Mgomo wa wabunge hasa wa CCM

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
Wapendwa wakati tukijadili suala la mgomo wa madaktari ambao wamesimama kidete kutetea hali mbaya ya utoaji wa huduma za afya nchini, kuna tetesi kuwa kuna mgomo mkubwa wa wabunge hasa wa CCM ambao wameamua kutohudhuria bunge kwa kigezo chakukerwa na spika kuwashinikiza kukubali kila kitu hata kama ni cha uongo, ilimradi kimetoka serikalini.

Hii inadhihirishwa na uhudhuriaji mdogo sana wa wabunge hawa wa CCM hali ambayo imempa wasiwasi sana spika wa bunge Anna makinda hadi akatoa tahadhari kuwa serikali inaweza kushindwa kupitisha makadirio ya bajeti zake iwapo wabunge (hasa wa CCM) hawahudhurii.

Wabunge wa upinzani wanahudhuria wa kutosha kiasi kwamba kuna wakati wanawazidi wale wa CCM, hivyo kura ikipigwa wanaweza kushinda(Wale mnaoangalia bunge ni mashahidi wa jambo hili).
CCM imetumia mbinu nyingi wakati wa kura ikiwepo mbinu ya kuwapigia simu wabunge wake waje upiga kura wakati wa kupitisha makadirio hata kama hawakuwepo wakati wa kuchangia.

Hali iliyopo ni kama ile ya madaktari kusaini asubuhi na kuondoka. Wabunge wa CCM wanafanya hivyo hivyo kuhakikisha wanalinda posho zao.
Mgomo huu pia nao unapaswa kujadiliwa na wote wenye akili.
 
Hawa wabunge wa CCM watakuwa wanafiki tena sana, kama wana nia njema na serikali yao wanaogopa nini kusema waziwazi kama jambo halina maslahi na Taifa?Hii mijitu ya ajabu sana.
 
Zile kura za ndiyo au hapana yakiwa Magamba mawili na Upinzani wote, utasikia waliosema ndio wameshinda. Mi nadfikiri kuna haja ya kurekebisha swala la upigaji kura bungeni liwe confidential zaidi kuliko ilivyo sasa.
 
Nimepata taarifa kuwa hata wale wa upinzani wanaoisapoti CCM nao wanafanya vivyo hivyo. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wakati wa kura unaitwa jina mmoja mmoja na unasema ndiyo au hapana. Hivyo kama wewe si "MWENZETU" tutakujua na ole wako uchaguzi ujao!! POSHO NA CHAMA KWANZA, NCHI NA WANANCHI BAADAE!
 
aise kweli naangalia star tv yaani viti vyeupeee ccm wote hakuna
Umeonaee!! Wengi wako mjini wanazurura zurura tu, hawana la kufanya maana wameshaambiwa ni lazima bajeti ipite na ole wake atakayeipinga!! Pia wameambiwa kuwa madaktari wanataka kuiangusha serikali (eti mgomo wao una siasa nyuma yake), ole wake anayewaunga mkono na kuletaleta hoja za kutaka kujadili mgomo wa madaktari!
 
Hivi hakuna sheria inayowabana Wabunge kuwepo Bungeni muda wote? Au namna nzuri ya kuwabana ni kwenye kusaini posho. Haupo imekula kwako.
 
Wapendwa wakati tukijadili suala la mgomo wa madaktari ambao wamesimama kidete kutetea hali mbaya ya utoaji wa huduma za afya nchini, kuna tetesi kuwa kuna mgomo mkubwa wa wabunge hasa wa CCM ambao wameamua kutohudhuria bunge kwa kigezo chakukerwa na spika kuwashinikiza kukubali kila kitu hata kama ni cha uongo, ilimradi kimetoka serikalini.

Hii inadhihirishwa na uhudhuriaji mdogo sana wa wabunge hawa wa CCM hali ambayo imempa wasiwasi sana spika wa bunge Anna makinda hadi akatoa tahadhari kuwa serikali inaweza kushindwa kupitisha makadirio ya bajeti zake iwapo wabunge (hasa wa CCM) hawahudhurii.

Wabunge wa upinzani wanahudhuria wa kutosha kiasi kwamba kuna wakati wanawazidi wale wa CCM, hivyo kura ikipigwa wanaweza kushinda(Wale mnaoangalia bunge ni mashahidi wa jambo hili).
CCM imetumia mbinu nyingi wakati wa kura ikiwepo mbinu ya kuwapigia simu wabunge wake waje upiga kura wakati wa kupitisha makadirio hata kama hawakuwepo wakati wa kuchangia.

