Na ndiyo enzi sahihi sasa! Enzi za kuumizana, kutesana, kuuana, kutishana, kupotezana, kudhulumiana, kuabudiana, kutukuzana, kusujudiana, kubaguana, nk. Hazina tija kwa ulimwengu wa sasa.
hakuna cha enzi yoyote, haya yote ni madhara ya utawala wa CCM kutawala kwa aina ile ile miaka nenda rudi - Kwa mfano Halmashauri iliyoongozwa na CCM miaka yote Temeke na sasa Kigamboni hawakujua watahitaji eneo kubwa la stand maeneo ya pale ferry ?
Na ndio matatizo ya kuongoza nchi kibabe bila kufuata taratibu. Wapinzani walipokuwa wanasema nchi iendeshwe kwa kufuata taratibu mlikuwa mnasema kuwa wanatumiwa na mabeberu, ikawa nchi nzima inafuata maamuzi ya mtu mmoja hata kama ni ya ovyo (kama kuruhusu wamachinga kila mahali)
Na ndiyo enzi sahihi sasa! Enzi za kuumizana, kutesana, kuuana, kutishana, kupotezana, kudhulumiana, kuabudiana, kutukuzana, kusujudiana, kubaguana, nk. Hazina tija kwa ulimwengu wa sasa.
Kwa nilivyockia mm mabas yote yanayotoka sehem zote lazima yapitie pale fery kushusha abiria ambao wanavuka kwa panton, n wanaotaka kupanda yale y machinga wanapelekwa mpaka apo tungi
Migomo na maandamano ni njia ya wananchi husika kufikisha ujumbe.
Wenye mamlaka wakae nao watatue changamoto zao.
Vitisho, Kuvunja kibabe maandamano na migomo ni dalili ya serikali isiyo fuata utawala wa sheria.
Naamini hali hii ingetokea miezi michache nyuma viongozi wa huo mgomo tungewatafuta kwenye fukwe za bahari.
Kigamboni kwa sasa ina wakazi wengi sana,ile stend mwanzo ilikua inaleta shida ata kwa watembea kwa miguu,maana daladala ni nyingi,ila waliko amishiwa ni mbali,navy pale kuna kubwa tu sema ndo hivyo eneo LA jeshi haliguswi,