utantambua
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,367
- 321
Hivi wana jf,lazima mtu afanyie intern mhimbili?akienda hospitali nyingine kuna tatizo gani?au hawa intern wanataka kwenda kufanya operation ya kichwa badala ya mguu kama siku zile?
Au ndio ule mtizamo kuwa lazima uishi dar na ufanye kazi dar ndio mambo yako yatakunyookea?ukienda mkoa una loose?
wasomi wetu wanatuangusha sana,sasa kama wao wanakuwa walalamikaji kama sisi,je nani atamsaidia mwenzake?nani atamuongoza mwenzake?
mi nawaomba hawa Intern wawe flexible,maisha popote,tena wao kutokana na elimu yao wakienda mikoani watafanya kazi vizuri sana maana kwanza kuna upungufu mkubwa wa wataalam hivyo watakuwa potential sana.
Acha kutoa tuhuma zisizo na mpango, hoja ya madaktari kufanya mazoezi muhimbili ama hospitali nyingine aliyoichagua kwa mujibu wa chama cha madaktari ni kwamba kila daktari huwa na ndoto za kuwa nani hapo baadae yaani za kubobea katika kijieneo fulani, na hivyo huenda kufanya mazoezi katika hospitali ambayo anaamini ina utaalam na vifaa ambavyo vitamsaidia kufikia malengo hayo. Kwao sio suala la kukaa Dar es Salaam bali ni hospitali gani inaweza kuwafanikishia malengo yao. Halafu kwa nini hujiulizi serikali iliwaruhusu kwenda kufanya mazoezi hapo Muhimbili halafu leo baada ya kuingia nao mgogoro ing'ang'anie kuwabadilishia vituo, ili iweje? Kuwakomoa?