Mgomo wa Mdaktari, Je ni Dhambi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Mdaktari, Je ni Dhambi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizamani, Jun 30, 2012.

 1. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika kutafutatafuta channel ya kuangalia, wakati nikimsubiri President kuhutubia taifa kama walivotangaza ITV na amabayo sijajua kama kaingia mitini au vipi, nimefungua channel ya ATN, nikamwona huyu mhindi akisema " repent for the sin of doctors, for their strike" nikajiuliza au huyu kakosa kitu cha kuhubiri. Mimi huyu baba na mkewe siwaamini amini sana kwani kuna ishu nilidili nao personally na niliona walivokuwa wanasema uongo kwenye jambo tulilokuwa tunalishughulikia.

  Wito:
  Kama ni mhubiri na huna jambo la kuhubiri ni vema usiseme tu kwa sababu unataka kusema.

  Hayo ni maoni yangu. Je kwako wewe?
   
 2. k

  keyjey Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya ni mambo ya Imani na kwa Imani yake
  huenda ndivyo anavyo amini.
   
 3. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Batili, dhambi na ni kazi ya wafuasi wa shetani.
   
 4. Umslpogaaz

  Umslpogaaz Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je mgomo wa serikali kususia kutoa huduma kwa wanachi wake walioiweka madarakani ni dhambi?
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Angeanza kwa kusema serikali itubu kwanza labda angeweza kunishawishi. Nikitazama maelfu ya watanzania tunakufa kutokana na kukosa huduma nzuri ya afya ya kiwango tunachokiweza (eg. vaccuum to rescue the new born child after inhealing amniotic fluid). Pia nikisikia ufisadi unaotukuzwa, utoroshwaji wa pesa na nyara za serikali ndiyo nachanganyikiwa zaidi. Serikali ingedhibiti ufisadi na viongozi wanaotorosha pesa za watanzania, wangeweza kuboresha zaidi huduma ya afya na nyinginezo nyingi.
   
 6. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhambi ni dhambi hata kama inatendwa na nabii. Kwa wanaoamini biblia, Yesu alimwambia pilato ...... Aliyenileta kwako yu na dhambi kubwa zaidi... Alikuwa akimaanisha kuwa yeye pilato kwa kumhukumu bila hatia yu na dhambi ila waliomfungulia mashtaka wana dhambi kubwa zaidi. Kwa hili la madoctor serikali inawajibika lakini madaktari wana dhambi kubwa ya kuwaacha wagonjwa wakijifia vitandani kwa madai yao wanoyodhani ni muhimu zaidi ya uhai wa mwanadamu. Kwanini waue watu hata ambao wangetibiwa kwa vifaa duni vilivyopo
   
 7. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lyimo... Naomba nikuelimishe, katika nadharia ya uzalendo maslahi ya umma yanatangulia yale ya binafsi. Iwapo madaktari ni wazalendo wangeanza na kuboreshwa huduma na mazingira ya kazi bila kuunganisha na maslahi binafsi. Kiyaweka yote kwa pamoja hata asiyefikiri sana atajua tu kuwa la kuboresha huduma ni tactic ya kubuy public support kwa ajili ya kufanikisha lao la maslahi.. The end justidies the means.. or viceversa
   
 8. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Huyo Mhindi analinda maslahi yake binafsi, kaishiwa mbinu.
   
 9. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Lakini ndugu yangu Mnyampaa, tukiondoa unafiki madai yote kwa pamoja nisahihi. Kama utakuwa mfatiliaji mzuri wa sakata hili, kwanini serikali ilisimamisha stahiki za madaktarri tangu 2010 (document zipo, hata ukiomba humu JF utapatiwa). Sema tu, kutokana na madai haya yote kuletwa kwa pamoja, imekuwa ni rahisi kwa kuyapikia propaganda za kisiasa. Sijawahi kusikia kajibu ya serikali hata siku moja yakielezea kuhusu kuweza/kushindwa kuboresha mazingira ya afya. Majibu ya Serikali yamekuwa ni kuhusu maslahi makubwa ya madaktari na kuyalinganisha na ya watumishi wengine ili waweze kuchonganisha madaktari na wananchi. Ingekuwa madaktari ni chama cha kisiasa tungekubali kuwa wameweza kupiga propaganda na kuwapikia fitna madaktari ili wananchi wasiwakubali. Sasa unaweza kuniambia ni vipi serikali imeweza kulishughulikia swala hili bila ya athari? Na je ni lini tutaanza kuwa na uhakika wa kusimamiwa afya zetu na serikali tuliyoipa dhamana? Kipaumbele cha kodi zetu kiko wapi? nk?
   
Loading...