise mgomo ni hatua ya muhimu sana kwa mfanyakazi, kama njia zinginezo muafaka zote zimeshindikana!!

mbabu ni yupi tena??

OFCOZ PJ hii maneno inachukua 'forever sasa bora tutunishe misuli sasa

jana kwenye habari nimesoma naona bado tunasuasua kusubiri 'ahadi' hewa za kila mei mosi

its like wanaenda kulainika hawa viongozi wa TUCTA
 
Mazingira yasiyo salama ya kazi, tija pia (manake mie nalalamika kwamba sijisikii kama natumiwa ipasavyo atii!).
Pamoja kwa sanaaaaa! Tukimaliza wa maslahi tuanzishe wa kugomea wanasihasa![/QUOTE]

kauli mbiu hapo zitakuwa nyingi tufanye kuchagua tu ipi irembeshe 'KAMUKUNJI' yetu
 
Nitashangaa sana kama walimi hawatagoma maana mazingira wanayofanyia kazi ni magumu mno.walimu wanateseka sana ofisi hazina meza, na ikumbukwe hizo ofisi ni madarasa so hazina hadhi kabisa kama za wafanyakazi wengine jamani.wanafanya kazi kwenye mazingira magumu mno hivyo wanahitaji mshahara wa maana sana.
 
Nitashangaa sana kama walimu hawatagoma maana mazingira wanayofanyia kazi ni magumu mno.
Mimi nitashangaa sana kama walimu watagoma, maana juzi juzi walimtosa Musiba kwenye mgomo wao. Walimu wetu hawa hawaeleweki kabisa!
 
Mgomo Tanzania hauwezi tokea. Watanzania waoga na pia wanaona aibu hata kudai haki za msingi. Mtu anaogopa kugoma akihofia kukosa kazi na kwa upande mwingine anaona akishiriki kwenye mgomo ataonekana amefulia. Unless tumebadilika na kuweza kujitolea kwa ajili ya wengine. Ndo mgomo unaweza tokea!
 
Mimi binafsi mtanzania nimemvualia kofia, hasa hasa sisi "WADANGANYIKA", wenzetu kule Zanzibar naona kama wana misimamo fulani wakati fulani. Linalonihusu hapa ni woga uliojengeka ndani ya mioyo na akili za watu. Kwa kweli huyu aliyeturoga tukafikia hatua hii ya akili zetu kuwa dhaifu kiasi cha kusahau na hata kutetea haki zetu alituweza.

Just imagine imagine katika kipindi cha miaka 5 baada ya uchaguzi mwananchi anataabika, hakuna ahadi zinazotekelezwa, kodi zetu zinaliwa na wajanja, hata wale tuliwapa dhamana ya kutulindilia hazina yetu wanaigeuka na kuanza kuitafuna. Lakini unapokuja wakati wa uchaguzi mtu anasahau kila kitu anachanganyikiwa na kuadaika na pesa/zawadi ndogo ndogo. Nina wasi wasi kama kweli hizi akili zetu zina uzalendon dani yake.

Kuhusa mada ya Mgomo, mimi binafsi ziwavunji moyo wale wachache wenye ujasiri, lakini nikionapo hapa serikali hii ilivyokuwa ya kisanii, itatoa vitisho na hata ikiwezekana kuwakamata viongozi wa TUCTA kama siom kuwaita chemba na kuwapatia fungu litakalowatoa umasikini, ambapo aidha hatutashangaa kusikia viongozi wakiahirisha mgomo, au wafanyakazi wachache kugoma.

Vinginevyo washikaji mgomo mwema
 
Back
Top Bottom