Nani zaidi? Wananchi au Mafisadi? Watanzania ndugu zangu, tumeonewa kiasi cha kutosha, tumeibiwa kiasi cha kutosha, tumedanganywa kiasi cha kutosha, tumedhulumiwa kiasi chakutosha. Sasa tumechoka na ufisadi huu, upole wetu umetuponza, kinachotakiwa sasa ni sisi wananachi kushika hatamu ya nchi yetu wenyewe. Tutakuwa wajinga kuendelea kuongozwa na mafisadi. Natoa wito wa mugomo nchi nzima, tuandamane kwa amani kuonyesha mshikamano. Kuanzia kwa vyama vya wafanyakazi, wanafunzi, vikosi vyote vya ulinzi, wakulima, wafanyakazi nk. tuandamane mpaka hao Mafisadi wa achie ngazi. Inabidi wananchi tuwe na mshikamano, tuachilie tofauti zetu za kichama ilitukomboe nchi yetu inayouzwa na mafisadi. Naomba polisi, JWTZ, Usalama wa Taifa, tuwe kitu kimoja wachie raia wakomboe nchi yao, isitoshe nanyie ni nchi yenu.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Tanzania