Hali iliyopo ni kama ile ya madaktari kusaini asubuhi na kuondoka. Wabunge wa CCM wanafanya hivyo hivyo kuhakikisha wanalinda posho zao.
Mgomo huu pia nao unapaswa kujadiliwa na wote wenye akili.
Hakuna shida ndio uchaguzi waliochagua. Kazi kula na kuiba tu! tufe tu hadi 2015!
 
Tabu ya wabunge waliopatikana kwa rushwa ndo hio, hakuna kujali wala ulazima wa kuhudhuria bunge
 
Jaribu kutunga propaganda zenye akili kama zile walizotunga wenzako za kumteka Dr. Ulimboka au ile ya kuaminisha wananchi kwamba CCM inakufa. Lakini hii iko below standards.
 
Wapendwa wakati tukijadili suala la mgomo wa madaktari ambao wamesimama kidete kutetea hali mbaya ya utoaji wa huduma za afya nchini, kuna tetesi kuwa kuna mgomo mkubwa wa wabunge hasa wa CCM ambao wameamua kutohudhuria bunge kwa kigezo chakukerwa na spika kuwashinikiza kukubali kila kitu hata kama ni cha uongo, ilimradi kimetoka serikalini.

Hii inadhihirishwa na uhudhuriaji mdogo sana wa wabunge hawa wa CCM hali ambayo imempa wasiwasi sana spika wa bunge Anna makinda hadi aka
https://www.jamiiforums.com/forum.php
 
wameshagunduwa wanatumika kupitisha au kuhalalisha ulaji wa watu wengine
 
Wapendwa wakati tukijadili suala la mgomo wa madaktari ambao wamesimama kidete kutetea hali mbaya ya utoaji wa huduma za afya nchini, kuna tetesi kuwa kuna mgomo mkubwa wa wabunge hasa wa CCM ambao wameamua kutohudhuria bunge kwa kigezo chakukerwa na spika kuwashinikiza kukubali kila kitu hata kama ni cha uongo, ilimradi kimetoka serikalini.

Hii inadhihirishwa na uhudhuriaji mdogo sana wa wabunge hawa wa CCM hali ambayo imempa wasiwasi sana spika wa bunge Anna makinda hadi akatoa tahadhari kuwa serikali inaweza kushindwa kupitisha makadirio ya bajeti zake iwapo wabunge (hasa wa CCM) hawahudhurii.

Wabunge wa upinzani wanahudhuria wa kutosha kiasi kwamba kuna wakati wanawazidi wale wa CCM, hivyo kura ikipigwa wanaweza kushinda(Wale mnaoangalia bunge ni mashahidi wa jambo hili).
CCM imetumia mbinu nyingi wakati wa kura ikiwepo mbinu ya kuwapigia simu wabunge wake waje upiga kura wakati wa kupitisha makadirio hata kama hawakuwepo wakati wa kuchangia.

Hali iliyopo ni kama ile ya madaktari kusaini asubuhi na kuondoka. Wabunge wa CCM wanafanya hivyo hivyo kuhakikisha wanalinda posho zao.
Mgomo huu pia nao unapaswa kujadiliwa na wote wenye akili.

hahaha...
Wagome tu,watanzania tutawapa zawadi yao 2015!!!
 
Wanaoafiki waseme ndiyo.
Ndiyooo...

Na wasiyoafiki waseme hapana.

Hapanaaa aaaaaaa aaaa.

Nazani waliosema NDIYO wameshinda!!
 
Naunga mkono, nafikiri upigaji kura uwe wa siri kuna wabunge wengi wa upinzani au chama tawala wangependa kuwa tofauti na msimamo wa vyama vyao kwa maslahi ya watanzania lakini wanashindwa kwa sababu ya kura kuwekwa wazi. Ni wabunge wachache mfano wa CCM wanaweza kuwa tofauti na vyama vyao pale tu wanapoona wananchi wanagandamizwa, lakini kwa sasa unaona kabisa issue yenye makosa inakubaliwa hata na wasomi wanaojua lakini kwa kuwa ni chama mbele sheria zinapitishwa kiholela

Back
Top Bottom